📖 JINA ULILOPEWA LINA MAANA GANI KIROHO ❓


                📖 JINA ULILOPEWA LINA MAANA GANI KIROHO ❓
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
📖 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Yohana 17:12
Yesu alipewa jina kubwa sana kiroho na jina lenye nguvu za kuokoa litajwapo mashetani hutetemeka.
Jina la Yesu lina mamlaka na nguvu za kushinda ufalme wa giza.
📖 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Yohana 17:11
 Jina ulilopewa yaani jina la ukoo lina maana gani ❓
Kuna majina ya ukoo yanaambatana na miungu ya ukoo
Jina ulilopewa nyumbani yaani jina la asili linaweza likawa limebeba tabia mbaya na roho za miungu zitakazo sumbua maisha yako.
Jina la ukoo lina tabia , fuatilia kujua tabia zake, Unaweza kupewa jina la babu yako aliyekuwa mganga , mchawi, mlevi , mzinzi , mgomvi n.k halafu hizo tabia zikajitokeza kwako pia .
Shughulikia tabia chafu za jina ulilopewa
 📖 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Wafilipi 2:9
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
Wafilipi 2:10
Yesu alipewa hilo jina likiwa na maana kubwa sana na nguvu za kuokoa
Jina lipitalo kila jina
Jina lenye nguvu kupita majina yote .
 Ombea jina lako ulilopewa na ukoo wako inawezekana kunashida inakutesa kwa sababu ya jina ulilopewa.
Kuna watu wanaitwa Shida , mateso , na wengine majina ya wanyama wamejikuta wanapata ugumu katika maisha yao .
 Tumia jina la Yesu kufuta tabia chafu za jina ulilorithi
 Kuna wengine walinunua majina ya watu kusomea , futa tabia chafu za hilo jina .
Haiwezekani usomee jina la mtu bila kujua tabia zake ,
Aliachaje shule na kwanini aliacha
Usije ukaanza kupata misukosuko katika masomo kama yake .
Kumbuka wengine waliacha masomo kwa sababu waliugua sana  mara kwa mara .
Unaweza ukalirithi hilo jina ukawa wa kuugua mara kwa mara .
 Nakutakia asbh njema .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*