SIRI KATIKA MAOMBI 🛐
SIRI KATIKA MAOMBI 🛐
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
SAUTI YA MUNGU MINISTRY
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
*🛐 KWANINI BAADHI YA WATU HUSHINDWA KUOMBA KWA MUDA MREFU ❓*
✍🏻 Kutokukaa ndani ya YESU kunamfanya mtu ashindwe kuomba kwa muda mrefu .
📙 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Yohana 15:7
✍🏻 Kutokusoma neno kunamfanya mtu aombe kwa mda mfupi akose cha kuongea .
💻 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Wakolosai 3:16
✍🏻 Dhambi usipoitubia vizuri ni kikwazo cha wewe kuomba muda mrefu
Dhambi inakusababisha uombe maombi ya kuchoka .
✍🏻 Na katika toba hawaingii na neno.
Toba kavu haina manufaa .
✍🏻 Fanya toba inayoambatana na neno .
Mfano :
💻 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
2 Mambo ya Nyakati 7:14
15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.
2 Mambo ya Nyakati 7:15
16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
2 Mambo ya Nyakati 7:16
17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;
2 Mambo ya Nyakati 7:17
18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 7:18
💻 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Isaya 1:16
18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Isaya 1:18
Mwambie Mungu
🛐 Eee Mungu unasema tujioshe , tujitakase , tuondoe uovu na tuache kutenda mabaya .
🛐 Ninakuja mbele zako sawasawa na neno lako lilivyoandikwa katika
Isaya 1:16,19
Nionye Bwana , nioshe dhambi zangu kwa damu ya YESU .
Pia neno lako linasema katika zaburi 51
💻 1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
Zaburi 51:1
2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
Zaburi 51:2
3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Zaburi 51:3
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Zaburi 51:4
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Zaburi 51:5
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
Zaburi 51:6
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
Zaburi 51:7
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
Zaburi 51:8
9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.
Zaburi 51:9
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
Zaburi 51:10
11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
Zaburi 51:11
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
Zaburi 51:12
Hii ndio toba ya kweli lazima iambatane na neno
Usifanye toba kavu yaani toba isiyo na neno .
Hii itakufanya uombe mda mrefu na Mungu atakujibu maombi yako
✍🏻 Kukosa umoja katika maombi kunasababisha upungukiwe maombi .
✍🏻 Tafuta marafiki mwe mnaomba nao kama kikundi .Hii itakuimarisha katika maombi .
✍🏻 Ukiona ulikuwa mwombaji sana halafu umepungukiwa kuna sababu mbili .
✍🏻 Umeanza maisha ya dhambi .
✍🏻 Unaishi na maeneo yasiyosalama wewe kuishi ( unaishi na wana wa uasi ) .
[
📙 UFANYAJE ILI UOMBE KWA MUDA MREFU ❓*
✍🏻 Anza na kumsifu Mungu kwanza maana kusifu kunawafukuza maadui .
✍🏻 Mshukuru Mungu kwa kukupa afya na uzima na kukupatia kibali cha kuomba .
✍🏻 Mwabudu katika roho na kweli .
( omba toba na reheme )
✍🏻 Msifu Mungu
✍🏻 Soma neno la kusimamia maombi yako .
✍🏻 Mkaribishe Roho Mtakatifu akufundishe kuomba na damu ya YESU ikufunike
Pia ita jeshi la malaika kutoka mbinguni likuzingire nikulinde .
✍🏻 Hakikisha unalitakasa eneo unapofanyia maombi ili asiwepo adui na mpelelezi yeyote wa kiroho .
✍🏻 Eneo unalofanyia maombi lazima liwe salama kiroho .
Maana kuna maeneo mengine yameugua yanaroho chafu .
📙 2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;
Kumbukumbu la Torati 12:2
3 nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.
Kumbukumbu la Torati 12:3
✍🏻 Hakisha unaorodhesha mahitaji yako ya kuombea hii itakufanya uombe kwa mda mrefu .
Kila hitaji mbele za Mungu lina ushahidi kutoka kwenye biblia yaani neno .
✍🏻 Kila hitaji lina neno la kusimamia .
Zingatia mifano ya mahitaji yafuatayo :
📙 KUOMBEA UCHUMI ( BIASHARA ) .
💻 11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.
Isaya 60:11
📙 KUOMBEA WAGONJWA
💻 1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 10:1
💻 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Marko 16:17
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Marko 16:18
📙 KUOMBEA AMANI
💻 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani.
Yeremia 29:7
📙 KUOMBEA HUDUMA KANISANI
💻 Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.
Habakuki 3:2
📙. KUOMBA ULINZI
💻 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
Isaya 62:6
Mwambie Mungu yeye anasema , kupitia maneno hayo mwambie afanye sawasawa na maneno hayo .
Neno linanguvu sana katika hitaji umwombalo Mungu .
Maoni
Chapisha Maoni