UWEZO WA DAMU YA YESU KATIKA KUSHUGHULIKIA NA KUONDOA MIUNGU INAYOTESA MAISHA YETU
UWEZO
WA DAMU YA YESU KATIKA KUSHUGHULIKIA NA KUONDOA MIUNGU INAYOTESA MAISHA YETU
Semina
Day
2. Mwl.Grace Elirehema
Ø Unaposhughulika
na miungu ya ukoo shughulika na majina ya ukoo.Kama unatoka koo za kifalme
shughulikia miungu ya kifalme iachie maisha yako.Pia shughulika na miungu ya
eneo (miungu ya kigeni).
Ø Shughulikia
miungu ya marafiki zako na miungu ya wapenzi wako uliozini nao.
Ø Shughulika
na miungu ya ndoa za wake wengi.
WAAMUZI 5:8
“
Walichagua
miungu mipya ,Ndipo kulikuwa na vita malangoni………”
KUTOKA 3:1-14
Ø Kila
unapoomba takasa hilo eneo kwa damu ya Yesu .
Ø Misri
inayozungumziwa hapa ni ardhi ambapo unaishi
Ø Bwana
ameyaona mateso,na maumivu.Maumivu yanawasimamizi.
Ø Ombea
malango ya mafanikio.
Mtu
ana malango yake ya mafanikio.Hakikisha unapambana sana shetani asiyamiliki
malango yako ya mafanikio.
Ø Pambana
na mikono ya adui zako ikuachie.
Mungu
amekuahidi atakuingiza kwenye eneo zuri kabisa .
KUTOKA 12:1-13
Mungu
alikuwa anawasemesha juu ya sadaka.
Unapomwaga
damu ya Yesu .Mungu anashuka kuharibu kila kitu kibaya kinachosumbua maisha
yako ,kila roho za miungu na madhabahu zitaondolewa.
Kila
mahali uingiapo weka damu ya Yesu na miili ya watu wako .
Ø Achilia
damu ya Yesu kwenye nguvu za miungu na kwenye ibada za miungu.
Ø Uiachiliapo
damu ya Yesu ,Mungu anapita katika eneo hilo
KUTOKA 12:12-14
Ø Kama
adui amepita kwenye malango ,achilia damu ya Yesu ipite kuondoa kila roho chafu
( mapepo).
Ø Damu
ya Yesu inapomwagwa inafanya hukumu na kuondoa miungu ya makabila.
Ø Damu
ya Yesu ikipita huondoa
·
Maumivu
·
Mateso
·
Kilio
·
Watesi
Kuna
wakati miungu hukaa kwenye vitovu vya watu.
KUTOKA 12:23
Ø miungu
huwa inasababisha uharibifu katika maisha ya mtu kama vile
urafiki,umoja,shule,mali n.k
Mharibifu
hataharibu tena
WAKOLOSAI 2:15
Damu
ya Yesu ina nguvu za kupambana na enzi na mamlaka ya nguvu giza.
1 WAKORINTHO 5:7
Kristo
alijifunua katika agano la kale ,lakini hawakutambua,akaja kujifunua katika
agano jipya.
ZABURI 82:1,8
Katikati
ya miungu atasimama na kuhukumu
Mwambie
Mungu asimame kwenye ardhi aihukumu miungu .
DANIELI 7:26-27
Mamlaka
ya miungu itaondolewa milele.
DANIELI 5:14
Ø Unapoombea
mtu au kujiombea mwenyewe ondoa:
·
miungu ya kabila
·
miungu ya ukoo
·
miungu ya familia
·
miungu ya waganga
·
miungu ya kigeni
·
miungu ya wapenzi( uliozini nao).
WAAMUZI
10:16
Ondoa
hiyo miungu kwa damu ya Yesu.
MUNGU
AKUBARIKI SANA
Maoni
Chapisha Maoni