MAOMBI YA TOBA JUU YA URITHI MBAYA
MAOMBI
YA TOBA JUU YA URITHI MBAYA
SEHEMU YA KWANZA
Mwl.Peter
Francis Masanja
0679392829
0744056901
5
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu
mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha
nne cha wanichukiao,
Kutoka
20:5
Bwana
Yesu asifiwe.
Karibu
sana katika mwongozo wa maombi haya ambayo nimeyaandaa ili yaweze kukusaidia
katika maisha yako na rafiki zako pia .
Roho
wa Mungu amenigusa kuandika haya maombi ili yaweze kukufungua pale unapoona
kuna shida lakini umeshindwa kujua namna ya kuingia katika toba.
Katika
maombi haya nataka nikupe onyo kwanza kwamba maana ya toba ni kukubali kuachana
kabisa ulichokuwa unakitenda na kuamua kukaa karibu na Mungu muumba mbingu na
nchi,aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nakusihi
sana na narudia kukusisitiza kwamba unapotubu hakikisha hurudii tena hiyo
dhambi.
Maishani
mwako kuna mambo mengi sana ambayo yanamchukiza Mungu na mengine uliyafanya kwa
makusudi ukisema kwamba utatubu tu bado upo kwenye neema.
Pia
kuna mengine ambayo wewe hukuyafanya katika maisha yako lakini yalifanywa na
ndugu zako au wazazi wako .Mungu akaachilia adhabu juu ya maisha yenu katika
familia yenu au ukoo wenu.
Adhabu
za kurithi ni pamoja na magonjwa na tabia ambazo ni aibu mbele za Mungu na
mbele za watu kuzisimulia kabisa maana hazifai kuigwa hata na watoto wako au
jamii inayokuzunguka.
Basi
leo naomba tushirikiane kuomba kwa pamoja maombi haya ili upate kufunguliwa
popote ulipo.
Nakuomba
sana uyasome maombi haya ili uweze kufunguliwa kwenye shida na mitego
mbalimbali ambayo shetani ameiweka juu yako ili akutese.
Nikukumbushe
kwamba mateso mengi anayopitia mtu ni matokeo ya dhambi.Mfano kuna baadhi ya
dhambi kama utoaji mimba na ukahaba huwa zina matokeo mabaya sana katika ukoo
na ndiyo maana utakuta kuna ukoo watoto ni makahaba au wazinzi sana kuanzia
kipindi wanapopevuka tu wanaanza kuwajua wanaume bila aibu kabisa.
Pia
utaona jinsi gani watu wanaotoka kwenye hizo familia wengi mahusiano yao huwa hayadumu
na ndoa zao huwa za tabu sana.
Kabla ya kuyatumia maombi haya
hakikisha unamwimbia Mungu wimbo wa kuabudu.
MAMBO YA KUOMBEA TOBA
Ø Zinaa
Ø Kuabudu miungu mingine kama vile
kwenda kwa waganga.
Ø Ardhi ambapo unaishi kwa sasa.
Omba toba juu ya miungu inayoabudiwa
mahali hapo kwa kujua au kutokujua.
Ø Ardhi ya nyumbani ulipozaliwa.
Ø Ardhi ya eneo unapofanyia kazi.
Ø Ardhi ya Kanisa unapoabudia.
Ø Tabia mbaya ulizorithi kutoka kwa
wazazi
Kuna
tabia za wazazi wetu kweli haziridhishi na hazifai kuigwa kabisa.
7
Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.
Maombolezo
5:7
Ø Majina ya kurithi.
Kuna
baadhi ya majina ya kabila mtu anayopewa yanaambatana na miungu ya ukoo na roho
za miungu kama vile uchawi na ushirikina ,ulevi,ukahaba,uzinzi,n.k
Hakikisha
sana unaomba toba juu ya majina hayo na kuondoa kabisa uhusiano wa hayo majina
na tabia chafu, uhusiano wa hayo majina na roho za miungu ,uhusiano wa hayo
majina na roho za magonjwa na umaskini,n.k.
Kuna
baadhi ya watu wamepewa majina ya wanyama ,hii imewafanya wawe na tabia kama
wanyama hao na kujikuta wanafanya mambo ya kuchukiza yaani maovu.
Ø Nafasi ya kazi uliyoirithi
Kuna
nafasi nyingi za kazi mtu hurithi baada ya kutoka mtu aliyekuwa katika nafasi
hiyo.Nafasi hizo huwa zinamatatizo kama mtu aliyetangulia alitenda dhambi na
adhabu ikaja katika eneo hilo kuleta mateso.
Zipo
ofisi na kampuni ambazo ma meneja huwa wakija baada ya miezi michache
wanakimbia kazi au wanakufa kabisa ,hii ni kwasababu katika nafasi hiyo kuna roho
ya uharibifu imemwagwa ili kila atakayeikalia apate mateso.Omba toba juu ya
nafasi ya kazi ambayo umekuta mtu kahama au kafariki halafu wewe ukaenda
kuichukua.Usiingie kienyeji ukakaa tu .Takasa ardhi ya hapo na kuondoa miungu
iliyosimama mahali hapo kufanya vita na kiti ulichokikalia .
Angalia
Daudi alipoichukua nafasi ya Sauli kutawala ,kulikuwa na njaa kubwa sana katika
Izraeli kwa sababu ya Sauli.
Daudi
aliona njaa inazidi kutesa utawala wake ikabidi amwulize Mungu .Ndipo akaambiwa
ni kwasababu ya Sauli.
1
Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye
Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa
nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
2
Samweli 21:1
Usipuuzie
matatizo unayoyaona yanajirudia katika nafasi unayoikalia,mwulize Mungu .
TWENDE TUINGIE KWENYE MAOMBI
NAKUOMBA UYASOME UMAANISHE
1.Toba binafsi
Ee
MUNGU baba ,nimekuja mbele ya kiti chako cha rehema ,nakushukuru kwa kuwa
umenjalia uzima na afya .Ninakushukuru kwa kuwa wewe ni mwema,umenichagua hivi
leo kuzungumza na wewe sawasawa na ISAYA 1:18-19
18
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana,
zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama
sufu.
Isaya
1:18
19
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya
1:19
Ninakuja
mbele zako maana nimesikia habari zako kuwa wewe ni Mungu unayesamehe na kufuta
makosa ya wakuitao.
Ninaomba
toba juu ya dhambi zote nilizozitenda kwa kujua na kutokujua .Nakuomba
unirehemu ,unioshe kabisa kwa damu ya Yesu .
Maana
nimejua ya kwamba nimekukosea na hasira yako ikawaka juu yangu.
Ninakuomba
,kuanzia sasa,unisafishe ,unitakase,unioshe dhambi zote nilizozitenda ,katika
jina la Yesu ,nakusihi Ee Mungu unisamehe kabisa sawasawa na ZABURI 51:1-10
kama ilivyoandikwa:
1
Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Zaburi
51:1
2
Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
Zaburi
51:2
3
Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Zaburi
51:3
4
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe
ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Zaburi
51:4
7
Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko
theluji
Zaburi
51:7
8
Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
Zaburi
51:8
9
Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.
Zaburi
51:9
10
Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
Zaburi
51:10
Nakuomba
Mungu unisamehe juu ya dhambi zote kupitia damu ya Yesu nafuta dhambi za
kutumikia miungu, kutokusamehe,n.k( TAJA MAMBO YOTE ULIYOYAFANYA MWENYEWE
AMBAYO YANAMCHUKIZA MUNGU) katika jina la Yesu nakuomba usikie kuomba
kwangu.Amen
2.Toba juu wazazi na mambo yote waliyoyafanya
ukayarithi.
Katika
jina lipitalo majina yote ,jina lenye nguvu kupita majina yote la BWANA Yesu
Kristo.
Mungu
mwenye rehema ,ninakuja mbele zako nikiomba toba juu ya wazazi wangu
,inawezekana kuna maovu walikutenda na hasira yako ikashuka juu yao na juu
yangu.
Nakuomba
sasa uwasamehe na kuwaponya na kila roho ya mauti ,inayofuatilia maisha yao
,roho ya magonjwa,roho ya kukataliwa,roho ya umaskini,roho ya zinaa,roho ya
miungu n.k kwa damu ya Yesu ninafuta kila roho chafu nilizozirithi kutoka kwa
wazazi wangu,katka ukoo wa baba na ukoo wa mama yangu ,maana neno lako Mungu
linasema:
5
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba
zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka
20:5
Ninafuta
dhambi zote walizozitenda ,zikatesa maisha yangu ,ninazifuta kuanzia kizazi cha
kwanza ,na cha pili ,na cha tatu na cha nne na kuendelea katika maisha yangu kwa damu ya Yesu ,kila dhambi za urithi nazifuta
sawasawa na neno la Mungu linavyosema katika Waebrania 9:22-23
22
Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu
hakuna ondoleo.
Waebrania
9:22
23
Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini
mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.
Waebrania
9:23
Ninafuta
kila urithi wa mabaya kutoka kwa wazazi wangu kwa damu Yesu ,ninajitoa huko mwili wangu,nafsi yangu,na moyo
wangu kila kitu kinachohusu maisha yangu natoka huko kwa damu ya Yesu.
Kila
asili na historia mbaya ya kurithi kutoka kwanza wazazi wangu naifuta kwa damu
ya Yesu sawaswa na Ezekieli 16:3-6,9
3 useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu
hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori
alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.
Ezekieli
16:3
4
Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako
hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo,
wala hukutiwa katika nguo kabisa.
Ezekieli
16:4
5
Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa
kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa,
katika siku ile uliyozaliwa.
Ezekieli
16:5
6
Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia,
Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu
yako, uwe hai.
Ezekieli
16:6
9
Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka
mafuta;
Ezekieli
16:9
Kwa
damu ya Yesu ,nafuta kila asili mbaya inayotesa maisha yangu,katika jina la
Yesu ,Ee Mungu usikie kuomba kwangu ,maana wewe ni kimbilio langu na mwamba wa
wokovu wangu na wewe pekee ndye msaada wangu ,nifunike kuanzia sasa na hata
milele.Amen.
MUNGU AKUBARIKI
SANA
Nakuomba
uendelee kufuatilia somo la maombi haya
Pia waweza
kunipigia simu kwa ushauri na maombi
0744056901/0679392829
Nimebarikiwa sana na maombi haya,Mungu wa Mbinguni azidi kukuinua zaidi na zaidi Mtumishi
JibuFutaAmina mtumishi kwenye maombi haya ukoo wangu kuna mambo ya kurithi yanatuumiza hasa wanawake ukiolewa ni matatizo kila kukicha. Ukifika miaka arobaini ndoa zinavunjika
JibuFuta