*✳FUNDISHO LA ANAYETETEA UVAAJI WA SURUALI KWA WANAWAKE NI LA KUZIMU KABISA‼*

*✳FUNDISHO LA ANAYETETEA UVAAJI WA SURUALI KWA WANAWAKE NI LA KUZIMU KABISA‼*

*šŸ”µNa:Charles Richard Mwaisemba*

                 *ISAYA 30:9-10*
_Kwa maana watu hawa ni *watu waasi,* watoto wasemao uongo, *watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA*;wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, *tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo*;_

*YEREMIA 50:6*

_Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, *wachungaji wao wamewapoteza;* wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika._

Ni Muhimu kufahamu kuwa nyakati tulizo nazo ni Nyakati za hatari sana ambapo Watu watakuwa na masikio ya Utafiti wakitafuta waalimu makundi makundi watakaowahalalishia na kueleza mambo laini yadanganyayo  ambayo hayatagusa maadili au maisha yao ya kila siku. Watu watakaka wavae wanavyotaka na wanafanye wanavyotaka hivyo watapata waalimu Ambao kweli watawaeleza hayo maneno laini ya kuwapaka mafuta ili nao wajione wanaenda Sawa kumbe wamedanganywa na kudanganyika

Vivyo hivyo nyakati hizi kumetokea Wachungaji wengi wanaowapoteza kondoo zao kwa kuwaeleza maneno laini yadanganyayo kwa kufariji kwa kupotosha na Kushindwa kuwaeleza kweli ya Mungu ilivyo na ni kwasababu wengi ndio hawapendi kweli wapate kuokolewa hivyo Mungu anawaachia nguvu ya upotevu wazidi kuamini uongo huo

Moja ya mambo ambayo waalimu na wachungaji hawa wa uongo wanayatumia kuwadanganya wanawake ni katika Swala la Uvaaji wa Suruali. Fundisho hili ni mada ambayo inaweza isiishe mpaka Yesu arudi maana kila kukicha kuna mijadala isiyoisha Kuhusu hili Fundisho. Na haliwezi kuisha kwasababu wadada wengi hawapendi kuelezwa iliyo kweli wapate kuokolewa ila wanapenda kuambiwa maneno laini ya kuwafariji ndio maana Wiki hii au leo kumekuwepp na waalimu au wachungaji wanatuma makala za Kupotosha na kuwafariji wadada juu ya *UVAAJI WA SURUALI ZA KIKE* ambazo zinasambazwa kwa nguvu kubwa na watu wanaopenda uongo ma wengi wanatetea juu ya hilo. Nimeona Nijibu baadhi ya mambo Yamkini wapo walio wa Mungu watakaoponywa na Uongo unaosambazwa

Waalimu hawa wanafundisha kuwa Eti Andiko la KUMBUKUMBU 22:5 linalotukataza kama wanaume kuvaa mavazi ya kike na wanawake kuvaa mavazi ya kiume kuwa halielezi Kutukukataza kuvaa mavazi ya kiume au ya Kike  Kwa sababu alizo zitoa yeye kuwa  sababu za kutamaduni kuwa tunatakiwa tusijaji kulingana na tamaduni.n.k

Ni Muhimu kufahamu kwanza Mungu ndiye Mwanzilishi wa mavazi  na ndiye ametupa misingi mbalimbali ya kimaandiko ya kuweza kutambua ni mavazi gani yanampasa Mwanaume na mavazi gani yanampasa mwanamke hata kama watu hawa wapo katika mazingira tofauti au wapo katika vizazi tofauti..


*1⃣MAVAZI NI YA KUFICHA UCHI*
Moja ya Msingi mkuu aliouweka Mungu mwenyewe mwanzo kabisa baada ya uumbaji ni Kumpa Mwanadamu *MAVAZI YA KUJISITIRI ILI AFICHE UCHI WAPI*. Mungu ndiye aliyempa Adam na Hawa Mavazi ya Ngozi  ili wafiche uchi wao!!

*MWANZO 3:7,21*
_Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa *uchi,* wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe *mavazi ya ngozi, akawavika*._


Unafikiri kwanini Mungu hakuwaacha katika Uchi wao bali aliwafanyia mavazi ya Kuvicha Uchi?  Wewe si unasema  haangalii mavazi? Je aliyeaniosha mavazi hapo ni nani kama si Mungu? Na Mungu ndiye anataka tuvae Mavazi ya Kuficha Uchi wetu.Ukiona mtu au tamaduni yoyote inaruhusu kuvaa vyovyote tu bila kuficha sehmu za Uchi au wanaacha maungo yao ya siri yaonekane hapo hakuna Mungu hata kama Tamaduni hiyo imekubaliwa na Taifa zima.

Sehemu za uchi si tu sehemu za siri tunazozijua bali ni sehemu zote zinazoonyesha maungo yetu mapaja, makwapa yetu ,matiti, tumbo na vitovu, mgongo wote n.k.Kama  wakristo hatunabudi kuzingatia Kanuni hii aliyoiweka Mungu bila kujali tupo kwenye tamaduni gani lazima  Mavazi yetu yafiche Uchi yaani yafiche sehemu za siri,yafiche matumbo, matiti na migogo ,makwapa n.k.Tukivaa kinyume na hapo tunamkosea Mungu aliyeanzisha mavazi

Ishu hapa umeficha uchi wako sio kwamba mbona sisi hatuvai ngozi! Ngozi lilikuwani vazi la nyakati hizo kabla ya kabla ya mengine kuwapo


Kumbuka Mungu anatufundisha Kuwa mavazi yanaweza kukutambulisha kuwa wewe ni kahaba *Mithali 7:10* au unaweza kutambulisha  wewe ni Msiri kumbe ni mwebrania kama ilivyotokea kwa Musa.Ingawa maandiko yanatufundisha kutokuenenda kama mataifa yaenendavyo


*2⃣MAUMBILE YANAPASWA KUTUFUNDISHA KUJUA KIPI NI CHA KUVAA WANAUME NA KIPI NI CHA KIKE?*

Jambo la Pili Msingi Wa muhumu aliouweka Mungu kwenye Neno lake ni *MAUMBILE KUTUFUNDISHA  1WAKORINTO 11:14* inasema

_"Je Maumbile yenyewe hayawafundishi kuwa Mwanamke akiwa na  ............."_

Katika hili Maumbile tu yanatufundisha kujua kuwa Suriali ji Vazi la Kiume kwa namna ambavyo lipo na limeshonwa ili kumrahisishia  Mwanaume hata namna anavyoweza kujisitiri kwa haraka anapolivaa.Ila kwa mwanamke hata alishone kwa namna wanayoita ni Suruali za Kike, ni lazima atapata shida sana katika kuweza kujisitiri katika hali ya dharura ikitokea maana ni lazima iwe hata ni shida kuivua au kuivaa.

Na zaidi sana kwa maumbile yake hawezi kuvaa suluali ambayo haitachora mwili wake na maumbile yake.Na hata utaweza kuona zile sehemu za mbele pale ikichora umbo la vii( V) ambapo ni matusi makubwa sana


*3⃣SURUALI NI VAZI LA KIUME TANGU AGANO LA KALE MPAKA SASA*

Tangu agano la kale hii sheria ya *Kumbukumbu 22:5* inatolewa ilikuwa inajulikana  na imezoeleka kuwa suruali ni vazi  lililovaliwa na wanaume si wanawake.Tunaona mifano kwenye maandiko mengi sana wakivaa makuhani na hata watu wakaida ambao wote ni wanaume hivyo hakukuwa na mwanamke aliyevaa suruali

                            *♨{KUTOKA 28:42}*

_Nawe wafanyie *suruali za nguo ya kitani,* ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;_

                      *♨{DANIEL 3:21}*

_Basi watu hao wakafungwa, hali *wamevaa suruali zao,* na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto._

Maandiko ya wazi yanayoonyesha Suruali kuvaliwa na wanaume yapo mengi katika Biblia, siwezi kuyaweka yote ila nenda kasome mwenyewe *KUTOKA 39:28,WAAMUZI 6:10, 16:4 EZEKIEL 44:18,DANIEL 3:27*

Hivyo napata tabu ninapoona watu wanatetea na kupingana na maneno ya wazi kama haya yanayoonyesha kuwa kumbe Suriali zilivaliwa na wanaume tangu awali.Sasa mijadala ni ya nini? Afadhali ingekuwa labda hilo halijawekwa wazi ndio tungeendelea kutumia au kuangalia Misingi mingine ya kujua Mavazi gani tunayopaswa kuvaa kwa vizazi vyote

Misingi ipo mingi ya kuizingatia ila kwa leo naishia kuitaja hiyo mitatu(3) itoshe kuonyesha kuwa Kumbe tangu zamani hata sasa  Mungu anataka tuvae *mavazi ya kuzisitiri*

                           ♨ *{1 Timothy 2:9}*
_"Vivyo hivyo wanawake na *wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri*, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, ..............."_

Vazi la Suruali kwa Wanawake halimsitili bali linatia aibu na zaidi ndilo linalera mitego na kuwakosesha watu wengi sana ndani na  nje ya kanisa isipokuwa hao wanaopenda kuwaona mkiwa mnaonyesha maungo yenu


*šŸ“›WANADAI TUVAE KWA TAMADUNI ZETU‼JE KILA TAMADUNI INA MUNGU❓*

Nimalizie na hoja ya mwisho ha wa watu ambayo ukiiangalia kwa juu juu ni kama ina ukweli fulani kumbe ni Uongo wa Kuzimu kamili. Utawasikia wanasema tuvae kukungana na tamaduni zetu zilivyo maana tamaduni zinatofautiana mahali kwa mahali. Hivyo utawasikia wanakwambia Mbona scotland wanaume ndio wanavaa sketi na wanawake suruali!!wanatumia hoja kama hiyo kutaka kuhalalisha kuwa  tamaduni za mahali mahali ndizo zinaweza kutujulisha hapa hili liwe baya ila kule sio baya.Wanawafundisha watu kuwa tuhubiri kulingana na mazingira na tamaduni za watu zilivyo.

Hapa jambo la Msingi la Kufahamu kuwa ni kweli kila mahali kunaweza kuwa na tamaduni tofauti tofauti ambazo nyingi nzuri tu wala si za Mungu wala si za shetani bali ni ambazo tumekubaliana kuziishi na hatufanyi tumkosee Mungu tukizifanya

Mfano tu, Kwa tamaduni zetu wakristo wengi hawajazoea kuvaa kanzu na kuingia nazo kanisani, lakini si kwamba ni mbaya tukivaa au tusipovaa! Hapo tunaweza tusivae na tusiwe na hatia au kwamba ni dhambi!!

Lakini kuna tamaduni nyingi zilizopo ulimwenguni ni za kishetani kabisa na zinaweza kuwa zinakubaliwa na Taifa zima au ulimwengu mzima mzima na hata zikafanyika kizazi baada ya kizazi hata ikaonekana ni kawaida ya Ukimwengu mzima au kawaida ya Taifa hilo kwa vizazi. Lakini haimaanishi kuwa kila kawaida hizo za Taifa au za ulimwengu ni sawa mbele za Mungu

Ni Muhimu kufahamu sisi kama wakristo,tunaowaza kwenda mbinguni, Kawaida yetu ni Neno la Mungu au Tamaduni yetu inapaswa isitufanye tutoke nje ya Neno la Mungu

Sasa tuone maandiko yanasema nini juu ya hizi tamaduni za mahali mahali au juu ya hizi kawaida za Taifa  inasema nini

*♨{2 WAFALME 17:26,33}*
_Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu *hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi*.Wakamcha BWANA, na kuitumikia miungu yao wenyewe, sawasawa na *kawaida za mataifa* ambao wao walihamishwa kutoka kwao._


Umeona inaeleza kuna kawaida za Mungu na kawaida za ulimwengu au kawaida za mataifa *Waefeso 2:2*

Kwahiyo ni Muhimu kujua Upo uwezekano Taifa zima zima au  hata vizazi vinaweza kupita vingi vikahalalisha kawaida fulani fulani na kufanya ndio sehemu ya utamaduni wao lakini kumbe ni kinyume na Kawaida ya Mungu ambayo tunaijua kwa kuangalia Misingi ya Mungu

Hivyo tusijifiche kwa mgongo wa utamaduni fulani wa watu fulani mbona wao kwao wanafanya hivi au vile na haina shida.Hatuongozwi na Tamaduni bali Neno la Mungu.Kanisa la Mungu linatakiwa liwe Uniform lenye maadili yote ya kibiblia si ya kitamaduni za watu

Ni Muhimu kujua wazungu sio kielelezo chetu kuwa mbona tamaduni zao kwao haina shida wanawake au wahubiri kuvaa suruali na wanahubiri tu. Kama tunataka kuiga tamaduni mbona msemi nchi nyingi za hao mnaowaiga wazungu au wamerekani  wao wanaruhusu ushoga na ni haki kabisa ya raia wao na ni Kawaida tu kaao kufanya hivyo!! Mbona na ninyi msiseme kwakuwa Ushoga ni halali  kwasababu ni utamaduni wao basi na sisi tuige tuwe kama wao?

Acheni kuleta mafundisho haya ya kigeni ya kutoka kuzimu na kutaka kuwafanya wadada zetu wawe makahaba na kufanya kanisa kuwa kama danguro la makahaba! Kwanini mnawafariji kama na ninyi si makahaba? Mnataka wawe uchi au waonyeshe maungo yao ili iweje? Mfanye nao uzinzi?Haya mafunisho yanayozagazwa nyakatinza leo ni Mafundisho ya kuzimu kamili yanalengo la kukufanya dada yangu unampenda Mungu uende kuzimu.

Ikiwa wewe ni mdada na umeokoka na unataka kwenda Mbinguni, nakwambia kwa upole choma moto suruali zako zote, usiwasikilize hawa wachungaji na waalimu wanaokupoteza ,wanatafuta uwe mshirika wao na uwape pesa usiondoke ndio maana hawakuelezi kweli hii.Mimi nakueleza kweli natafuta roho yako iponywe wala Usije ninakosali bali ifahamu kweli hii

*♨KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI*
                *šŸ”µNa: Shujaa Charles Richard Mwaisemba*
                    *0712-054498/ 0759-420202*
                          _stmwaisembac@gmail.com_

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

šŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA šŸ›*