TAFTA KUJUA NI KITU ULICHONACHO AMBACHO ADUI ANAKIWINDA


 TAFTA KUJUA NI KITU ULICHONACHO AMBACHO ADUI ANAKIWINDA



MWL.Peter Francis Masanja
0744056901

BWANA YESU ASIFIWE
Ø  Unaweza ukawa unaombea jambo fulani kumbe adui hakitafti hicho anatafuta kingine kabisa .
Ø  Unaweza ukawa unaombea uchumi wako kumbe adui anawinda uhai wako .
 Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.
Zaburi 38:12
Ø  Tafta kujua nini adui anakiwinda kwako ,
Ø  Mwulize Mungu atakujulisha ni nini adui anawinda kwako .
Ø  Mtu wa Mungu , lazima ujue je anawinda nini huyo adui .

v  Inawezekana Anawinda:
·         Watoto wako .
·         Afya yako
·         Ndoa yako
·         Uchumba wako .
·         Huduma yako ( utumishi wako aiue )



Ø  Halafu wewe ukajikuta unaombea uchumi tu ambao hawindi kabisa .
Ø   Baada ya kujua anachowinda tafta kujua anatumia mbinu gani na silaha gani .
Ø  Adui anaweza akaja kwa kujifanya rafiki kwako lakini anakuvizia akumalize .
Ø   Adui anaweza kuleta mtu asiyesahihi , mchumba , mke asiye sahihi kwako ili aue huduma yako .
Ø   Baadhi ya vijana wamejikuta wanakimbia huduma na kumwacha Mungu kwa sababu ya maneno yaani kukosolewa katika kila walifanyalo .
 Kijana tambua kuwa ukiona unasemwa sana na kupigwa vita vya maneno hiyo inamaanisha kuwa adui anapambana na huduma yako anataka kuiua  kwa kukutia roho ya kukata tamaa.
Ni jukumu lako kuombea huduma yako sasa .
 Kabla ya kuingia kwenye maombi lazima ujue unaombea jambo gani na ni kwanini
 Umeona kuna hitilafu gani mpaka hitaji hilo uliweke kwenye maombi .
 Kama hujaona hitilafu ombea ulinzi na kibali cha Mungu kitawale juu ya eneo hilo .
 Baada ya kujua anachokiwinda adui hakikisha Mungu yupo upande wako .
 Unaweza ukaanza kupambana na adui kumbe Mungu hayupo upande wako ( hayupo pamoja na wewe) ukajikuta unashindwa kumpiga adui wewe anakupiga .
 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
Zaburi 56:9
 Maombi ya kupambana na adui ( maombi ya vita ) yanahitaji ukaribu na Mungu zaidi .
 Lazima umkaribie Mungu ili awe pamoja na wewe katika vita uliyonayo .
 Lakini Bwana yu pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Yeremia 20:11

 UFANYE NINI BASI ILI KUHAKIKISHA KATIKA VITA YA KIROHO ULIYONAYO BWANA AWE UPANDE WAKO ?
Ø  Tenda mema ili Mungu asikuache katika vita ya kiroho uliyonayo .
 Ukitenda mema hakuna wa kukudhuru maana utakuwa unalindwa na Mungu .
 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
1 Petro 3:13
Ø  Uwe na desturi ya kuomba toba ( kujitakasa ) mbele za BWANA.
Rejea ZABURI 51
Ø  Epuka maisha ya dhambi , dhambi inakutenga mbali na Mungu , dhambi inamfanya Mungu akuache na kupigwa na adui .
Ø   Israeli walipofanya dhambi Mungu akawaacha , wakapigwa sana na kuwa watumwa .
Adui anaweza kukupiga kwa sababu ya maisha ya dhambi .
 Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana; Bwana akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba
Waamuzi 6:1
Ø  Kuna vita mtu inaweza ikamwandama na kuteswa kwa sababu ya mfumo wa maisha fulani ambao unamzuia Mungu kuwa pamoja naye na kisha adui kuwa na uhalali wa kuleta mateso .

Ø  Maombi ya vita yanahitaji kujisafisha ( kusafisha njia zako ) .

Hii itamfanya Mungu awaaibishe adui zako .
 Mungu akubariki sana

Karibu katika mwendelezo wa somo hili siku nyingine


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*