MAOMBI BILA NENO LA MUNGU NI SAWA NA GARI BILA MAFUTA
📖 MAOMBI BILA NENO LA MUNGU NI SAWA NA GARI BILA MAFUTA 📙
Mwl.Peter Francis
Masanja
0744056901
📖📖📖📖📖📖📖📖📖
✍ Kumshinda shetani siyo
kazi nyepesi kama huna neno la Mungu ndani yako .
✍ Neno la Mungu ndiyo
kweli na hii kweli humweka mtu huru kabisa kutoka kwenye mitego ya ibilisi.
📖 11 Nao
wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao
hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12:11
✍ Neno la Mungu na damu
ya YESU ni silaha kuu ya kumshinda shetani .
Bila neno maombi yako
yatakuwa kama kusoma gazeti tu .
: ✍
Kama unadesturi ya kuanza maombi bila neno nakushauri acha kabisa na uanze
kusoma neno la kusimamia mahitaji yako unayompelekea Mungu .
✍ Maombi yakikosa neno
yanachosha na hayawi na nguvu ndani yake .
✍ Umefunga na kuomba na
umeorodhesha mahitaji ya kuombea , pia usisahau kuweka neno la Mungu
litakalosimamia kila hitaji .
✍ Baraka za Mungu
zinaletwa na neno la Mungu pekee , ukilisimamia vizuri na kulitendea kazi
utafanikiwa .
: ✍
Neno la Mungu ni silaha ya kumpigia shetani kwahiyo litumie katika maombi
✍ Usipambane na watoto
wako kwa fimbo , bali weka msingi mzuri wa kumjua Mungu
✍ Watakapoingia kwenye
maombi wafundishe kutumia neno wawe waombaji mashujaa .
✍ Jiwekee ratiba ya
kutafakari neno kila siku , ili mwovu akikujia umchape vizuri .
✍ Huwezi kumshinda
shetani kama huna ushirika na neno la Kristo .
✍ Halleluya 🎤🎤
Neno la Mungu
likuongoze katika maombi , ujiepushe na maombi ambayo hayatumii neno maana ni
dhaifu .
✍ Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni