EPUKA MIKATABA ITAKAYOKULETEA VITA KWENYE MALANGO YAKO YA UCHUMI
📖
EPUKA MIKATABA ITAKAYOKULETEA VITA KWENYE MALANGO YAKO YA UCHUMI
Mwl.Peter
Francis Masanja
0679392829
📖
Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao
au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli?
Waamuzi
5:8
✍
Uchumi wa watu wengi umepigwa baada ya kuingia kwenye mikataba haramu (
mikataba ambayo inahusu miungu ).
✍
Milango mingi ya biashara za watu imefungwa baada ya kusaini mikataba na miungu
migeni
Unaposaini
mikataba na miungu mingine Mungu huruhusu roho ya uharibifu ipige uchumi wako .✍ Kuna vita kali sana
pale mtu anaposaini mkataba na miungu mipya .
Malango
yake ya uchumi hupigwa katika kila kona .
✍ Shambani atavuna
kidogo sana au asivune kabisa, kwenye mifugo kutakuwa na uzazi mbaya au roho za
utasa na magonjwa.
Watu
ni miungu kwa sababu wana roho , roho ya uzima na roho ya mauti .
✍ Ufanyapo agano nao
mfano kupitia zinaa uchumi wako unaweza ukapigwa sana .Pia na afya yako inaweza
kupigwa .
Mkataba
wowote utakaoufanya na mtu ( agano )
Mfano
mke au mume ana athari kubwa katika uchumi wako
Yeye
anaweza akakuvuruga akili yako usifikirie kuhusu maendeleo na kujikuta Mungu
anakuzuilia baraka usipomwombea na kumpenda .
12
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam,
miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Yoeli
1:12
17
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika;
kwa maana nafaka imekauka.
Yoeli
1:17
18
Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana
malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
Yoeli
1:18
Siku
zote ukisaini mkataba feki huzuni huingia na mambo huharibika ndani
Labani
alisainishwa mkataba na Yakobo ukamfunga 🤣🤣🤣🤣🤣
📖
32 Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na
madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na
marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu.
Mwanzo
30:32
33
Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya
mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au
asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.
Mwanzo
30:33
34
Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo.
Mwanzo
30:34
35
Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake
walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote
waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe.
Mwanzo
30:35
✍ Labani aliona jambo la
furaha sana kabla ya kusaini mkataba , lakini baada ya kusaini uchumi wake
uliporomoka sana.
✍ Vivyo hivyo na wewe
unapomkubali mtu awe rafiki yako na mshauri katika mambo yako ujue umesaini
mkataba unaoweza kukuporomosha au kukuinua kiuchumi.
Unapotaka
kuoa pia unatarajia mambo mazuri lakini kama mtu unayemuoa akiwa ni kichomi
utakuwa umesaini mkataba feki na uchumi wako utapigwa usipokaa vizuri unaweza
usijenge .
Maoni
Chapisha Maoni