HAKI , SHERIA , NA NEEMA


               HAKI , SHERIA , NA NEEMA

                                  Mwl.Peter Francis Masanja

                                                0744056901


Bwana YESU asifiwe
Kuna wakati mtu wa Mungu unaweza ukakaa mda mrefu sana huoni matunda ya kile ambacho umemwomba Mungu .
Kitu chochote ambacho unakiomba ndani yake lazima kuwe na neno imani ili uweze kukipokea .
Imani inazaa haki yaani kitu unachostahili kukipokea .
Ibrahimu alihesabiwa haki  kwa imani

Maana yake alipokea kile alichostahili sawasawa na kile alichokiamini .
πŸ’» 17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;

Waebrania 11:17
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
Waebrania 11:18
19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Waebrania 11:19
Ibrahimu hakusita alipoambiwa na BWANA amtoe mwanaye , Isaka
Aliamini kuwa Mungu atamfufua Isaka  akatii sauti ya Mungu .
  Huyu Ibrahimu kupitia imani hiyo kuna ahadi aliipokea kwa Mungu .

πŸ’» 1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
Mwanzo 22:1
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Mwanzo 22:2

9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
Mwanzo 22:9
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
Mwanzo 22:10
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
Mwanzo 22:11
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Mwanzo 22:12
14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Mwanzo 22:14
15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
Mwanzo 22:15
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
Mwanzo 22:16
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Mwanzo 22:17
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Mwanzo 22:18

  Ibrahimu alikuja kupokea vitu vingi sana vizuri toka kwa Mungu kwa sababu ya ile imani . Aliamini kuwa Mungu ni msaada wake pekee .
Mtu wa Mungu lazima utambue kuwa imani inanguvu katika kupokea kile unachokiomba.
  Imani lazima iambatane na matendo ndani yake kile unachokiamini lazima ukitendee kazi ili kionekane.
 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2:26
  Ibrahimu aliitendea kazi ile imani akaitwa mwenye haki, akabarikiwa sana .
 πŸ’» 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.

Warumi 1:17
  Maisha yako ya imani yaambatane na utii . Mtu wa Mungu palipo na sheria kuna dhambi .
  Dhambi ilipoingia ndipo Mungu akaleta sheria yaani amri ambazo mwanadamu anatakiwa azifuate .
Pamoja na sheria za Mungu kuletwa bado hazikumzuia mwanadamu kuzivunja .
  Sheria ambazo Mungu alizitoa pale Sina kwa mkono wa Musa hazikutosha kumwokoa mwanadamu.
Sheria haikutosha kumfanya mwanadamu awe mbali na dhambi .
Mungu akaona ni vema sheria zake aziandike kwenye moyo wa kila mwanadamu.
  Mungu akamtoa YESU Kristo afe kwaajili ya dhambi zetu ili tuwekwe huru tutengwe mbali na dhambi.
  Ndipo tulipoingizwa katika kipindi cha neema mpaka sasa tupo huru mbali na dhambi .
Mpaka sasa hakuna amwaminiye Yesu asiyezijua sheria za Mungu .
Sheria haiwezi kumtenga mtu mbali na dhambi bali neema ya Kristo .

 16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo,
Waebrania 10:16

Mtu wa Mungu , huyu Yesu kupitia neema yake ametuzawadia vitu vingi sana .
v  Tumepokea wokovu .
v  Uzima wa milele.
v  Neema imetupa mamlaka ya kuishinda dhambi

14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
Warumi 6:14

v  Katika kipindi hiki cha neema , sisi ni watumwa wa haki ( matendo mema ).
 18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
Warumi 6:18
v  Dhambi haina mamlaka ya kututawala tena bali sisi tunayo mamlaka ya kuitawala ( kuishinda).
 12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
Warumi 6:12
v  Neema imetupa mamlaka ya kushinda dhambi .
 Ili mamlaka ya kuishinda dhambi ikae ndani yetu tunatakiwa kukaa ndani ya Yesu , tusiende mbali.

ΓΌ  Tudumu katika sala.

ΓΌ   Tusome neno

ΓΌ  Tulifanyie kazi  neno .


 Bila kukaa ndani ya YESU imani yetu katika yeye haiwezi kuzaa matunda.
v  Bila kukaa ndani ya YESU vizuri imani yetu itakuwa ya kutiana faraja kuwa mwenye haki ajapo anguka mara saba atasimama tena.

v  Mtu wa Mungu kamwe usiamini katika kuanguka na kusimama tena maana huwezi kujua siku unaanguka ndyo mwisho wako .

v   Mungu hajakuleta duniani uangukeanguke alikuleta usimame imara kabisa kama neema inavyotufundisha kukataa ubaya wowote.
 πŸ’» Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.
1 Wakorintho 16:13

Mtu wa Mungu usiruhusu mbengu ya kuanguka na kusimama tena
Ruhusu mbegu ya kusimama imara katika imani bila kuanguka .
v  Neema imetupa ujasiri wa kuonya .
v  Neema imetukataza kutenda dhambi za kujitakia ( za kujua ).

 πŸ’» 47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
Luka 12:47

 Hakuna kitu kibaya kama kufanya jambo ukijua kuwa ni katazo .
v  Mtu wa Mungu hii neema tuliipokea kwa ajili ya kutenda mema .


Ø  Tumeokolewa kwa neema.
Ø  Tunaishi kwa neema .
Ø  Tumechaguliwa kwa neema.
Ø  Tumepokea mamlaka ya kumuliki na kutawala kwa neema.
Ø  Tumeuona utukufu wa Mungu ndani yetu kwa neema .
Ø  Tumepokea karama , vipawa, na huduma mbalimbali kwa neema .
Ø  Tumempokea Roho Mtakatifu kwa neema .
Ø  Tumefanyika wana wa Mungu kwa neema .
Ø   Tunawashangaza wakuu wa dunia kwa neema.
 Neema ya Mungu inafaida sana kwetu .

 Mungu akubariki sana .


Neema ya Mungu iangaze maisha yako popote ulipo .

Neema ya Mungu izuie kila mabaya yasikupate .
Neema ya Mungu iambatane na kila ulichonacho kifanikiwe .
Neema ya Mungu ifufue miradi yako iliyokufa .
 Nakutakia jioni njema .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*