UHUSIANO KATI YA ZINAA NA MIUNGU YA KIGENI ,KATIKA KUHARIBU NDOA NA UCHUMI WA MTU
UHUSIANO KATI YA ZINAA NA MIUNGU YA KIGENI ,KATIKA KUHARIBU NDOA NA
UCHUMI WA MTU
Mwl.Peter
Francis Masanja
0679392829
Kutoka
:
Mtwara
_Tanzania
📖
Kuna hirizi kwenye ndoa za vijana wa leo zinatakiwa zitolewe Hirizi hizo
zimewafanya vijana wakwame kiroho na kiuchumi.
✍ Ni kweli ulizalia
watoto nje ya ndoa takatifu , ndyo maana maisha yako ni ya tabu sana .
Ukiambiwa
zinaa ni mbaya kabla ya ndoa unasema utatubu pole sana .
Zinaa
inakatibisha adui aue kila kitu kinachohusu maisha ya mtu
✍Kuna
koo ambazo wanahistoria ya uganga , na uzinzi na wameokoka lakini
hawakutengeneza , wamekwama sana .Mpaka inatia huruma
✍Uchumi
wako unapimwa kwenye hali yako ya ndoa , na Mungu huzipiga sana ndoa zilizoanza
na uzinzi halafu wakaacha kutubu na kujitoa kwenye dhambi hiyo .
Unaponificha
mimi mchungaji kuwa hamjajuana kabla ya ndoa , ujue ndoa yako itapigwa sana
✍Wafuatao
ndoa zao hupigwa wasipotubu .
📖
Wanaoitana baby ,sweet, honey n.k kabla ya ndoa
📖
Wanaopeana busu wakati si make na mume.
📖Wanaojamiana
kabla ya ndoa
Hawa
wote wasipotubu ndoa zao matatani
Na
uchumi wao mgumu .
✍ Utasema Peter
anafundisha ndoa kila siku sasa sikiliza nikwambie leo
Ndoa
ikiwa ngumu uchumi hupigwa pia .
Ndoa
ikipigwa na uchumi hupigwa pia .
✍
Kuna watu walikuwa na dira ya maisha lakini walipojichanganya wakaoa watu wasio
sahihi hawajajenga mpaka sasa uchumi wao mbovu .
✍
Katika zinaa huja roho ya miungu
✍Hakuna mwenye roho ya
miungu aliye na amani kila siku yeye hofu na mateso.
✍
Mbaya sana , kuna miungu ya kabila, ukoo na familia
✍ Kuna miungu ya waganga
ambao walikuja kufanya tambiko na mazindiko kwenye familia ya huyo mtu
unayezini naye hujui kama aliitoa au la .
✍
Hujui masharti ya hiyo miungu yalikuwaje kuhusu uchumi au ndoa kutoka kwenye
ukoo wa huyo mtu .
✍ Na wewe bila wasiwasi
wazini kabisa ukijiona upo salama kuwa
wewe ni mjanja kumbe umekufa .
✍
Madhara ya zinaa yanapiga ndoa kwanza inakuwa na vurugu kisha uchumi unapigwa
mpaka utashangaa .
✍ Watu hufikiria
kutumikia miungu mpaka uende kwa waganga tu hata kwa kukutana na wapenzi kabla
ya ndoa unaweza ukaunganishwa kwenye madhabahu ya kabila , ukoo au familia
inayotumikia uganga na ushirikina na uchawi .
Sasa
umejiingiza na umebeba maagano na roho za huyo mtu utaumia sana na huwezi
kufanikiwa kimaisha .
✍
Unaweza ukajihisi wewe huendi kwa waganga kumbe ulipozini na mtu mwenye maagano
ya uganga ,na uchawi ulibeba kila kitu toka kwake na ndyo maana umekwama
husongi mbele.
✍
Ukianzisha mradi wa kuku kuku wanakufa , hawatagi mayai .
✍ Ukifuga ng'ombe
hawazai wanakuwa na afya mbaya .
✍
Mshahara wako unauona hautoshi kwa sababu umebeba roho ya uganga kutoka kwa mtu
uliyezini naye
✍
madeni yamekuwa mengi mpaka unajikuta mshahara unaishia kwenye madeni
Unakuwa
mtu wa maisha ya kukopakopa yaani roho ya madeni
✍ Tafakari umezini na
wangapi na uyajue majina yao uingie kwenye toba uondoe roho zao ndani yako taja
majina yao amru waachie moyo wako na mwili wako ili uwe huru .
✍
Umelala na wanawake 19 _30 kabla ya ndoa na ndoa yako inasumbua ingia kwenye
maombi orodhesha majina ya watu hao tubu na uvue roho zao kwa kuwataja .
📖 1
Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao,
wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa
Wahiti,
1
Wafalme 11:1
2
na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie
kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani
akaambatana nao kwa kuwapenda.
1
Wafalme 11:2
3
Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze
wakamgeuza moyo.
1
Wafalme 11:3
4
Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate
miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama
moyo wa Daudi baba yake.
1
Wafalme 11:4
5
Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo
la Waamoni.
1
Wafalme 11:5
6
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa
utimilifu, kama Daudi baba yake.
1
Wafalme 11:6
✍
Aliyejuana kabla ya ndoa na watu wengi hana upendo ndani yake ,hajui kupenda na
hawezi kumpenda mwenzi wake kwa sababu moyo wake umebeba miungu ya kigeni
kutoka kwa watu aliozini nao .
✍
Unaweza ukasema huna ndoa za wake wengi kumbe Mungu anakutambua kuwa unawake
wengi au unawaume wengi japo kimwili unaonekana una mmoja
✍ Hii ni kwa sababu roho
za watu uliozini nao kabla ya ndoa zipo ndani yako zinafanya vita na ndoa yako
zinapambana na mwenzi wako wa ndoa zimeugeuza moyo wako umdharau na kutompenda
kabisa
✍
Suleiman alipooa wake wengi moyo wake uligeuzwa akatumikia miungu mingine
Vivyo
hivyo na mtu ambaye hakutubia zinaa kabla ya ndoa moyo wake umetekwa na roho za
wapenzi wake wa zamani .
✍
Na Mungu huachilia adhabu kwenye ndoa za aina hii wasiposhtuka wanaweza kufa
mapema sana wakiwa maskini kabisa .
✍ Mungu anapoziadhibu
ndoa zilizoanza na uzinzi ambazo wanandoa walificha dhambi hupiga pia na
uchumi.
📖
12
Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako;
nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.
1
Wafalme 11:12
13
Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya
Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.
1
Wafalme 11:13
✍ Adhabu aliyoipata
Suleiman ilikuwa ni fundisho kwa wengine
Ufalme
wake aligawanywa na makabila mengi yakatawaliwa na mtumwa wake .
Mtoto
wake akapewa kabila moja tu na hii ni kwa sababu Mungu alimkumbuka Daudi
mtumishi wake .
📖
8
Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao
au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli?
Waamuzi
5:8
✍ Vita uliyonayo kwenye
ndoa yako ni kwa sababu ya miungu ya wapenzi wako wa zamani ambao ulifanya
agano nao na hujatubu na kuwaondoa mwilini mwako .
✍
Malango ya ndoa na ya uchumi yamekwama , kuna vita kali
📖
16 Bwana akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa
wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa
kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao.
Kumbukumbu
la Torati 31:16
17
Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha
uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata
waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu
hayumo kati yetu?
Kumbukumbu
la Torati 31:17
18
Nami nitawaficha uso wangu kwa kweli siku hiyo, kwa maovu yote waliyoyafanya,
kwa kuigeukia hiyo miungu mingine.
Kumbukumbu
la Torati 31:18
✍
Wapenzi uliozini nao kabla ya ndoa miungu ya makabila yao inafanya vita kwenye
uchumi na ndoa yako pia kwasababu hujatubu na kuondoa roho za miungu yao bado
umeunganishwa kwenye ibada za miungu yao huko
Na
Mungu anakupiga bila wewe kujua sasa leo zinduka 🤣🤣🤣🤣
📖 14 Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa
kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.
Kutoka
34:14
15
Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu
yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.
Kutoka
34:15
16
Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao,
wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.
Kutoka
34:16
✍
Kila mwanamke au mwanaume unayekutana naye kimwili anakuunganisha kwenye
madhabahu ya kabila lake, ukoo wake , na familia yake , na wewe unakuwa wa huko
kama kuna uchawi na uganga na ndoa za wake wengi na ulevi hayo yote yatakuwa
yako na yatakutesa mpaka utatamani kuikimbia ndoa yako na uchumi wako utakuwa
mgumu sana .Kwa sababu umeunganishwa kutumikia miungu mingine na hasira ya
Mungu ipo juu yako .
✍ Chukizo lingine
linalopiga ndoa na uchumi wa mtu
Ni
kuzini na wafuatao :
👉🏻
Mzazi
👉🏻
Dada au kaka
👉🏻
Ndugu yeyote ambaye mnauhusiano wa damu ( kiukoo).
✍ Kuna watu wanazini na
watoto wa wake za baba zao wakidai ni ndugu wa mbali
✍ Ndugu ni ndugu tu
usiseme kuna undugu wa mbali utapata tabu sana kufanikiwa .Tena ni laana.
📖 6 Mtu ye yote aliye wa kwenu
asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi
ndimi Bwana.
Mambo
ya Walawi 18:6
7
Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako;
usifunue utupu wake.
Mambo
ya Walawi 18:7
8
Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
Mambo
ya Walawi 18:8
9
Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa
nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.
Mambo
ya Walawi 18:9
📖
10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao
usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.
Mambo
ya Walawi 18:10
11
Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako,
usifunue utupu wake.
Mambo
ya Walawi 18:11
12
Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu.
Mambo
ya Walawi 18:12
13
Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya
karibu.
Mambo
ya Walawi 18:13
📖 14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba
yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako.
Mambo
ya Walawi 18:14
15
Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake
huyo.
Mambo
ya Walawi 18:15
16
Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.
Mambo
ya Walawi 18:16
17
Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au
binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu
mkuu.
Mambo
ya Walawi 18:17
📖
19 Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya
unajisi wake.
Mambo
ya Walawi 18:19
20
Usilale na mke wa mwenzio , ukajitia unajisi naye.
Mambo
ya Walawi 18:20
21
Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi
jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.
Mambo
ya Walawi 18:21
22
Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
Mambo
ya Walawi 18:22
23
Wala usilale na mnyama ye yote , ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke
asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
Mambo
ya Walawi 18:23
24
Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa
nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
Mambo
ya Walawi 18:24
25
na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake,
na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa .
Mambo
ya Walawi 18:25
✍ Wazinio na ndugu zao
ardhi huwatapika na kila kitu wafanyacho hakifanikiwi , ndoa zao zinamatatizo
na maisha yao magumu mno .
✍ Kuwa makini sana
wengine wamezini na shemeji zao hii ni hatari sana .
✍ Ardhi inakutapikaje
sasa ❓
Tusome
Yoeli
1:1_18
📖 1 Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa
Pethueli.
Yoeli
1:1
2
Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya
yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu?
Yoeli
1:2
3
Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na
watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
Yoeli
1:3
✍
Mabaya yanayoendelea kwenye familia yanahistoria yake ( chanzo chake ) na mambo
mengi huenda kizazi hadi kizazi
Nani
wa kuwaambia ❓
Ni
Mungu kupitia watumishi wake .
✍ Hawa watu wanaonekana
kuna matatizo yanawatesa kwenye kabila , ukoo na familia zao .
✍Hii
yote ni kwa sababu ardhi imewatapika .
📖 4
Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na
parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
Yoeli
1:4
5
Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa
sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Yoeli
1:5
6
Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno
yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa.
Yoeli
1:6
7
Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake
kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
Yoeli
1:7
✍
Ardhi ikimtapika mtu atavuna kidogo sana au asivune kabisa .
✍
Unapata mshahara matatizo yanaibuka , mtoto kaugua ,mama kaugua n.k
✍ Maisha yako ya
mshahara hayako tofauti na yule aliyelima akavuna kidogo , usalama wako uko
wapi .
📖 8
Ombolea kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili ya mume wa ujana wake.
Yoeli
1:8
9
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana; Hao
makuhani, wahudumu wa Bwana, wanaomboleza.
Yoeli
1:9
10
Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya
imekauka, mafuta yamepunguka.
Yoeli
1:10
11
Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili
ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
Yoeli
1:11
12
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam,
miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Yoeli
1:12
13
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;
Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa
sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
Yoeli
1:13
✍ Kila kitu
unachoanzisha kinaharibika kwa sababu ya adhabu ya kuigeukia miungu ya kigeni
kwa njia ya zinaa .
✍ Na vijana wazinzi
wanahonga pesa nyingi kuliko hata sadaka .
Sadaka
anatoa shilingi miatano lakini vocha ya kumpigia kahaba anaweka ya shilingi
1500
Hana
akili kabisa .
✍
Akija kukutana na fimbo ya Mungu ndyo anatafta kuombewa
Hii
ni hatari sana .
✍
Fimbo ya Mungu ikikukosa kabla ya ndoa kwenye ndoa itakupitia tu .
Mbaya
zaidi inapiga kila kitu ✍✍✍✍✍
📖
14
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa
nchi; Waende nyumbani kwa Bwana, Mungu wenu, Na kumlilia Bwana,
Yoeli
1:14
15
Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama
uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Yoeli
1:15
16
Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko
mbali na nyumba ya Mungu wetu?
Yoeli
1:16
17
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika;
kwa maana nafaka imekauka.
Yoeli
1:17
18
Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana
malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
Yoeli
1:18
✍
Mrudie Mungu haraka sana ,kwa maana zinaa ni dhambi inayoua vitu vingi sana
maishani mwako .
✍
Dhambi hii inakuingiza kwenye ibada ya miungu ya kigeni .
Na
ukiabudu miungu ya kigeni ardhi inakutapika .
✍Hapo
mwanzo wa darasa hili nimesema kwamba
📖
Kila aliyefanya aliyezini na wapenzi wake kabla hajaoa au kuolewa ameunganishwa
kwenye madhabahu ya wapenzi wake .Kama wapenzi wake ni waabudu mizimu na
wanaendesha ndoa zao na uchimi wao kwa masharti ya mizimu na yeye huyu atapata
tabu mno .
Na
kwa sababu hiyo kama hakuwavua wapenzi wake kwa toba na kuyataja majina yao na
kuzivua roho zao amekuwa mwabudu mizimu na yeye.
Na
Mungu anaipiga sawasawa ndoa yake na uchumi wake .
✍
Pia nikasema
Wale
ambao wanajiita wachumba lakini wanaitana majina mazuri ya mahaba na kupeana
busu iwe kwa simu au vyovyote pia hawa wanazini katika fikira zao na Mungu
anawahesabu wazinzi wakubwa sana .
Nao
watubu na kuacha .
🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂🏃🏻♂
Biblia
inasema msiyachochee mapenzi mpaka yatakapoamua yenyewe ( ndani ya ndoa
MUNGU
AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni