LAZIMA UJUE TOFAUTI KATI MTU NA MWANADAMU


 🍇 LAZIMA UJUE TOFAUTI KATI MTU NA MWANADAMU 🍇
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829

Mtu anatabia ya kimungu ndani yake .Amebeba utu ( matendo ya haki ).

Mwanadamu amebeba tabia za mnyama ( anatenda mambo kama mnyama ) .Kila kitu kwake kufanya ni sawa tu .

  Mwanadamu anaroho ya uasi ndani yake na anafanya uadui na Mungu .

📖 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:26

Mtu anasura na mfano wa Mungu yaani utendaji wake ndani yake .
Mwanadamu yeye anaunyama ndani yake

Akijisikia aoe wake wengi anaoa , akijisikia akalewe au akanunue makahaba anaenda tu kwasababu anasifa kama mnyama .

 📖 1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
Mwanzo 6:1
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6:2
3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Mwanzo 6:3
  Katika kitabu cha Mwanzo 6:1_3 , Mungu anawazungumzia wanadamu kwa tabia ya kinyama na siyo tabia ya utu ( kutenda kama Mungu atakavyo ) .


Hajasema kwamba hatashindana na mtu au watu

Amesema hatashindana na mwanadamu ( wanadamu ) .
Mungu pia anasema watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa hajasema wanadamu wanaangamia kwa kukosa maarifa .
 📖 6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Hosea 4:6
Alizungumzia watu akimaanisha wanaofuata sheria zake ( watakatifu ) .
Ndyo maana leo pia tunaona makanisani kuna wanadamu wamejiingiza huko kuleta roho ya uasi .
Ndyo maana leo tunaona mtu anachumbiwa na mwanadamu na siyo mtu 🤣🤣🤣🤣
Hakikisha marafiki zako ni watu na siyo wanadamu ,wanadamu hawana utu
Hakikisha mchumba wako awe mtu asiwe mwanadamu
Akiwa mwanadamu atatenda kama mnyama na haoni aibu kukufanya mke wa pili .
🙏Somo limeishia hapo 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*