JE, UNA MHURI WA MUNGU ?


 📙 JE, UNA MHURI WA MUNGU ?

Mwl.Peter Francis Masanja
0744056901
BWANA YESU ASIFIWE

KARIBU TUJIFUNZE KWA PAMOJA SOMO HILI
 1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.
Ufunuo wa Yohana 7:1
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
Ufunuo wa Yohana 7:2
3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Ufunuo wa Yohana 7:3

Ø  Muhuri ni uthibitisho wa umiliki wa kitu fulani , ni alama ya ambayo inatambulisha kitu fulani kipo chini ya mamlaka fulani.
Ø  Mhuri pia ni alama inayofanya kitu fulani kikubaliwe kuwa halali .Bila mhuri kitu hicho hakiwezi kupokelewa .
Ø  Mhuri pia unasemekana kama chapa au alama ya utambulisho .
Ø  Mhuri ni kadi au kitambulisho au cheti kinachoweza kumruhusu mtu aingie mahali fulani.
Ø  Wewe mtu wa Mungu umewekwa mhuri ambao utakufanya uingie katika ufalme wa mbinguni.
 Mhuri huu tunaouzunguzia ni mhuri ambao siku ya mwisho utakupatia uhalali wa kuurithi ufalme wa Mungu ( mbinguni).
 Biblia inasema , si kila mtu aniambiye Bwana , Bwana ataurithi ufalme wa mbinguni .
Maadamu upo duniani hapa wewe mtu wa Mungu napenda Mungu akujiulize maswali yafuatayo:
Ø  Ninaombea watu pepo wanatoka lakini ninao mhuri wa Mungu ?
Ø   Ninaombea wagonjwa wanapona je,ninao mhuri wa Mungu ?
Ø   Ninaonyesha ishara na matendo ya miujiza je,ninao mhuri wa Mungu?
Ø   Ninahubiri sana injili na kumwimbia Mungu na kumpigia vinanda je,ninao mhuri wa Mungu?

 Mwulize rafiki yako je, unao mhuri wa Mungu ?
 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 7:21
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Mathayo 7:22
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Mathayo 7:23
Kwanini si kila mtu aliitaye jina la BWANA ataingia katika ufalme wa mbinguni ?
Ø  Kwasababu si kila aliitaye jina la BWANA ana mhuri wa Mungu.
 Mhuri wa Mungu unathibitishwa na matendo ya haki , hiki ndyo kigezo cha msimgi cha kumfanya mtu awe na mhuri wa Mungu.
 Wanaotiwa mhuri wanatoka katika kila.

👉🏻Taifa
👉🏻 Kabila
👉🏻 Jamaa
👉🏻 Lugha n.k
 Kama mtu anasali na anaishi maisha ya dhambi , hatawekwa mhuri wa Mungu.
 Na kama hatawekwa mhuri wa Mungu anakazi gani kanisani , maana anafanya kazi haitazaa matunda kwake .
 9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
Ufunuo wa Yohana 7:9
Ø  Tunawekwa mhuri kama saini ya kwenda mbinguni .
12 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.
Ezekieli 20:12
20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Ezekieli 20:20
 Unapodumu katika kujitakasa kwa damu ya Yesu ili uwekwe mhuri wa Mungu.
Sote tuliompokea YESU na wanaotarajia kumpokea kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tumealikwa kwenda mbinguni tukiwa tumewekwa mhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zetu.


 📙 HITIMISHO

Kuuingia ufalme wa mbinguni lazima tutiwe mhuri wa Mungu.Tuvae matendo mema.
Kama ilivyo kwenye sherehe au harusi bila kadi huingii ndivyo ilivyo na kuuingia ufalme wa Mungu .
Matendo mema ndiyo utambulisho wa kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Mungu akubariki sana


KWA MASWALI
Piga simu namba: 0679392829 au 0744056901
Waweza kunipata whats app kwa namba hizo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*