TAHADHARI KWA BINTI ZETU
TAHADHARI
KWA BINTI ZETU
Kutoka kwa MWL.Peter Francis Masanja
Vashti alikuwa mwanamke mrembo , yaani mzuri sana wa
kuvutia
Uzuri wake ulimfanya amdharau mumewe
Mfalme
Ahasuero
Tupo katika
dunia hii ambayo mwanamke akisifiwa mzuri na kila mtu anaweza akamdharau mumewe
akisema hata mkiachana yeye hatachelewa kupata bwana .
✍ Uzuri na mvuto
wa mwanamke hauifanyi ndoa idumu bali tabia njema ndyo uimara wa ndoa .
✍ Esta , alikuwa mwanamke mrembo mzuri sana na kila
mtu alimtaka naye alijua kabisa kuwa ni mzuri
Lakini Esta alikuwa mwombaji na mwombolezaji ( mcha
Mungu ) , mpole ,mnyenyekevu , mtiifu,
na mwenye kumsikiliza mumewe na watu wote .
Ahasuero akamuoa mrembo Esta akaachana na Vashti .
✍ Uzuri wa
mwanamke bila kujitoa kwa Mungu haunafaida kabisa na huambulia kuwa pango la
wazinzi na waasherati.
📖 11
wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili
kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.
Esta
1:11
12
Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa
wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake
ikawaka ndani yake.
Esta
1:12
Vashti alika
alimdharau mumewe
Hii ni kwa
sababu alijiinua sana huyu Vashti
✍ Lakini Esta,
mwanamke aliyejaa upendo , huruma , upole , utii, na ucha Mungu na uzuri wake
alisifika sana na akawa mkombozi wa watu .
📖 7
Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana
baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo mzuri na uso mwema ; nao
walipokufa baba yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake yeye.
Esta
2:7
8
Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi
wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa
katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
Esta
2:8
9
Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa
vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa
nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali
pazuri katika nyumba ya wanawake.
Esta
2:9
15
Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye
alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile
vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake . Naye
huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona .
Esta
2:15
16
Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero,…
MUNGU AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni