ALAMA BARABARANI


                              ALAMA BARABARANI


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

Maisha ya mwanadamu yapo kwenye barabara ambayo imejaa sheria , kanuni na taratibu amabazo zinatakiwa zifuatwe.
Mungu ameweka alama katika barabara yako ya kiroho.
Zipo alama nyingi sana ambazo zinayaendesha maisha ya mwanadamu na kujua matumizi ya barabara yake ya kiroho .
Maisha yako ya kiroho ni barabara ambayo Mungu ameweka alama uzifuate ili uweze kufika salama uendako .


ZIFUATAZO NI ALAMA ZA KUZINGATIA NA KUZIFUATA KATIKA BARABARA YAKO YA KIROHO


Mtu wa Mungu unatakiwa kufuata alama hizi ili ufanikiwe kufika katika safari yako ya kiroho( wokovu ).
1. Utakatifu
 Utakatifu ni alama nzuri sana katika barabara yako ya kiroho. Bila utakatifu barabara yako ya kiroho itakuwa chafu na itaangamia yaani utapata ajali ya kiroho yaani anguko .
Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.



Mambo ya Walawi 20:26
Utakatifu ni alama ya Mkristo aliyehai katika barabara yake ya kiroho
Japo wakristo wengi huikana hii alama kuwa hawana katika barabara yao ya kiroho.
Sikiliza nikueleze mtu wa Mungu.

Duniani kuna watakatifu ambaye wa kwanza ni mimi na wewe hapo Mungu anatuhitaji sana
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
1 Petro 1:15
kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
1 Petro 1:16
Mungu ni Mtakatifu na wanaomwabudu inawapasa wawe watakatifu yaani wajitakase watubu dhambi zao na kuziacha kabisa .
Kwahiyo alama hii lazima iwepo kwenye barabara yako ya kiroho.
Kuna baadhi ya wakristo husema hakuna mtakatifu duniani hasa wanapoonywa kuwa barabara yao ya kiroho imechafuka inabidi waisafishe.
Maswali haya wanauliza
Inamaana wewe ni mtakatifu ?
Wewe ni nani unanihukumu ?
Mpendwa huhukumiwi unatakiwa ushukuru na kutengeneza njia zako ukaishi maisha matakatifu .
Tupo katika dunia ambayo kila mtu anadai anajua neno vizuri anakataa maonyo .
 Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.



1 Wakorintho 8:2
Katika alama hii ya utakatifu ni ya muhimu sana kuijua kwa upana zaidi maana vijana wengi huchafua barabara zao za kiroho kumpa nafasi shetani awamiliki wakisema hakuna mtakatifu duniani .Kitu ambacho siyo kweli
 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Zaburi 16:3
Ufalme wa Mungu haumilimiwi na watu ambao hawana utakatifu .
 Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.
Danieli 7:18
Ufalme wa Mungu utatekwa na watakatifu , yaani wataumiliki wao .
: Izingatie alama hii ya utakatifu lazima iwepo katika barabara yako ya kiroho.

2.Neno na nguvu .
Hii ni alama nyingine katika barabara yako ya kiroho.
Neno ni alama nyingine ambayo inatakiwa ionekane katika barabara yako ya kiroho.
Neno litakufanya ung'are ukilisoma ukalielewa na ukaishi sawasawa na linavyosema.
Alama hii vijana wanatakiwa waitafte kwa bidii sana na kuhakikisha isifutike mioyoni mwao . Alama hii ndyo imebeba nguvu za kiroho na nguvu za ushindi.
Alama hii pia imebeba nguvu ya kukua kiroho na kuimarika sana .
.... Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

1 Yohana 2:14
Kijana usalama wa barabara yako ya kiroho upo ndani ya neno pekee na hilo neno lazima libadilishe mfumo wa maisha yako .
Maisha yako ya imani , yapo ndani ya neno
 Neno ni alama ambayo inafanya barabara yako ya kiroho iwe safi kabisa na kila mtu atatamani maisha yako .
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Zaburi 119:11
15 Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako.
Zaburi 119:15
16 Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.
Zaburi 119:16
Neno ndyo alama pekee ya Mkristo inayomfanya ashinde dhambi.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Waefeso 6:11
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:17

                                     SOMO LITAENDELEA
Mungu akubariki sana



Mungu anakuwazia mema


Mungu anataka ulishike neno lake na kulitii na kuliishi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*