WEWE NI NANI MPAKA UMFANYE MUNGU WA ZIADA
💫 WEWE NI NANI MPAKA UMFANYE MUNGU WA ZIADA ❓*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
💫 Huna mda hata wa kumtunikia Mungu unasingizia biashara na chaajabu biashara yako haiingizi hata 50000 kwa siku tayari umeringa na kumsahau Mungu .
💫 Wewe ni muuza chakula tu gengeni unaacha kwenda ibadani .Eti upo busy unatafta pesa mambo ya Mungu badae hivi unajua kuwa hata kwenye hicho kibanda amekuweka Mungu ❓
💫 Wapo watu wakubwa sana makanisani wamefanikiwa na hawajaacha kumtumikia Mungu kwa sababu ya mali zao wewe umepata kazi mda mfupi tu umemdharau Mungu na kumfanya wa ziada .
� Vipi kuhusu wanasheria na madaktari wapiga vinanda makanisani , je huwaoni hao ❓
Mbona hawajamfanya Mungu wa ziada ❓
Wewe ni nani mpaka umfanye Mungu wa ziada ❓
💫 Kwanini unasoma neno siku ya ibada hadi siku ya ibada tu ❓
Au huoni kuwa umemfanya Mungu ni wa ziada ❓
💫 Je haujui kuwa imeandikwa ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu ❓
👉🏻 Sizungumzii nguvu za kimwili nazungumzia nguvu za kiroho yaani wale wafanyao kazi ya Mungu kwa bidii watauteka ufalme wa mbinguni .
💻 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Mathayo 11:12
💫 Kazi ya Mungu ni ya kwanza kabisa tena ipangie mda wa kutosha maishani mwako .
💫 Jifunze kumwomba Mungu kwa kila ufanyalo na kumshukuru pia naye atakubariki zaidi .
💫 Wapo watu watakufa maskini kwa sababu hawamtii Mungu wamemfanya kuwa wa ziada .
💫 Mungu anawaangalia na kusema ,
👉🏻 Mtu huyu nimemfanikisha kidogo tu kanisahau nikimpa utajiri si ataniasi huyu
Simpi utajiri wangu huyu
🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂
💫 Saivi tu umeanza kuacha kanisani ukidai kazi nyingi miradi yako itasimama , nakwambia hiyo miradi itakufa mpendwa kama hutamtii Mungu .
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
💫 Mungu anakanuni za kumfanya mtu awe tajiri .
1⃣ Anataka umtii
👉🏻 Umtumikie ndiyo akuzidishie mali zako
Usipo mtumikia kwa bidii utakuwa hupigi hatua kiuchumi kila siku wewe kukicha unakula matembele tu
🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂
💫 Mwangalie Ibrahimu jinsi alivyokuwa mtii hakumwacha Mungu kwa sababu ya vitu alivyonavyo .
💻 1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Mwanzo 17:1
2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
Mwanzo 17:2
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
Mwanzo 17:6
💫 Mtumikie Mungu kwa bidii na kutenda mema
💫 Mungu anakuangalia je , umejitoa kwake ❓
Kama hutaki kumtumikia na kumheshimu kukupa utajiri sahau kabisa .
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
💻 1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
Kumbukumbu la Torati 28:1
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 28:2
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Kumbukumbu la Torati 28:3
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Kumbukumbu la Torati 28:4
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
Kumbukumbu la Torati 28:5
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
Kumbukumbu la Torati 28:6
7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Kumbukumbu la Torati 28:7
8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 28:8
💫 Usipomtumikia na kumheshimu atakuacha kwenye maisha ya tabu sana , anakubakiza kiwango ulichonacho hakuzidishi mpaka utakapoamua kutii ndyo atakupandisha zaidi .
💻 34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
Danieli 4:34
36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.
Danieli 4:36
2⃣ Utoaji
👉🏻 Hii ni kanuni nyingine ambayo inamfanya Mungu akuinue kiuchumi
💫 Utoaji siyo sadaka tu , hata kuwasaidia wasiojiweza , yatima na wajane ni sehemu ya utoaji pia .
👉🏻 Kuna watu wamebakia maisha ya mateso kwasababu siyo watoaji
Katika
✍🏻 Zaka
✍🏻 Kusaidia yatima na wajane
✍🏻 kusaidia wagonjwa
Hivi vitu ni vizuizi kwako usiinuliwe kiuchumi .
💫 Mungu anaangalia na kusema
Hivi tu nilivyomfanikisha amesahau watu na kuwapita hawajali
Nikimzidisha si atanyanyasa watu huyu ❓
Simpi utajiri nimwache ahangaike na umaskini asiniasi .
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
💻 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malaki 3:10
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 3:11
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Malaki 3:12
💫 Kama nilivyosema mwanzo kuwa utoaji wako mbele za Mungu uambatane pia na kusaidia watu wenye shida mbalimbali ambao hawajiwezi .
💻 1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Matendo ya Mitume 10:1
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Matendo ya Mitume 10:2
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10:4
💫 mwangalie Kornelio jinsi Mungu alivyombariki na kumkuza kiuchumi kwa sababu tatu .
1⃣ Kumcha Mungu
2⃣ Kumtolea Mungu
3⃣ kusaidia watu
👉🏻 Hata kumwambia mtu fanya hiki ni kumsaidia pia .
Mungu akubariki sana
Tutaendelea siku nyingine
Maoni
Chapisha Maoni