NAJUTA KUMJUA
😭 NAJUTA KUMJUA 😭😭
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
✍ Ni ujumbe mzito
uliojaa simanzi na kuchoma mioyo ya vijana .
Maadamu upo duniani wewe ni kijana kuna watu ulijuta
kuwajua .
Unaona ni heri usingewajua kabisa ukawa na amani
moyoni mwako .
Naam , hii ndiyo dunia tambua hujaja duniani kuishi
bila kukutana na upinzani.
Unaona ni heri usingewajua kabisa ukawa na amani
moyoni mwako .
Naam , hii ndiyo dunia tambua hujaja duniani kuishi
bila kukutana na upinzani.
Kuna wakati Mungu alijuta kumweka Sauli awe mtawala
mpaka akachukua maamuzi magumu ya kumng'oa kwenye ufalme na kumchagua Daudi
atawale .
Wewe wajuta kuwajua baadhi ya watu , tambua kuna
wakati Mungu anajuta pia kukuita wewe mwanaye .
📖
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma,
asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana
usiku kucha.
1
Samweli 15:11
Kuna wakati kweli unajuta kuwajua baadhi ya watu kwa
sababu wamekuingiza katika shida na tabu , maisha yako wameyaweka matatani
yamekuwa magumu.
Lakini nakuambia usijutie hilo ni fundisho
utafundisha na wengine wapate kujihadhari namna ya kuchagua marafiki wa
kuambatana nao .
Mungu alijuta kwanini alimchagua Sauli atawale ,
mpaka akamtumbua madarakani kwa nguvu .
✍ Inawezekana na
wewe kijana Mungu anakuangalia na kujuta kwanini ulikiri kuacha dhambi siku
unampokea Yesu ukisema ninamkataa shetani na kazi zake zote .
Lakini anakuangalia anakufananisha na Sauli .
Kuna wakati pia hata wewe unajuta kwanini uliolewa
na yule au kwanini ulimuoa huyo , yaani anakusumbua na kuleta mawazo kwako kuna
wakati unawaza ukimbie .🏃🏻♂🏃🏻♂
Majuto unayopitia Mungu ameyaona atayatatua ,
huhitaji kujuta omba Mungu akupe amani maana yeye ni Mfalme wa amani .
JEHOVAH SHALOM
✍ Kuna wakati pia
unajuta kumjua rafiki yako wa kiume yaani boyfriend alikupa ujauzito
akakutelekeza .Akakuachisha masomo
Sikiliza
usijute binti , yupo Mungu amekuandalia mume wako wakati ukifika hutaona
kujuta kwako .
Na sasa nakuambia acha kujuta .
Yupo Mungu mpaji anampa mtu apendavyo
JEHOVAH JIREH
📖 20 Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye
amebariki, nami siwezi kulitangua.
Hesabu-Numbers
23:20
: ✍
Balaamu alitumwa akawalaani Israeli lakini akakutana na neno la Mungu
limesimama kinyume chake .
Alipotaka kuweka laana akakuta zimewekwa baraka .
✍ Adui yako
ukimjua wewe sema na Mungu tu , huhitaji kujuta kumjua acha Mungu amshughulikie
.
✍ Aliyekusaliti
usijute kumjua shukuru kumjua kwasababu ungeendelea naye angekuua , tambua
Mungu kakuepusha na matatizo .
✍ Cha kujutia
duniani ni anguko yaani dhambi , yakupasa utubu na kuiacha kabisa maana inatoa
uhusiano wako na Mungu .
📖 9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;
Uzifute hatia zangu zote.
Zaburi
51:9
11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako
mtakatifu usiniondolee.
Zaburi
51:11
✍ Dhambi pekee
inakuletea majuto kwa sababu inamwondoa Mungu kwako .
✍ Adui ni mtaji
na ni mtumwa wako wa baadae ,
Usijute kumjua anayekupiga vita
Vita vya maneno , na kukufanyisha kazi ngumu au
kukudhihaki baada ya kukufanyia ubaya akaanza kukucheka 🤣
Ipo siku atakuja analia umsaidie .
✍ Yusufu ,
aliuzwa Misri kwa Potifa kuwa mtumwa lakini alifanikisha nyumba ya Potifa mpaka
akaambiwa vitu vyote aguse lakini mke asiguse.
Yusufu alipata kibali machoni mwa Mungu pamoja na
majuto aliyopitia .
✍ Hata wewe leo
mtu aliyekuumiza ni sawa na mmisiri tu lakini ipo siku atakuona umeinuliwa na
ataanza kushangaa
Na kuanza kusema Oooh huyu alikuwa rafiki yangu
lakini saivi mmmmh kafanimiwa mno au kaolewa au kaoa.
📖 Kisha Bwana akawapa raha pande zote,
sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote
hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye Bwana akawatia adui zao
wote mikononi mwao.
Yoshua
21:44
: ✍
Mungu atakupa raha isiyokoma , na yule aliyekufanya ujute hutamkumbuka tena.
✍ Historia ya
aliyekuumiza nafsi yako , yaani aliyekuingiza kwenye tabu na dhiki utaisahau
saa inakuja Mungu atakujaza furaha na mafanikio .
✍Hupaswi kusema unajuta kumjua , cha kufanya muombee
ipo siku atakuja kutambua kwamba alifanya makosa na atatubu .
Ipo siku atakukumbuka hupaswi kujuta .
✍ Kuna wakati
Mungu anamleta yule aliyekufanya ujute ili audhihirishe ukuu na uweza wake
.Akutoe kwenye hiyo shida ili liwe fundisho kwa wengine wapate kumwamini kuwa
yeye yupo .Na yote kwake yanawezekana .
📖 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa
Mungu.
Luka
1:37
✍ Unayejuta
kumjua pia atakuja apate fundisho kupitia wewe .
Mungu anakuwazia mema kila wakati
Yeremia 29 :11
Asantee tutakutana siku nyingine kuendeleza somo
hili .
Najuta kumjua
✍Ndiyo ujumbe wa
leo ambao unazungumzia mambo yanayogusa mioyo ya watu na kujutia kuwa na
marafiki wabaya
Lakini ni fundisho kwa uliyemjua na kwako pia
ikifika saa ya kuinuliwa kwako .
✍ Faida ya ujumbe
huu ni kuwa
Marafiki waliokuumiza ni fursa ya kuinuliwa kwako .
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni