JIHADHARI NA MAJUTO YA NDOA
JIHADHARI NA MAJUTO YA NDOA
Mwl.Peter Francis
Masanja
0744056901
✍ UKIPANDA KWA MWILI UTAVUNA UANGAMIVU
HISIA ZA MAPENZI ZINAKUFANYA UKOSEE KUOA AU
KUOLEWA .
Acha vijisababu
visivyokuwa na mashiko katika kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa .
📖 Siwezi kumwacha
kwa sababu tumetoka mbali sana
✍ Mungu akikataa
amekataa wewe ng'ang'ana utavuna ndoa ya majuto .
📖 Siwezi kumwacha
kwa sababu nimegharamia mno acha nimuoe tu 🙆🏻♂
✍ gharama unayoiona
inakusukuma umuoe mtu ambaye si sahihi ni sawa na kumlipa pesa jambazi aje
akukate mapanga .
📖 Nampenda mno
lazima nimuoe au anioe
✍ Badilisha maamuzi
unaweza ukampenda mtu lakini kama Mungu amemkataa acha kabisa itakuwa ni majuto
kwako .
📖 Sipati usingizi
kwa sababu yake .
✍ Wewe ndye unajikosesha
usingizi kwa jambo ambalo Mungu kalikataa unalazimisha kwa hisia za mwili wako
Acha utavuna ndoa ya
majuto .
📖 Namwona yeye tu
sioni mwingine .
✍ Acha uongo , hisia
zisikutawale msikilize Mungu nini anasema juu yako .
Epuka ndoa ya majuto .
📖 Nimenfia
✍ Usiseme umemfia mtu
ambaye siye sahihi utakufa ndani ya ndoa .
📖 Namsikia
akitembea moyoni mwangu .
✍ Acha uongo subiri mume
au mke ambaye Mungu kamwandaa kwaajili yako , mwili wako usikuendeshe.
📖 Nitaolewa na
aliye nizalisha .
✍ Kuzalishwa siyo kigezo
cha kuwa huyo ni wako ambaye Mungu alikupangia , tambua hata ulipozalishwa
ulimkosea Mungu .
Tulia subiri Mume wako
toka kwa Mungu .
📖 Hakuna kijana
aliye mwaminifu siku hizi
✍ Kauli hii ukiishika
itakuletea ndoa ya majuto , utamtilia mashaka mwenzi wako .
🖊 KWANINI VIJANA
WENGI WANACHAFUANA KABLA YA NDOA ❓
✍ Kuchafuana kunaleta
ndoa ya majuto .
Ø ZIPO SABABU ZA KIMWILI AMBAZO
VIJANA WENGI HUDHANIA NI FAHARI KUMBE NI MAJUTO BAADA YA KUINGIA KWENYE NDOA .
1. Wanaimarisha
mahusiano ( urafiki wao )
2. Kujamiana ndiyo uhakika wa kwamba unampenda
mwenzako .
3. Kujamiana kabla ya ndoa ni kumfanya mwenzako
atulie kwako asiende kwa wengine .Eti umfanye awe wako tu .
4. Baadhi
ya wasichana huona ndiyo njia ya kumfanya kijana wa kiume amkubali lakini
mwisho wake anaishia kuachika .
5. Wasichana hujamiana ili wapate mimba na
mwishowe wang'ang'anie kuolewa na mwanaume kwa kisingizio cha mimba .
🖊 MADHARA YAKE
📖 Baadhi ya
wasichana wanadharauliwa na kuachika na kuachwa na maumivu makali hata mimba
pia.
📖 Kukosa hofu ya
Mungu .
Wanamkosa Mungu
Mwanzo 39:9
✍ Zinaa ni dhambi
inayomtoa Mungu kwa mtu na kumwacha peke yake .
📖 Kuondoa akili (
ufahamu mzuri ) .
Mithali 6:32_33
📖 Hata wakiingia
kwenye ndoa bila toba ndoa yao Mungu ataitapika kwa sababu hawajautubia
uasherati wao .
Waebrania 13:4
📖Wakizaa watoto
katika hali hiyo , watoto wao watakamatwa na roho ya uzinzi /uasherati , na
matokeo yake utaona binti zao wanazalia nyumbani bila kuolewa .
Zaburi 51:5
✍ Unapoona mwanao
kazalia nyumbani jihoji wewe kabla ya ndoa hukuwa mwasherati na je ulitubu ❓
Kama hukutubu
umehatarisha maisha ya wanao kwenye eneo la ndoa .
📖 Haya yote
ukiyaepuka utakuwa na ndoa isiyo na majuto .
✍ Utasikia binti
anaambiwa Usipo nipa sikuoi nakuacha maana naona umenibania 🤣🤣🤣🤣
Mwambie kwamba
nashukuru kwa sababu Mungu kanidhihirishia kwa maono kuwa wewe hunifai nenda
kwa makahaba watakubali unavyotaka ,mimi namsubiri mume wangu toka kwa BWANA.
NITAMJUAJE KAMA NDIYE WANGU KUTOKA
KWA MUNGU ❓
✍ Swali hili ni zuri
sana na ni rahisi sana kwa kulijibu
📖 18
Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye.
Mwanzo 2:18
✍ Vijana wengi hukosea
ramani kuisoma hasa wanapotaka wenzi wa ndoa .
[✍
Kumpata mwenzi sahihi lazima ufuate kanuni kama mtu asomavyo ramani , kuna
ufunguo ( kiongozi ) ambaye ni Mungu
Kazi yake ni
kukuonyesha yule unayemkusudia amebeba nini kiroho , amebeba tabia zipi na
vipaumbele gani katika maisha yake .
Je hivyo vitu
vinaelekeana na vyako ❓
3 Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Amosi
3:3
✍ Mungu hajaahidi
kukuletea mtu asiyefanana na wewe lakini akili zako na macho yako ( mwili)
ukiufuata unaweza ukakuletea mtu asiyesahihi kabisa na kujutia kuoa au kuolewa.
✍ Aliye sahihi mtaendana
interest ( vitu mvipendavyo ) siyo huyu anapenda miziki ya kidunia halafu wewe
unapiga kwaya hiyo ndoa itakuwa ya kisiasa , chama tawala na chama pinzani .
✍ Huyu haamini kuwa
zinaa inashindwa halafu wewe unaamini na unaipiga vita , hapo ujue kabisa huna
mtu jifariji ujuavyo .
✍ Wewe unafunga na
kuomba yeye hizo habari anazipinga hawezi kujitesa , hapo pia ujue unaoa au
unaolewa na mtu asiye na maono mda wowote utalia .
✍ Wewe ukiongelea mambo
ya kiroho anakuingizia mambo ya kidunia kubishana na wewe , huyo siyo wa
kufanana na wewe .
: ✍
Aliye sahihi mtania mamoja , mtaombea mahusiano yenu , atakushauri mambo ya
kiroho na kukuambia piga injili mpaka dunia ishangae .Atakushirikisha ratiba na
mambo ya kiroho anayojifunza .
Mtacheka 🤣🤣mtafrahi
, mtaimba Zaburi .
Kila mtu atamkumbuka
mwenzake na kumwona wa thamani sana na ni zawadi toka kwa Mungu
✍ Siyo unakuwa na mtu
anajifanya kaisari mpaka na shetani anamshangaa amezidi viwango
Baada ya wiki kaingiza
gia ya kwazo mpaka utajuta kumjua .
USIVAE SHELA BILA KUTUBIA ZINAA
✍ Kama mmejuana kabla ya
ndoa msivae shela harusini Mungu ataiadhibu ndoa yenu .
✍Tubuni ndiyo mvae hiyo
shela ili ndoa yenu isiwe ya majuto .
✍ Kwanini shela
isivaliwe na watu ambao wamejuana kabla ya ndoa ❓
✍ Kwasababu tafsiri ya
kuvaa shela ni ubikra , je unapoivaa halafu hujatubia zinaa humdhihaki Mungu ❓
Hapo ndiyo maana ya
kwamba usivae shela kama mmejua kabla ya ndoa, tubu ili uvae usipotubu ndoa
inaweza ikapigwa .
Mungu akubariki sana
nitaendelea siku nyingine kwa ufafanuzi zaidi
Maoni
Chapisha Maoni