NGUVU YA MSAMAHA 2


             NGUVU YA MSAMAHA
         Mwl.Peter Francis Masanja
              0744056901
 Second lesson 


 Somo letu lililopita tuliangalia faida ya msamaha kiroho .
Leo tuangalie faida hasara za kutokusamehe kiroho na kiafya.
1. Kutokusamehe husababisha ugonjwa wa hasira.
🏻 mtu wa Mungu tambua kuwa hasira miongoni wa magonjwa ambayo yanatesa vijana katika maisha yao .
Usiposamehe itakuwa kila unapomwona aliyekukwaza au kukukosea hasira zinapanda tena .
Usiposamehe utakuwa mwepesi wa hasira ukikwazwa jambo dogo tu hasira kali inakupanda .
 Kuna vijana walijikuta wamepoteza dira ya maisha kwa sababu ya hasira .
 Kutokusamehe hupansikiza mbegu ya wepesi wa hasira .
Tafiti zinaonyesha vijana wengi walioumizwa kwenye mahusiano wengi ni wepesi wa hasira .
Hii ni kwasababu ya kutunza kumbukumbu za wapenzi wao .
Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
 Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Mithali 15:18



2. Kutokusamehe huzeesha mapema .
Mtu wa Mungu unaposamehe maana yake unamwondoa kabisa mtu aliyekukosea moyoni mwako .
Ukikaa na mtu umemchukia hutaki kumsamehe unaweza ukakwama kiafya.Watakuona kila siku unakonda tu .
 Hali hii ya kuzeeka mapema hujidhihirisha kwa wanandoa .
Utaona binti ameolewa alikuwa na ngozi nyororo na umbo zuri lakini walipopishana kidogo tu kila siku huzuni ukimwuliza anasema haifurahii ndoa yake .
Kila siku utamwona anakonda kama ukuni mkavu
Binti kaolewa lakini miaka mitatu amezeeka na yupo na mumewe anakula vizuri kabisa , tafakari.

3. Kutokusamehe huleta magonjwa ya moyo .
 Mtu wa Mungu unatakiwa uepuke sana hali ya kutokusamehe .
 Usiposamehe maana yake ukimwona aliyekukosea mapigo ya moyo yanapanda .
Mishipa ya moyo inatanuka , presha na stress zinakuua uzeeni .
 Kuna mama mmoja alikosana na mume wake alipata stress akalazwa .Mama hakutaka kabisa kuonana na mumewe ilikuwa kila akimwona ugonjwa unaanza upya .
 Mama yule alikataa mpaka kula chakula anaomba afe tu .
 Yule mama alipotoka hospitali alirudishwa nyumbani kwao lakini haukuisha mwaka akafariki.

 4. Kutokusamehe hupandikiza roho ya mauti
 Maana yake ukishindwa kusamehe kifo kinakunyemelea wewe mwenyewe .
 Ukijisikia huna ule moyo wa kusamehe jua shetani yupo kazini anataka akumalize.


 5. Kutokusamehe husababisha roho ya kisasi ( kulipiza kisasi ) pamoja na Roho ya uuaji( umwagaji damu ) .
  Kuua siyo lazima uchukue upanga au silaha yoyote ,
 Hata kumchukia mtu ni kuua mbele za Mungu .

 21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
Mathayo 5:21
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Mathayo 5:22
 Chuki nyingi za ndugu zimeleta uuaji na wengine kuua undugu kwa kutangaziana kabisa kwamba fulani siyo ndugu yangu kuanzia leo
 Tatizo ni kutokusamehe .

6. Kutokusamehe humfanya mtu asisamehewe dhambi zake mbele za Mungu.

15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6:15
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11:25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Marko 11:26
Samehe ili Mungu akusamehe dhambi zako.

7 Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.
Warumi 4:7

8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.
Warumi 4:8

7.Kutokusamehe Husababisha Maombi Yako Yasijibiwe.
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

Marko 11:25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

Marko 11:26

 Kwanini usiposamehe Mungu hawezi kujibu maombi yako.
Kwa sababu moyo wako umebeba

📙 UCHUNGU
📙 KINYONGO
📙 CHUKI

📙 UNAFIKI

📙 UONGO


n.k

Moyo wa mtu asiyesamehe ni mchafu .
Mungu anataka ufanye maombi ukiwa na moyo safi .
 Bila kuwa na moyo safi huwezi kumwona Mungu( maombi yako hayatajibiwa )

 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Mathayo 5:8

8. Kutokusamehe Humleta Mtu Hukumuni
 35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Mathayo 18:35
 Mtu wa Mungu kutokusamehe ni dhambi kwahiyo usipoiacha inaweza ikakuzuia kuurithi ufalme wa mbinguni .
Mungu akubariki sana leo naishia hapa


Karibu tena siku nyingine



francispeter424@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*