UHUSIANO ULIOPO KATI YA ARDHI ,MBINGU NA MAISHA YA MTU KIROHO NA KIMWILI
UHUSIANO
ULIOPO KATI YA ARDHI ,MBINGU NA MAISHA YA MTU KIROHO NA KIMWILI
Mwl.Peter Francis
Masanja
0744056901
✍ Mungu akubariki sana
wewe uliyepata kibali cha kujifunza somo hili .
Karibu tuendelee .
Tuombe
Mtakatifu
🛐Mtakatifu 🛐Mtakatifu 🛐
Baba wa mbinguni ,
tunakushukuru kwasababu ya kibali ulichotupa cha kujifunza somo hili , tunakuomba ufungue macho yetu ya kiroho ,masikio
yetu ya kiroho , fahamu zetu na mioyo yetu tukapate kusikia neno lako katika
jina la Yesu .Amen
✍ Inawezekana umeomba
mda mrefu sana lakini bado unaendelea kukutana na vita kali sana katika maisha
yako .
Hii ni kwasababu
hujawahi kumwambia Mungu juu ya ardhi na mbingu mahali unapoishi .
: ✍
Naomba tuiangalie ardhi inasifa gani ambazo zinaweza kuathiri maisha yako ya
kimwili na kiroho .📖
📖 SIFA AU TABIA ZA
ARDHI KIROHO 📖
Ardhi katika biblia
imeandikwa kwa jina la nchi
Kwahiyo hakuna tofauti
kati ya nchi na ardhi .
Nchi ni ardhi yenye
mipaka halali ya umiliki .
ARDHI
INAMASIKIO
✍ Ardhi inasikia kila
kitu ambacho itaambiwa na kukitekeleza kabisa .
✍ Ardhi inaposikia neno
inaliandika na kulitekeleza .
1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na
nchi isikie maneno ya kinywa changu.
Kumbukumbu la Torati
32:1
: ✍Mungu
alipoiumba ardhi aliumba na mbingu akazifanya pamoja haziachani .
Zote zinasikia na
akiziita zinamtii
13 Naam, mkono wangu
umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo
husimama pamoja.
Isaya 48:13
Palipo na ardhi kuna
mbingu na ukinena neno juu ya ardhi na mbingu husikia pia kwa maana zipo sawa
na pande mbili kwenye sarafu .
29 Ee nchi, nchi, nchi,
lisikie neno la Bwana.
Yeremia 22:29
30 Bwana asema hivi,
Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa
siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi
katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Yeremia 22:30
✍ Ardhi imepewa masikio
katika ulimwengu wa roho .
ARDHI
INA KINYWA
✍ Ardhi inauwezo wa
kumeza na kutapika .
Inauwezo wa kufungua
kinywa chake na kuhifadhi mambo mazuri au mabaya .
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika
ardhi, iliyofumbua
kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
Mwanzo 4:11
12 utakapoilima ardhi
haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mwanzo 4:12
📙 ARDHI INA MACHO
✍ Ardhi ina macho na ni
shahidi ya mambo yote ayatendayo mtu na kuyanena , mema na mabaya .
📖 Nazishuhudiza
mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,
baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
Kumbukumbu la Torati
30:19
📙 ARDHI NI KITABU CHA KUHIFADHIA MAMBO
YANAYOMHUSU MTU , MEMA NA MABAYA
✍ Inaandika na kuhifadhi
mema au mabaya .
📖 29 Ee nchi,
nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Yeremia 22:29
30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana
watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika
wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala
tena katika Yuda.
Yeremia 22:30
✍ Kuna Wakristo
walipohamia maeneo fulani walienda kupata tabu sana katika maisha yao kwasababu
ya kuenda kuishi kienyeji bila kumwuliza Mungu ardhi waliyoihamia imebeba nini
.
✍ Kuna ardhi zimeandika
habari chafu , zimenenewa kwa kila atakayekuja kuikalia lazima apate mateso .
✍ Tafta sana kufahamu
siri iliyopo kwenye ardhi utakayohamia kwenda kuanza maisha juu yake .
Hii itakusaidia kujua
vita juu ya eneo hilo iko wapi .
✍ Ardhi ikiambiwa kila
mtu atakayoikalia augue magonjwa au asifanikiwe au ndoa yake ivunjike au awe
mzinzi au awe mlevi au kahaba , au asizae , au watoto wake wasioe wala kuolewa
inatekeleza kabisa .
✍ Unaweza ukashangaa
kwenda tu kuikalia yakaibuka matatizo maishani mwako .
✍ Maarifa ya kiroho
yanahitajika sana ili kung'oa hizo roho chafu ambazo zinasimamia mabaya juu ya
ardhi .
✍ Kuna ardhi zingine
ukiikanyaga tu , inaanza kukupa ishara kuwa imeugua , ina magonjwa inahitaji
tiba .
ARDHI
HUUGUA
✍ Ardhi ikifanyiwa maovu
mfano , uganga, uchawi , kupitia tambiko na mazindiko inaugua kabisa na inakuwa
na roho za mauti .
: 📖 14 ikiwa
watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na
kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na
kuwasamehe dhambi yao, NA KUIPONYA NCHI
YAO.
2 Mambo ya Nyakati 7:14
✍ Pigia mstari neno
" na kuiponya nchi yao "
✍ Maovu yakitendeka juu
ya ardhi ardhi huugua na kuwa ya tofauti sana
✍ Ardhi iliyougua
inawafanya watu wanaoikaa kulala usingizi mgumu
Unalala unamka asbuhi
unapiga miayo na uchovu juu yako , unaamka unaenda kazini lakini uchovu
unausikia .
✍ Kwahiyo unatakiwa kuwa
mtu makini sana katika ardhi unayohamia kwenda kuishi , hata kwenye nyumba ya
kupanga .
✍ Angalia maisha ya
kiroho ya watu wanaokuzunguka , angalia maendeleo yao ya kiafya , na kiuchumi .
Angalia tabia zao na za
watoto wao zikiwa ni mbaya ujue kabisa kunashida kwenye ardhi .
✍ Kisha ingia kwenye maombi ya toba juu ya
ardhi hiyo .
📖 14
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na
kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na
kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
2 Mambo ya Nyakati 7:14
15 Sasa macho yangu
yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.
2 Mambo ya Nyakati 7:15
16 Maana sasa
nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko
milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
2 Mambo ya Nyakati 7:16
17 Nawe, ukienda mbele
yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru,
na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;
2 Mambo ya Nyakati 7:17
18 ndipo nitakithibitisha kiti cha
enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa
kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 7:18
✍ Vunja ile madhabahu
iliyosimama juu ya ardhi kusimamia mabaya .
📖 2
Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa
mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti
wenye majani mabichi;
Kumbukumbu la Torati
12:2
3 nanyi zivunjeni
madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na
sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na
mahali hapo.
Kumbukumbu la Torati
12:3
✍ Futa maneno yote na
habari zote mbaya zilizoandikwa juu ya ardhi hiyo .
Futa kwa damu ya Yesu .
7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili
halitasimama wala halitakuwa.
Isaya 7:7
Mwambie Mungu aitakase hiyo ardhi kwa damu ya
Yesu .
22 Na katika Torati karibu vitu
vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9:22
Damu ya Yesu inamamlaka
ya kuitakasa ardhi iliyonenewa mabaya
Nimebarikiwa sana na mafundisho kuhusu ardhi mbingu na jinsi mahusiano haya yaniadhirivyo.
JibuFutaNimebarikiwa na mafundisho
JibuFuta