HISTORIA YA MAKANISA SABA
HISTORIA
YA MAKANISA SABA.
MWL.LAMECK
KIJALO
+255 656 824 479:
JESUS CO-WORKERS MINISTRY
Ø Makanisa
haya yanapatikana katika kitabu cha UFUNUO sura ya 2&3
Ø Hivyo
kwa wenye Biblia ni vizuri mkafungua hizo sura na kuzipitia wakati Somo
linaendelea
Makanisa saba
hayo ni:-
1)Kanisa la Efeso. Ufunuo 2:1-7
2)Kanisa la Smirna
Ufunuo 2:8-11
3)Kanisa la Pergamo.
Ufunuo 2:12-17
4)Kanisa la Thiatira.
Ufunuo 2:18-29
5)Kanisa la Sardi.
Ufunuo 3:1-6
6)Kanisa la Filadelfia
Ufunuo 3:7-13
7)Kanisa la Laodikia.
Ufunuo 3:14-22.
Kanisa ni nini?
Ø Kanisa
ni mtu, au kusanyiko la watu pamoja na Jengo wanalotumia, mtu au watu
wanaomwamini Mungu na kufanya taratibu zote za Ibada, kama vile kuabudu,
kufanya maombi, kusifu, kujifunza maneno ya Mungu n.k.
Ø Makanisa
saba(7) huonyesha historia ya Kanisa iliyopitia vipindi saba ambapo Leo hii
tupo kwenye Kanisa la kipindi cha saba liitwalo Laodikia.
Ø Vipindi
hivi vya Kanisa vilianza pale Yesu alipopaa kwenda mbinguni, ambapo tunaona
kuwa Kanisa la kwanza Kabisa kuanzishwa ni Kanisa la Efeso. Kanisa
lililoanzishwa na Mitume.
Ø Ikumbukwe
kuwa Kiini cha kuwepo kwa Kanisa ni Yesu
Kristo mwenyewe. Na katika vipindi hivi saba suala la majina ya madhehebu kama
Roman Catholics kuwa ndiyo Kanisa la kwanza hayana ukweli wowote kwani kama
tulivyo Leo hii kwenye kipindi cha Kanisa la Laodikia basi madhehebu yote
humezwa humo. Na yamkini kwenye kipindi cha Kanisa la Waefeso yalikuwepo
Madhehebu mengi tu yanayounda Kanisa.
Ø Tambua
kuwa kila kipindi cha Kanisa kina msimamizi wake ambaye ni Malaika.
Ø Ndiyo
maana Biblia inasema; Na kwa Malaika wa Kanisa lililoko...... Andika.
Ø Hivyo
Malaika alikuwepo wa Kanisa la kwanza akamaliza kazi yake, na wa pili,...,
mpaka leo tunaye Malaika wa Mwisho katika hili Kanisa.
Ø Tambua
kuwa vipindi saba vya Kanisa, ni ukamilifu wa uumbaji, kama ambavyo Mungu
aliumba dunia kwa SIKU sita, SIKU ya saba ambayo ni ukamilifu wa kila kitu
akapumzika.
Ø Hii
inamaana tupo kwenye kipindi cha mwisho Kabisa na sifa zote za Kanisa la
Laodikia ndizo tunazo sasa.
Ø Katika
hivi vipindi kuna makanisa yalitiwa Moyo, kuna makanisa yalionywa, na
kushauriwa. Hivyo vipindi hatutaviingia kwa undani sana kwani muda wangu ni
mdogo.
Hivyo twende haraka kuangalia mapito ya Kanisa
katika hivi vipindi saba.
KANISA
LA EFESO.
Ø Hili
ni Kanisa la kwanza Kabisa.
Ø Ni
Kanisa lililopitia taabu nyingi sana. Hiki ndicho kipindi ambacho Paulo
alihusika kuwaua wakristo na mmoja wa Wakristo aliyeuliwa ni Stephano. Wengi wa
mitume walifungwa jela. Hakika mwanzo SIKU zote huwa mgumu sana. Lakini licha
ya mateso na kuuliwa kwa baadhi ya wateule wa Mungu, bado Imani iliendelea
kuenea na kushika hatamu.
Ø Pia
kuna watu walijifanya ni watumishi wa Mungu kumbe ni waongo, lakini
walijaribiwa na kuonekana ni waongo, ndiyo maana imeandikwa Ijaribuni kila roho
ili kujua kama yatokana na Mungu au la. Kina Mtume Petro kipindi hiki walikuwa
si watu wa kuchezea imani zao.
Lakini mwisho hili Kanisa lilikosa Upendo,
Ø Hivyo
likaonywa likumbuke ni wapi lilipoupoteza huo Upendo na kuuanzisha upya.
Lilisifiwa kwa kuyachukia matendo ya Wanikolai ambao
wao walikuwa ni waabudu sanamu.
Hivyo watu Hawa waliahidiwa kuwa ikiwa watashinda
yote hayo na kutekeleza maagizo waliyoagizwa basi watakula matunda ya mti wa
uzima, ulio katika bustani ya Mungu
KANISA LA SMIRNA.
Ø Hili
ni Kanisa ambalo ni la kipindi cha pili.
Ø Waamini
wa kipindi hiki walipitia dhiki kubwa na walipitia hali ya umaskini sana.
Walikuwa wakitukanwa, na wengine walionekana ni waumini wazuri lakini kumbe
walikuwa ni wa Shetani.
Ø Waumini
Hawa walitiwa Moyo kuwa wasijione ni maskini bali wao ni matajiri, pia
waliambiwa wasiogope japo watatiwa magerezani. Lakini walitakiwa wawe waaminifu
hata kufa. Na wakaahidiwa taji ya uzima.
Ø Naomba
niishie kwa Leo kwenye makanisa haya mawili, next wiki nitamalizia mengine
matano.
Ø Katika
haya makanisa mawili, vitu vya kujifunza ni kuwa mpaka Leo tunatakiwa kujifunza
juu ya suala la:-
1) Kuishi kwa
Upendo.
2) Kuyapinga
matendo mabaya ambayo ni machukizo kwa Mungu kama vile kuabudu sanamu,
uzinzi, anasa, n.k.
3) Kuzijaribu
kila roho zinazojidai kuwa zatokana na Mungu, yaani tuwajaribu wachungaji,
manabii, wainjilisti, mitume, walimu, waimbaji n.k. kama je ni kweli
wanamtumikia Mungu?
5) Tusiogope
kufa wala kufungwa magerezani tunapoitetea imani yetu.
6) Hata kama unaishi maisha ya umaskini lakini
kwa sababu ya kuwa mwaminifu mbele za Mungu, jione kuwa Wewe ni Tajiri sana
7) Lakini tunajifunza kuwa tunapokosea ni
sharti tujue ni wapi tumekosea au kutenda dhambi kisha tutubu, la sivyo
tutahukumiwa
8) Tambua
kuwa ahadi zote za Mungu juu ya wanaomtumikia ni njema sana mfano kula mti
wa uzima. Kupewa taji ya uzima.
Je nani hapendi uzima?
Mungu awabariki sana.
KARIBU TENA
Kanisa la sardi maana halis
JibuFutaNimebarikiwa sana maana nilikua sijui maana ya hili kanusa la saba
JibuFuta