SIKILIZA UONGOZI WA BWANA 📙
📙 SIKILIZA UONGOZI WA BWANA 📙
Mwl. Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
💻 8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Zaburi 32:8
✍🏻 Bwana akufundishe namna ya kuongea na watu vizuri .
✍🏻 Bwana akufundishe kusamehe waliokukosea siku ya leo , usamehe na kusahau .
✍🏻 Bwana akufundishe kutafakari neno lake .
Bwana akuonyeshe mambo mazuri kwaajili ya maisha yako leo katika jina la YESU .
✍🏻 Bwana akuonyeshe ni wapi umekosea ukashindwa kupata majibu ya maombi yako leo akujibu katika jina la YESU .
✍🏻 Bwana akuonyeshe marafiki wazuri watakao kusaidia kiroho siku ya leo katika jina la YESU.
✍🏻 Bwana akuonyeshe mambo makuu ambayo yatafanikisha ukuaji wako wa kiroho na kiuchumi katika jina la YESU .
✍🏻 Bwana akushauri kufanya maamuzi sahihi katika ndoa yako au uchumba wako .
✍🏻 Bwana akushauri katika maamuzi yoyote unayotaka kufanya .
✍🏻 Bwana awe mshauri wako mkuu katika jambo lolote unalolifanya .
✍🏻 Bwana akutazame asikuache kila upitapo awe pamoja na wewe .
✍🏻 Bwana aitazame biashara yako asiiache aibariki na kuilinda 🎤 Halleluya
✍🏻 Bwana aitazame huduma aliyoiweka ndani yako aikuze .
✍🏻 Bwana akitazame kila kitu ulicho nacho akifanikishe katika jina la YESU Kristo .Amen
📙 Fuata uongozi wa Mungu ili uishi maisha ya viwango vya juu .
Mungu akubariki sana akufanikishe katika jambo ulifanyalo
https://peterfrancismasanja.blogspot.com
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
Maoni
Chapisha Maoni