GIZA LINALOZUIA KUZIONA BARAKA ZA MUNGU
GIZA LINALOZUIA KUZIONA BARAKA ZA MUNGU
UTANGULIZI
Katika
kitabu hiki, natumaini wewe unayesoma utapata maarifa zaidi yatakayokusaidia
kutatua changamoto za kiroho zinazo watesa watu wengi katika maisha yao
kutokana na matendo ya giza yanayowazuilia wasimwone Mungu akitenda katika
maisha yao.Nilikuwa natafakari sana wakati nataka kuandika kitabu hiki cha
kwanza katika maisha yangu ya wokovu.Siku moja Roho wa Mungu akanipa msukumo wa
kuandika kitabu hiki ili kiwasaidie watu katika kuzijua siri zilizofichika
katika maisha ya mtu juu ya kutenda matendo ya giza yaani maovu ambayo yamekuwa
kikwazo kwa watu wa Mungu katika safari
yao ya wokovu.Mfumo wa maisha ya mtu unaweza ukaathiri mambo mengi sana katika
maisha yake hasa katika maeneo matatu yanayohusu maisha yake akiwa hapa duniani
yaani Ukuaji wa kiroho , Uchumi,Afya na hali ya ndoa .
Matendo mabaya (matendo ya Giza) ni kizuizi
cha kupokea baraka kutoka kwa Mungu.Matendo hayo ndiyo yamekipa kitabu hiki
jina liitwalo “Giza linalozuia kuziona baraka za Mungu” hii ndiyo sababu ya
kuandika hiki kitabu.
“Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi
na tuyavye matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.”
Warumi 13:12
Maovu yanamtia mtu
giza katika macho yake ya kiroho asizione baraka za Mungu, yanamfanya Mungu asitimize
ahadi aliyomwekea mtu katika maisha yake.
10 Macho yao yatiwe giza ili wasione,
Ukawainamishe mgongo wao siku zote.
Warumi 11:10
Giza la
dhambi linamfanya mtu asione baraka zake na apoteze dira ya maisha yake.
35Basi Yesu akawaambia, Nuru
ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza
lisije likawaweza; maana aendaye gizanihajui aendako.
Yohana 12 :35
Waliokaa katika giza na uvuli
wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma,
Zaburi 107:10
Pia
tunajifunza kuwa matendo ya giza yanamfanya mtu aishi maisha ya tabu na mateso
kwa sababu Mungu amezuilia ahadi ambayo alikuwa amekusudia kumpa huyo mtu.
Mungu akubariki sana.
SURA YA KWANZA
UASHERATI NA UZINZI
Uasherati na uzinzi ni giza linalozuia watu wengi wasione Baraka za MUNGU, uasherati na uzinzi unamzuia mtu katika Nyanja kuu tatu.
1.kukosa ibada
Uaesherati unamfanya mtu akose mda mzuri wa kuwa karibu na Mungu hii ina maana kwamba uasherati na uzinzi ni giza linalomfanya mtu asimwone Mungu.
Tafiti za kiroho zinaonyesha vijana wengi walioangukia kwenye uasherati na uzinzi wamepungukiwa uwezo wa kufikiri mambo ya Mungu yaani ufahamu wao juu ya sheria za Mungu umefinywa kwasababu akili zao zimetiwa giza.
EZEKIELI 23:18
“Basi alifunua uzinzi wake, na kufunua uchi wake;ndipo roho yangu ikafarakana naye, kama ilivyofarakana na umbu lake.”
Uzinzi unufanya
moyo wa mtu ufarakane na Mungu na kumwacha atembee
katika matendo yake ya giza ambayo mwisho wake ni uangamivu.
Kwahiyo uaesherati na uzinzi ni giza limfanyalo mtu asiwe karibu na Mungu na mtu akiwa mbali na Mungu hawezi kuona Baraka.
Wengine watauliza mbona waasherati na wazinzi wanaongoza ibada kanisani?
Mpendwa nataka ujue kua sio kila ummwonae kanisani ni mwana wa nuru wengine ni wana wa giza ingali wanazijua sheria za Mungu lakini ni masinagogi ya shetani.
Hukumu inakuja tena kali kwa wale wanaoijua sharia ya Mungu na kuivunja huku wakitembea gizani.
LUKA 12:47
“ Na mtumwa yule aliejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, walakuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.”
2. Kupungukiwa muda wa kusoma neno la Mungu
Hili pia ni giza linalokumba vijana wengi leo. Wameshindwa kusoma
neno , wanatafakari mambo ya zinaa. Hili jambo linawafanya wakose Baraka za Mungu.
3. Vifungo na maagano ya uasherati na uzinzi.
Hili pia ni giza ambalo linazuia vijana wengi hata kwenye kuoa na kuolewa, giza hili linazifunga ndoa za vijana wetu leo waishi maisha duni na kuingia kwenye mafarakano.
Vijana wengi husema ndoa ni ngumu kumbe wao ni wagumu lakini ndoa ni rahisi na ina raha sana, tatizo ni kwamba wanandoa mmeingia kwenye ndoa kila mtu kabeba roho chafu kutoka kwa wapenzi wake hizo roho zimezuia ndoa yenu Mungu asiibariki.
Mungu hawezi kuwamwagia Baraka kama hamjazivua roho za wapenzi wenu wa zamani, roho hizo ni giza linalozuia ndoa yenu isibarikiwe.
1 WAKORINTHO 6:16
“Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, wale wawili watakuwa mwili mmoja.”
Pia kuoa na kuacha mke au kuongeza
wake wengineni giza linaloua maisha ya mtu asifanikiwe katika viwango ambavyo
Mungu anataka.
ZABURI 107:10-12
“waliokaa
katika giza na uvuli wa mauti, wamefungwa katika taabu na chuma, kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, wakalidharau shauri
lake aliye juu. Hata akawadhili moyo kwa taabu, wakajikwaa wala hakuna msaidizi.”
SURA YA PILI
KUTUMIKIA MIUNGU MINGINE
Kutumikia miungu mingine ni giza kubwa ambalo linamfanya mtu asione Baraka za Mungu.
KUTOKA 20:4-6
“usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho
juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu
maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”
Kutumikia miungu mingine ni hasara kubwa sana katika maisha ya mtu. Kutumiki miungu mingine huleta uangamivu na mateso katika maisha ya mtu.
WAAMUZI 2:11-15
“Wana wa Israeli
walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya
Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba
zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine,
baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote,
wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali
na Maashtorethi. Hasira ya
Bwana ikawaka juu ya Israeli,
naye akawatia katika mikono ya watu
waliowateka nyara, akawauza na kuwatia
katika mikono ya adui zao pande
zote; hata wasiweze tena
kusimama mbele ya adui zao. Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana
alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.”
Baada ya kufa Yoshua, Israeli waligeukia miungu mingine wakaacha kumtumikia Mungu aliye watoa
utumwani misri.
Angalia mateso waliyoyapata baada ya kumsahau Mungu, yaani
Mungu aliwatia mikononi mwa adui.
Kwa maana hii Mungu aliwaacha hakuwalinda na
adui nao wakaingia kwenye mateso makali sana.
WAAMUZI 10:10
“Ndipo wana wa Israeli
wakamlilia Bwana, wakisema, Sisi tumekufanyia
dhambi, kwa sababu
tumemwacha Mungu
wetu, na kuyatumikia Mabaali.”
Angalia jinsi walivyotumikishwa na adui
mpaka wakaamua kumrudia Mungu.
1 SAMWELI 7:3-4
“Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia
Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa
katika mikono ya Wafilisti.Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake.”
Najua siku za leo ni vigumu kuona kuwa Mungu amekutia mikononi mwa adui pale unapomsahau na kutumikia miungu mingine.
Ishara zifuatazo utaziona kwa wale wanaotumikia miungu
mingine.
• katika uchumi utaona mtu hafanikiwi na hata akifanikiwa kwa Baraka
za kipepo bado uchumi wake hautadumu. Uchumi bila Baraka za Mungu haudumu.
• katika afya utaona mtu ana mali lakini magonjwa kwake ni rafiki
sana. Hii ni kwa sababu wamemsahau Mungu na
kugeukia miungu mingine.
KUTOKA 23:25-26
“Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula
chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.”
Ukiona familia inatumikia miungu mingine ujue Baraka za
Mungu hazipo na roho za magonjwa na vifo huibuka sana.
• katika elimu utaona watoto wengi wanaotoka
katika familia za wanaotumikia miungu mingine hawana akili darasani wao ni kufanya
vibaya tu. Hii ni kwa sababu ndani yao hakuna maarifa yatokayo kwa Mungu.
MITHALI 1:7
“Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na
adabu.”
Kutokumtumikia Mungu ni giza
linalozuia Baraka za Mungu kumfikia mtu katika elimu.
Angalia mikoa ambayo kuna uganga na uchawi mwingi kiwango cha elimu
kipo duni sana na waliosoma ni wachache sana. Linganisha watoto wanaotoka katika familia za wacha Mungu na za wanao abudu miungu
mingine utaona kuwa kuna wasomi wengi katika familia za
wacha Mungu,
kwa
sababu Mungu kafungua mlango wa Baraka
katika elimu na kuwapa
watoto uwezo wa
juu
sana katika masomo.
Kutumikia miungu mingine kuna mkosesha mtu Amani
kwa kuwa Mungu hayupo pamoja naye.
2 MAMBO YA NYAKATI 17:3-5
“Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za
kwanza za Daudi babaye,
asiyatafute mabaali;lakini alimtafuta Mungu
wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo
ya Israeli. Kwa hiyo Bwana akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati
akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele.”
Tunamtazama Yehoshafathi katika utawala wake alifanya
vizuri sana mpaka mataifa wakamletea zawadi hii ni kuashiria kuwa alikwenda katika njia
za
Mungu Baraka za
Mungu zikawa juu yake.
Epuka kutumikia miungu mingine maana kuna Baraka za kipepo ambazo ni za muda mfupi, mtumikie Mungu peke yake ili Baraka zinazodumu zikujilie.
Rejea kumbukumbu la torati 28:15
Kutumikia miungu mingine ni giza linalofanya Baraka za Mungu zisikufikie.
SURA YA TATU
KUTOKUSAMEHE
“Nanyii kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu;ili na baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Naomba nikukumbushe kuwa msamaha ni jambo kuu sana ambalo Mungu analiangalia katika maisha ya mwanadamu. Kama yeye Mungu alivyo na tabia ya kusamehe na kusahau ndivyo ilivyo na kwa mtu.
Kutokusamehe ni dhambi mbele za Mungu, dhambi hii inakufanya
wewe ukose baraka za Mungu maishani mwako.
Hata hivyo napenda kugusia juu ya sala ambayo wakristo wengi tunakiri tukisema.
“utusamehe makosa yetu kama tunavyowasemehe waliotukosea”
Jiulize mpendwa je, nimesamehe walionikosea, ndipo mwambie Mungu, “unisamehe makosa yangu kama ninavyowasamehe wanaonikosea”
MATHAYO 6:12-15
“Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Kwa maana mikiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Ni nini basi Mungu anataka ujifunze, anataka ujifunze kuwa usiposamehe
Mungu hawezi kukubariki kirahisi.
LUKA 11:4
“Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni lakini tuokoe na yule muovu”
Tujifunze kwamba mtu yeyote asiyesamehe bado yupo mikononi mwa shetani kwa hiyo inabidi ang’oe roho ya kutokusamehe ili Mungu amsamehe na kumrejesha kwake.
Imekuwaje basi kutokusamehe liwe giza linalo kuzuia baraka zako za Mungu kukufikia ?
Jibu ni kwamba kazi ya giza ni kumzuia mtu asione anachokitafuta.
Au ni nani aliye wahi kutafuta sindano gizani akaiona?
Kwa hiyo kutokusamehe kunamfanya mtu asione baraka za Mungu. Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni dhambi na dhambi ni giza.
LUKA 17:3-4
“Jilindeni; kama ndugu yakoi akikukosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema nimetubu, msamehe”
Jifunze kusamehe na kusahau ili Mungu akubariki. Msamaha ni jambo la msingi sana maishani mwako na kama uliapa kutokusamehe mtu basi futa maneno yako na uachilie msamaha ili Mungu akusamehe pia.
Kusamehe ni njia inayomfanya mtu aone baraka za Mungu haraka sana.
Anayesamehe ana furaha, Amani na upendo moyoni mwake. Na ijulikane
kuwa Mungu anapenda moyo wenye furaha.
Wengine ni wapendwa wanasali kanisa moja lakini walikwazana na hawataki kusalimiana kabisa na ibadani hushikana mikono kwa unafiki, watu kama hao hawawezi kuona baraka za Mungu maishani
mwao mpaka wasameheane. Na hata hivyo ijapokuwa wanatoa sadaka, sadaka yao ni uchafu mbele za Mungu maana inanena dhambi.
MATHAYO 5:23-25
“Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu,
uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka
kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.”
SURA YA NNE
KUFANYA KAZI YA MUNGU KWA ULEGEVU
“Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.”
Yeremia 48:10
Kuna hasara kubwa sana kwa mtu amtafutaye Mungu kwa mazoea. Kutokumtafuta Mungu kwa bidii kuna mfanya mtu akose baraka ambazo anazistahili kupata, bidii yako katika kumtafuta Mungu ndiyo wingi wa baraka kutoka kwa Mungu.
Usimtafute Mungu katika tatizo tu, mtafute Mungu kila wakati.
ZABURI 78:34-35
“Alipowaua ndipo
walipokuwa wakimtafuta; wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii. Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu aliye juu ni mkombozi
wao.”
MITHALI 8:1
“Je hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake?”
MITHALI 8:17
“ Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.”
Bidii yako ni ya
thamani sana mbele za Mungu.
WAEBRANIA 12:14
“Tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote, na huo utakatifu,ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”
Dumu sana katika neno usilegee soma neno kila siku. Weka
bidii yako katika maombi ili Mungu akujaze baraka {akujibu maombi}.
Udhaifu katika maombi ni giza linalomzuia mtu asipate baraka zaMungu.
“Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu
ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate
kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa
sana, akiomba kwa bidii.
Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena,
mbingu zikatoa mvua,
nayo nchi ikazaa matunda
yake.”
Mwangalie Eliya alivyoomba kwa bidii tunaona maombi yake yalileta matokeo mazuri. Yakobo aling'ang'ana katika kuomba mpaka akabarikiwa , iangalie
bidii yake.
MWANZO 32:24-29
“Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata
alfajiri. Naye alipoona
ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu
wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema,
Niache, niende, maana kunapambazuka.
Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana
umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.”
Hakikisha unamtafta Mungu kwa moyo
wako wote ili uone baraka zake.
KUMBUKUMBU LA
TORATI 4:29
“Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho
yako yote.”
Ukimtafuta Mungu kwa bidii utapokea kibali cha kumiliki na kutawala.
1 WAFALME 2:4
“ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari
yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu
kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa
mtu katika kiti
cha
enzi cha Israeli.”
Weka bidii
katika kuwajulisha watoto wako kumjua Mungu ili wafanikiwe
KUMBUKUMBU LA TORATI 4:9
“Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije
ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka
moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;”
Kwahiyo kutokufanya kazi ya Mungu kwa bidii ni giza linalozuia baraka za Mungu kumfikia mtu.
Mungu akubariki
sana.
SURA YA TANO
KUTOKUKAA NDANI YA YESU
YOHANA 8:31
“Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;”
Ukikaa ndani ya Yesu kunafaida kubwa sana.
Nini maana ya kukaa ndani ya Yesu?
kukaa ndani ya Yesu ni kuyavaa matendo yake na kutii neno la Mungu kwa uaminifu huku ukilifanyia kazi.
YAKOBO 1:22-23
“Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika
kioo.”
Neno la Kristo likikaa ndani yako utapokea mambo mengi sana
kutoka kwa Mungu. Siyo tu neno likae kwa wingi pia inabidi neno lilokaa ndani yako ulifanyie kazi ili lilete mabadiliko.
YOHANA 15:4-7
“Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu;
kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka;
watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
Ili Mungu akustawishe katika huduma yako au utumishi wako pamoja na mambo yako yote , anakutaka ukae ndani ya Yesu kwanza. Ukikaa ndani ya Yesu umekaa katika neno na hilo neno litakaa ndani yako
na neno hilohilo litaruhusu baraka za Mungu kukufikia kwa wingi.
WAKOLOSAI 3:16-17
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
Kukaa ndani ya Yesu pia inamaanisha kuishi maisha matakatifu.
1 PETRO 1:15
“bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;”
Maisha ambayo Mungu anamtaka mkristo aishi ni maisha matakatifu maana yeye ni mtakatifu. Na utakatifu ni kudhirisha kuwa Kristo
anakaa ndani yako.
Tukikaa ndani ya Yesu tutakuwa tumekaa nuruni na siyo gizani tena.
1 YOHANA 1:7
“bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.”
Tukikaa nuruni yaani ndani ya Yesu tutakuwa tumeliondoa giza linalotuzuia kupata baraka za Mungu.
Mungu akubariki sana.
SURA YA SITA
KUJITAMKIA AU KUTAMKIWA MANENO MABAYA
MITHALI 6:2
“Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,”
Kujitamkia maneno ya kushindwa jambo fulani kulifanya,
kunamfanya mtu aishi maisha ya kushindwa kufanikiwa kwa sababu amejifungia
kufanikiwa.
Maneno mabaya yanakamata mfumo wa maisha ya mtu na kumfanya
aishi kulingana
na alivyotamka.
Leo kuna changamoto nyingi sana na matatizo mengi kwenye ndoa kwa sababu vijana wengi wamejitamkia maneno mabaya kabla ya ndoa.
Utasikia kijana anasema naolewa tu ili nitoe aibu lakini ndoa ni ngumu sana , mpendwa kama unaingia kwenye ndoa na wazo la kuwa ndoa ni ngumu ndoa yako itakuwa ngumu .
Neno lolote unalojinenea
ni mbegu inayoota maishani mwako na mwisho wake utakuja uvune ulichokipanda. Ukipanda kushindwa utavuna kushindwa.
Wengine walijitamkia sitakaa niolewe lakini wakaolewa ,na sasa ndoa zao zipo kwenye hatari ya kuvunjika kwa sababu ya maneno mabaya waliyojitamkia.
MITHALI 18:20-21
“Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
Unaona jinsi gani maisha ya mtu yanabebwa na neno analojitamkia.
Vijana wengi walishindwa kufanikiwa kwa sababu ya maneno yao mabaya.
Anajitamkia Mimi ni maskini , mimi siwezi , mimi wa hivyohivyo , n.k
Sasa haya matamko yanamzuia Mungu kumbariki kwasababu tayari huyu
mtu amejitia vifungoni mwenyewe
na roho ya kushindwa.
AYUBU 26:4
“Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka
kwako?”
Neno ni roho , na mtu akijitamkia kushindwa atakuwa amekamatwa na roho ya kushindwa.
Ukumbuke kuwa vitu vyote viliumbwa kwa neno.
YOHANA 1:1-5
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote
kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.”
Kwahiyo epuka kujitamkia maneno
mabaya
ili Mungu akufungulie
milango ya baraka.
YEREMIA 22:29-30
“Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.”
Pia tunaona mtu anaweza kutamkiwa maneno ya kutokufanikiwa ikawa ni chanzo cha mateso maishani mwake.
Kupitia kutamkiwa maneno mabaya watu wengi wamejikuta wanakwama katika maisha yao. Futa
maneno yote mabaya uliyojitamkia au kutamkiwa.
ISAYA 8:10
“Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.”
Maneno yote uliyotamkiwa hayatasimama yafute maishani mwako.
ISAYA 7:7
“Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.”
Neno lolote baya haliwezi kusimama katika maisha yako ukilifuta. Maneno mabaya ni giza linalozuia baraka za Mungu kukufikia.
Popote ulipojitamkia kushindwa au ulitamkiwa kushindwa tamka kufanikiwa.
ZABURI 33:9-10
“Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama. Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.”
Futa maneno ya kushindwa na uweke neno la kufanikiwa lisimamie maisha yako ili Mungu akubariki.
KUMWAGA DAMU
Umwagaji wa damu ni kitendo ambacho Mungu anakichukia sana katika
maisha ya mtu,damu pekee yenye uhalali wa kumwagika ni damu ya Yesu pekee ili
ifute makosa yetu sisi.Lakini mtu anapomwaga damu ya mtu kwa sababu ya kumkosea
au kwa njia ya kutoa mimba ni dhambi inayoweza kumfanya mtu aishi maisha ya
kutangatanga.
Tunajifunza kwa kaini pale alipomuua ndugu yake Habili tunaona
kaini amepoteza thamani yake kwa Mungu na kupewa adhabu ( laana).
MWANZO 4:9-12
“Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui,
mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya
nini? Sauti ya damu ya
ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika
ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono
wako; utakapoilima ardhi
haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye
na kikao duniani.”
Tukimwangalia Kaini alivyomwua ndugu yake , tunaona jinsi damu ya
ndugu yake ilivyokuwa ikidai haki kutoka kwenye ardhi. Ardhi inaweza kufunga maisha
ya mtu asifanikiwe, hii ni kwasababu ardhi ni lango linalopitisha laana au baraka kwa mtu.
Kaini alipomwaga damu ya
ndugu yake tunaona ardhi haikumzalia matunda (
kumletea mafanikio) .
Jambo lingine
ni utoaji wa mimba, kutoa mimba pia ni umwagaji wa damu isiyokuwa na hatia
na
pia ni uuaji wa kiumbe cha Mungu kisichokuwa na hatia.
Umwagaji wa
damu unamfanya mtu asiuone
ufalme wa Mungu (uzima wa milele).
Ukitoa mimba na ukanyamazia hiyo hali
uendelee nayo bila kuitubia inatakuletea shida
sana
katika maisha yako .
Ukitoa mimba unaweza kusababisha yafuatayo
maishani mwako na kizazi
chako
1 Roho ya kuharibu mimba
2 Roho ya utasa
3 Roho ya kutokuolewa.
4 Kushindwa kuurithi ufalme wa mbinguni.
Damu ya mtu
ikimwagika kwa mikono ya mtu ,mfano utoaji wa mimba ,damu hiyo iliyomwagika
itadai haki yake siku ya hukumu.Inahitaji toba ili mtu apate kusamehewa juu ya
dhambi ya umwagaji wa damu .Binti zetu inawezekana walipata ujauzito kipindi
cha uasherati lakini wakawa wanatoa mimba kwa siri wakidai wanaficha aibu
katika jamii bila kujali Mungu anasema nini juu ya umwagaji wa damu .Umwagaji
huo wa damu isiyo na hatia ni hatari sana katika maisha ya mtu.
Damu pekee iliyona kibali cha kumwagika ni damu ya Yesu pekee ndyo iliyopata kibali iyafuye makosa yetu.
Lakini kumwaga damu ya mtu ni kujiandalia makao ya jehanamu.
Lakini usiogope maana Mungu anasamehe
kila dhambi isipokuwa ya kumkufuru roho Mtakatifu.
MARKO 3:28-29
“Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu,
na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,”
Umeua au umetoa mimba usikae na hiyo dhambi itakuzuia kufanikiwa
tubu.
MITHALI 28:13
“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
Kwahiyo bado kuna nafasi ya kufanya toba mbele za Mungu na
kurudisha uhusiano wako na Mungu kupitia damu ya Yesu.
Usiiangalie hiyo dhambi ukakosa
amani mwangalie Mungu afutaye
dhambi .
ISAYA 1:18-19
“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu
sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii
mtakula mema ya nchi;”
Mungu ni mwenye rehema kubali kutubia dhambi ya
umwagaji wa damu
isiyokuwa na hatia
ili ufanikiwe .
ZABURI 51:1-8
“Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa
na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya
maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi
utoapo hukumu. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe
kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko
theluji Unifanye kusikia furaha na shangwe,
Mifupa uliyoiponda ifurahi.”
Kwahiyo
,umwagaji wa damu ni giza linaloweza
kumfanya mtu asione baraka za Mungu hii ni kwa sababu Mungu anakuwa
hasikii kuomba kwa mtu huyo kwa sababu ya dhambi ya umwagaji wa damu.Maana
popote mtu amwagapo damu ,ardhi inamkataa isiweze kumzalia matunda .Binti
aliyetoa mimba anaweza akaolewa na akazaa watoto kabisa ,lakini kama hakutubu
juu ya damu aliyoimwaga roho ya utoaji mimba na kuharibu mimba inaweza
kuonekana kwa watoto wake .Aidha, anaweza akaolewa lakini ndoa yake ikawa ngumu
sana na isiweze kudumu kabisa kwa sababu damu ya mimba aliyoitoa inadai
haki.Usinyamazie dhambi ikiwa unajua kabisa umefanya dhambi itakuzuia kuona
baraka za Mungu maishani mwako utakuwa unasikia wengine wanainuliwa na Mungu
lakini wewe umebaki katika taabu na mateso.
Maoni
Chapisha Maoni