LETA HOJA ZA NGUVU π*
π± LETA HOJA ZA NGUVU π*
Mwl.Peter Francis Masanja
0744056901
π Mungu akisikia hoja zako anawaza kwa sauti na kucheka π€£π€£π€£π€£
π Katika maombi Mungu huangalia hoja zako na imani katika hoja unazompelekea .
π Umeingia kwenye maombi lakini unamwendea Mungu na hoja za kimaskini .
✍ Mungu anaangalia
1⃣ Imani
2⃣ Hoja ( mahitaji ya moyo wako )
π kama imani yako ni ndogo katika kile uombacho , utachukua muda mrefu sana kutendewa .
✍ Kama unaamini kupokea vitu vidogo sana, utavipokea kweli .
✍ kama utaamini kupokea vitu vikubwa kutoka kwa Mungu utavipata .
π» 21 Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo. .
Isaya 41:21
✍ Peleka hoja za nguvu kwa Mungu , epuka kupeleka hoja zilizochoka .
✍ Kuna wakati mtu anamwomba Mungu ampe angalau mtaji wa laki moja aanzishe biashara .
✍ epuka kuweka imani katika vitu vidogo maana Mungu hajakuleta duniani upokee vitu vidogo , vitu vilivyochoka .
✍ Weka imani yako katika vitu vikubwa Mungu atavileta kwako lakini ukiweka imani yako katika kupokea vitu vidogo Mungu mwenyewe atakushangaa sana.
✍ Aliyeomba mtaji wa laki moja atapata na atakayeomba mtaji wa milioni mbili atapata .
π Wote wamemwomba Mungu lakini wanatofautiana viwango vya imani na kupokea .
✍ Mwingine anamwendea Mungu akisema Mungu nipe angalau laki moja nifungue biashara nipate hela ya kulisha familia yangu .Hii hoja mbele za Mungu haifai.
✍ Mwingine anamwendea Mungu anaomba mtaji mkubwa kwake , amfanikishe awe na biashara kubwa na nyumba nzuri, na gari la kutembelea .Hizi ni hoja zenye nguvu
✍ Utapokea sawasawa na kile unacho muomba Mungu .
π Ukimwomba akupa maisha ya kawaida yaani si tajiri wala si maskini atakupa hayo maisha kwasababu uliyataka .Ukitaka kuongezeka anakupunguza π€£π€£π€£π€£π€£π€£
π Ukimuomba akujaze utajiri na akuweke juu sana atakutendea kwa kadiri ya imani yako .
✍ Wapo watu akiambiwa mwombe Mungu akufungulie milango ya uchumi wako umiliki biashara wanasingizia serikali
Ivi Mungu anazuiliwa kukubariki na serikali ❓
Serikali yenyewe kaiweka Mungu na anamamlaka ya kuivunja .
Jinsi unavyoamini kuishi kiuchumi ndivyo utakavyomfanya Mungu akuweke kwenye maisha unayoyaamini .
π Unaamini kwamba wewe huwezi kumiliki nyumba nzuri utaishi bila kukaa kwenye nyumba nzuri hata kama umeajiriwa .
π» 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
Warumi 1:17
✍ Imani yako ndiyo maisha yako .
✍ Unajua mfalme Sulemani alipeleka hoja zisizo na nguvu kwa Mungu ❓
π Mungu akamwuliza ni hilo tu umeomba ❓
✍ Mungu aliiangalia hoja ya mfalme Sulemani akaona haina nguvu .
π» 11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
1 Wafalme 3:11
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
1 Wafalme 3:12
✍ Nikisoma 1 Wafalme 3:12 naona Mungu anaweza kufanya sawasawa na umwombacho .
✍ Katika kufanikiwa Wakristo tunatofautiana sana kwa sababu kuna baadhi ya watu wameweka imani yao kuishi maisha ya chini na ndicho wamwombacho Mungu .
✍ Mungu alipomsikia Sulemani anaomba kitu kimoja tu akashangaa sana kwanini Sulemani amesahau vitu viwili
1⃣ Maisha marefu
2⃣ Utajiri
Hivi ni vitu vya msingi kwa kila amchaye Mungu .
✍ Kwahiyo weka imani yako katika vitu vikubwa utavipokea kwa jina la YESU .Amini hivo maana Mungu anataka hoja zenye nguvu ( hoja zenye mashiko ) .
π Usimwombe Mungu akuweke maisha ya chini mwombe akuinue juu
✍ Na katika kufanikiwa kwako unahitaji adui ✍✍✍✍✍✍✍
✍ Wewe unaomba kidogo jirani yako anaomba kikubwa akipewa na Mungu acha kumwonea wivu hicho ndicho alikiomba kwa Mungu wake na wewe upo hali chini kwa sababu uliomba kwa Mungu akakuweka hivo sawasawa na imani yako .
✍ Kuna watu walinunua gari kwa sababu ya kutimuliwa vumbi na marafiki zao njiani.
✍ Mvua inakunyeshea halafu jirani yako kabisa anakupita na gari lake tena anakanyaga maji yanakurukia moyoni mwako ukasema huyu jamaa ni mpumbavu nitamwomba Mungu anipe gari zuri zaidi yake namimi nimiliki langu katika jina la Yesuπ€£π€£π€£
✍ Ukinyimwa kitu utakuwa na akili ya kutafuta kwa bidii , Ulimwomba Mungu akupe nyumba na upo umepanga , sasa kama umeshamwambia ukanyamaza atakukumbusha kwa kutumia watu na watu wanaweza kuwa maadui yaani baba mwenye nyumba anaweza kukuanzishia ukorofi mpaka ukaona kero π€£π€£π€£ kumbe Mungu anatumia mbinu hiyo wewe uwe na nyumba yako π€£π€£π€£
✍ Yakobo baada ya kuona upinzani akapata wazo la kuondoka kwa Labani ,
✍ Yakobo alifanyiwa hila na baba yake mkwe .
✍ Yakobo alipoona sasa labani ameanza kumpiga vita akaona heri awachukue wake zake akaanze maisha yake .
✍ Tunahitaji upinzani ili tufanikiwe π€£π€£π€£
✍ Tunahitaji upinzani ili tuwe na bidii
✍ Tunahitaji upinzani ili tuanzishe vitu vyetu .
π» 2 Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi.
Mwanzo 31:2
3 Bwana akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe.
Mwanzo 31:3
5 Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama jana na juzi. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami.
Mwanzo 31:5
9 Hivi Mungu akamnyang'anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi.
Mwanzo 31:9
✍ Upinzani alioupata Yakobo kwa Labani mpaka akaambiwa ondoka ulikuwa mkali sana .
✍ Aliona jicho la mzee Labani linabadilika kila siku .
✍ Sasa na wewe ndugu yangu ukiona baba mwenye nyumba amekubadilikia tambua kuwa kuna mahali Mungu kapaandaa ukajenge ili uishi .
✍ Ujue tusiwe wepesi wa kutegemea usafiri wa watu , yaani unategemea lift ya gari la mtu halafu akikufikisha uendako unaanza kumwambia
π Mungu akubariki sana akuongezee na magari mengine ufanikiwe zaidi .
π Jiombee nawewe usipeleke kwa wengine tu .π€£π€£π€£π€£π€£π€£
π Wengi wanajua kubariki wengine na mpaka wanabarikiwa sana lakini wao hawajitamkii hizo baraka .
HITIMISHO
Kwa imani peleka hoja zenye nguvu mbele za Mungu naye atakubarik
✍ Mwambie Mungu aamuru baraka zake zikujie katika utumishi wako , uchumi wako , ndoa yako , watoto wako, n.k
π Hizi ndiyo hoja zenye mashiko yaani hoja za nguvu mbele za Mungu .
Dai vitu kadri uwezavyo , dai vingi Mungu atakupatia.
✍ Epuka kudai vitu vidhaifu dai vitu vyenye nguvu Mungu atasikia maombi yako , Mungu atakuandalia watu wazuri wa kukusaidia kufikia malengo yako .
Maoni
Chapisha Maoni