JE ,KUNA TOFAUTI GANI KATI YA HEKALU,SINAGOGI NA KANISA?
JE ,KUNA TOFAUTI GANI KATI YA HEKALU,SINAGOGI NA KANISA?
Mwl.Elias
Mgallah
( 0768
645 718)
Jesus Co-Workers Ministry
BWANA YESU APEWE SIFA
Ø Ipo
tofauti kati ya Hekalu,Sinagogi na kanisa ingawa tofauti yenyewe si kubwa sana
na ndio maana unaweza ukadhani vyote ni sawa lakini kumbe si sawa kwa sababu ya
utofauti wao.
Ø Si
wengi wenye kuweza kuelezea maana kamili ya matatu hayo yaani hekalu,sinagogi
na kanisa. Tofauti ya kila moja imejificha kiasi kwamba kuonekana ni
vigumu,kama vile tofauti iliyojificha kati ya maneno haya mawili;
Agano na Mkataba.
Ingawa ipo tofauti kati ya agano na ,mkataba.
Ø Basi
siku ya leo napenda nikueleze maana ya hekalu,sinagogi na kanisa kwa ufupi
kidogo,nami ninatumaini kwamba utapokea jambo kubwa siku ya leo.
TUANZE
KUZUNGUMZIA
01.HEKALU.
Ø Ilikuwa
ni sehemu takatifu ya kwa Waisraeli,hivyo hekalu lilikuwa na sehemu tatu
muhimu;
1.Ukumbi wa nje.
2.Hekalu au patakatifu.
3.Sehemu ya juu/patakatifu pa patakatifu.
Ø Kulikuwa
na utofauti kati ya hekalu/patakatifu na sehemu ya patakatifu pa
patakatifu,tofauti ya kwanza ni kwamba sehemu ya patakatifu pa patakatifu
ilikuwa ni sehemu ya juu zaidi wakati katika hekalu palikuwa chini yake.sijui
kama unanielewa.
Ø Tofauti
nyingine ni kwamba patakatifu pa patakatifu ndio ilikuwa sehemu hasa ya
kulihifadhi sanduku la agano,na
palitenganishwa na pazia kati ya patakatifu na hekalu ( Soma 1 Wafalme sura ya
6 yote). Kuhani mkuu ndiye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja kwa
mwaka ( Walawi 16:15-17).
v Hekalu
ni nyumba kubwa ya ibada ya jamii ya Wayahudi.Hekalu hukusanya watu wenye kunia
mamoja katika kumfanyia ibada BWANA.).
v Patakatifu pa patakatifu
ni mahali ambapo panaaminika kuwa ndipo Bwana Mungu hushuka na kuigusa dunia.
Ø Panaaminika
ndipo mahali ambapo Mungu huketi,hivyo kuhuni huingia mara moja kwa mwaka kwa
ajili ya kupeleka mahitaji ya watu wake waliopo chini.
Ø Kwa
sababu kuhani anakwenda kukutana na Mungu,hivyo ilimbidi kwanza ajitakase yeye
kwanza kabla ya kuachilia utakaso kwa wengine ambapo watu wote wakimsubilia
chini.
Ø Jambo
hili tunaliona likitendeka kwa kuhani Zekaria wa zamu wa Abiya pale kura
ilipomwangukia
” Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani
katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, kama ilivyokuwa desturi ya
ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. ” Luka
1:8-10
Ø Katika
biblia yetu tuisomayo kila siku,inaeleza kuwa Hekalu lilianzia tangu agano la kale. Mara ya
kwanza tunasoma habari za hekalu kupitia kuhani Eli ambaye alikuwa akiketi
hekaluni siku zote.( 1 Samweli 1:9 )
Ø
( i ) Hekalu katika Jerusalemu ( hekalu katika
Uyahudi )
Kwa mujibu wa historia ya Waisraeli,kulipatwa
kujengwa mahekalu matatu yaliyojengwa katika nyakati tofauti tofauti na watu
tofauti tofauti ndani ya Yerusalemu
1.Hekalu la
Sulemani ~ Mwaka 950 kabla ya Kristo,ambapo hapo baadae hekalu hili liliteketezwa
na Wababuloni katika mfalme wake Nebukadreza II mnamo 586 kabla ya Kristo.
2.Hekalu
lingine dogo ~ Hekalu hili lilijengwa mahali hapo hapo mnamo mwaka wa 515 kabla
ya Kristo,katika kipindi cha Ezra ndani ya utawala wake mfalme Dario ( Ezra 6:15-16).
3.Hekalu lililojengwa upya na Herode mkubwa ~
Lilijengwa mnamo kuanzia mwaka wa 19 kabla Kristo baada ya uhamisho wa Babeli
Ø (
Uhamisho wa Babeli ni kipindi ambacho Wayahudi walilazimishwa kuishi Babuloni.
kwa lugha nyingine ni kwamba Wayahudi walilazimishwa kuishi Babeli,ambayo kwa
sasa tunaweza kusema
Ø walipelekwa
Iraq,sababu magofu ya Babeli yapo katika mji wa kisasa wa Al-Hillah,kando ya
mto flati kama 90km kusini mwa Baghdadi). Hekalu hili liliteketezwa (baada ya
uvamizi ) na Warumi katika mwaka 70 baada ya Kristo.
Ø Hata
hivyo baadhi ya Wayahudi wanaamini kuwa na hekalu jingine pale Yerusalemu kitu
ambacho wataalamu wa mambo ya historia wametilia shaka kwamba inaweza kutokea
mapigano makubwa baina ya wenye kutaka na wasiotaka hali hiyo sababu katika
eneo ambapo hekalu lilipokuwapo kwanza,sasa wapo wenye imani tofauti na
Kikristo.
( ii ) Hekalu
katika ujio wa Kristo Yesu.
Ø Ujio
wa Bwana Yesu,ulihamisha hekalu la kujengwa kwa mikono hata kila aaminie
anakuwa ni hekalu ambapo Roho mtakatifu hukaa ndani yake. ( 1 Wakorintho 6:19).
Yeye Yesu Kristo ametununua kwa damu yake ya thamani,na sasa tu mahekalu ya
Roho mtakatifu.
02.SINAGOGI
Ø Neno
hili limetoka katika lugha ya kigiriki ” Sinagoge ” lenye maana ya “ Mkutano”
ni tafsiri ya kiebrania ni beit knesset lenye maana ‘“ Nyumba ya mkutano”
1 Wakorinto:6.19
Ø Au
hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Ø Katika
lugha ya kiebrania neno “ beit ”
linamaana “ nyumba” ndio maana hata ukisoma bethsaida “ Nyumba ya mvuvi”
au bethsania-Nyumba ya masikini. (Soma injili imetajwa sana majina haya ).
TOFAUTI
KATI YA HEKALU NA SINAGOGI
Ø Hekalu
huwa ni jengo kubwa lenye sehemu mbali mbali za ibada,wakati sinagogi huwa ni
mkutano tu wa watu katika jengo lisilokuwa na mgawanyo mkubwa.
Ø Hekalu
lina sehemu ya patakatifu pa patakatifu,sinagogi halina sehemu hiyo.
Ø Hekalu
lilikuwa kuanzia agano la kale mpaka agano jipya mfano kuanzia kitabu cha 1
Samweli 1:9,mpaka Ufunuo 21:22- Wakati Sinagogi lenyewe halitajwi katika agano
la kale bali agano jipya tu.
Ø Hekalu
hukusanya jamii ya watu wenye kuamini,wenye kunia mamoja katika ibada wakati
Sinagogi huchukua wanye kuamini na wasioamini,Sinagogi huchukua watu safi na
hata watu ovyo.
Ø Ukiwa
ni mfuatiliaji mzuri wa neno la Mungu,utaona kipindi ambacho Bwana Yesu au hata
mtume Paulo alipoingia katika Sinagogi kuhubiri,mara nyingi sana alishindana
nao. Sababu ya kuwa na watu wenye kuamini na wengine wasioamini. Mfano mdogo
waweza soma Matendo 17:1-5.
Ø Mara
baada ya uhamisho wa Babeli na kuvunjwa kwa hekalu la pili mwaka 70 tunaona
sinagogi likishamili sana.
Matendo ya Mitume:17.1
Ø Wakiisha
kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na
sinagogi la Wayahudi.
Matendo ya
Mitume:17.2
Ø Na
Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa
maneno ya maandiko sabato tatu,
Matendo
ya Mitume:17.3
akiyafunua na
kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha
ninyi habari zake ndiye Kristo.
Matendo ya Mitume:17.4
Ø Wengine
miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha
Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Matendo
ya Mitume:17.5
Ø Na
Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio
na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea
watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
03.KANISA.
Kanisa ni nini?
Ø Kwa
mujibu wa neno la Mungu zifuatazo ni tafsiri tano tafsiri sahihi za maana ya
neno hili “kanisa“.
Ø Awali
ya yote neno hili “kanisa” tunalolitumia leo,lenye chimbuko la lugha ya
kiyunani kwa jina la “ Kuriakon” yenye maana ya “ mali ya Bwana ” ndio maana
katika Mathayo 16:18 Yesu anasema “ nitalijenga kanisa langu,” ikiwa na maana kanisa ni mali ya Bwana
Ø Lakini
ikumbukwe ya kwamba katika agano neno hili lilitafsiriwa kwa jina la Kiyahudi “
ekklesia” yaani “ watu fulani walioitwa na Bwana,au watu waliotengwa na Bwana”
1.Kanisa ni
mwili wa Kristo
“ akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka
awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake,
ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Waefeso 1:22-23.
Ø Biblia
inaeleza ya kwamba Yeye Kristo ndie kichwa cha kanisa,lakini kanisa ni mwili
wake. Neno “kichwa cha kanisa ” lina maana ya “ kiongozi mkuu wa kanisa” .
Ø Katika
tafsiri hii ya kwanza ni vyema kufahamu kuwa tu viungo vya Kristo kwa kuwa tu
mwili wa Kristo.
Ø Ni
jambo la aibu ikiwa kanisa linaitwa kwa mwili wa Kristo lakini limekumbatia
dhambi,Je mwili wa Kristo waweza ukashiriki dhambi? Hapana hauwezi kushiriki
dhambi yoyote ile.
2. Kanisa ni
kusanyiko la waaminio katika Kristo Yesu.
Ø Na
kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na
sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.”
Yoh.10:1
Ø Ikumbukwe
kwamba kusanyiko hili la waaminio limepewa jina kondoo waliokusanyika kama
kundi pa moja na mchungaji wao. Kupitia andiko hili,Yesu anasema analo kundi
jingine ambalo anapaswa kulileta pamoja na kwa kuwa ni mali ya Bwana
basi,watamsikia.
3.Kanisa ni
hekalu/jengo/nyumba ya kuabudia.
Ø Tafsiri
hii ni moja ya tafsiri ambayo watu wengi wameijua,kwa maana watu wanapotamka
kuhusu kanisa humaanisha kwamba kanisa ni jengo fulani hivi. Kupitia fasiri
hii;wanakuwa hawajakosea. Biblia inaeleza pia kwamba;20 Mmejengwa juu ya msingi
wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
Ø Katika
yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika
Bwana.Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Ø Mmejengwa
juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la
pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu
takatifu katika Bwana.Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu
katika Roho.” Waefeso 2:21-22.
4.Kanisa ni
bibi harusi wa Kristo;
Ø Kwa
sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao
wawili watakuwa mwili mmoja.Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya
Kristo na Kanisa.” Waefeso 5:31-32.
Ø Ikumbukwe
kwamba katika ulimwengu wa roho,kila aliyeokoka na kumfuata Kristo Yesu
amefanyika kama bibi harusi.
Ø Kwa
lugha nyepesi tumefunga naye agano;na ndio maana mtu akimuacha Kristo Yesu
kisha akaigeukia miungu mingine basi anaitwa ni mzinzi/amezini.
Ø Umewahi
kujiuliza kwa nini uitwe mzinzi hali hujazini katika mwili? ( ufunuo 2:14). Hivyo tumuonapo bibi harusi
basi ni dhahiri yupo bwana harusi na pia kuna harusi yao.
Ø Katika
ulimwengu wa roho KristoYeye mwana-kondoo ndiye Bwana harusi kwa maana kuna
harusi ya mwana-kondoo huko mbinguni ( soma Ufunuo 19:7)
Ufunuo:2.14
Ø Lakini
ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya
Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba
wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
Ufunuo:19.7
Ø Na
tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo
imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
5.Kanisa ni
hekalu la Roho mtakatifu.
Ø Tafsiri
hii inalenga hekalu za namna mbili. Hekalu la kwanza ambapo Roho mtakatifu
anapokaa ni ndani yako ya moyo na hiyo ndiyo madhabahu ya kwanza ya mwamini ( 1
Wakorintho 3:16).
Ø Pia
hekalu la pili ni katika madhabahu sehemu fulani ya kanisa iliyotengwa kwa
ajili ya kazi ya Bwana. Madhabahuni pa Bwana,mahali ambapo dhabihu
zinapotolewa..
1
Wakorinto:3.16
Ø Hamjui
ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani
yenu?
Ø Hivyo
tafsiri hii inamlenga mwamini mmoja mmoja kuwa ni kanisa ( mwamini ametengwa
kwa ajili ya Bwana,huitwa pia ni sehemu ya kanisa kwa sababu moyo wake u
madhabahu). Kigezo kikubwa cha kanisa ni uwepo wa madhabahu mahali ashukapo na
akaapo Bwana Mungu.
Mkazo mkubwa wa kanisa kama mwili wa Kristo.
Kwa kuwa tumeona maana ya kanisa kiundani,basi
hatuna budi kuweka mkazo juu ya kanisa kwamba Yesu mwenyewe ndio kichwa cha
kanisa sisi tu viungo kila mmoja wetu. (Wakolosai 1:18)
TOFAUTI
YA KANISA NA HEKALU NA SINAGOGI
Wakolosai:1.18
Ø Naye
ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza
katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Ø Katika
kanisa huzungumzia mtu moja tu, pasipo kuleta maana halisi ya jengo,wakati
hekalu muda mwingine huonesha jengo,na sinagogi huonesha kusanyiko la watu.
Ø Katika
kanisa sisi tu viungo vya Kristo,hii inaonesha kuwa sote tunahitajiana
kuukamilisha mwili wa Bwana tofauti kabisa na hekalu na sinagogi.
Nakupongeza
kwa kujifunza fundisho hili,Mungu akubariki sana
Mungu akubariki sana mtumishi wa Bwana Yesu, nimejifunza hakika nilikuwa sijui baadhi ya mambo lakini sasa nimejua barikiwa sana.
JibuFuta