IBADA INAUHUSIANO UPI NA UCHUMI WA MTU

[8/18, 17:16

 Mwl.Peter Francis Masanja:



IBADA INAUHUSIANO UPI NA UCHUMI WA MTU ❓


💒💒💒💒💒💒💒💒


😊😊 IBADA INAJUMUISHA


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Mungu

Madhabahu


Watu


Uimbaji


Maombi



Sadaka




📖📖📖📖📖📖📖📖

👉🏻 Katika eneo la sadaka Wakristo leo hatutoi 😊😊😊😊


👉🏻 Wengi saana tunakurupuka kutoa sadaka 😊😊😊😊


👉🏻 Tunakurupuka kwa sababu hatuziombei sisi binafsi


👉🏻 Hatusemi na Mungu kabla ya kutoka nyumbani mwetu Mungu atutendee nini kupitia hizo sadaka


👉🏻 Unaweza ukazua maswali

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


Mbona namtolea sana Mungu lakini sifanikiwi ❓


Ni kwasababu utaratibu wako wa utoaji haueleweki

Humwambii Mungu mambo yako


👉🏻 Yaani Kabla ya kutoka nyumbani ijue sadaka yako kisha ishike inua mikono juu huku umeishikilia mwambie

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


Mungu kupitia sadaka hii, ninayoenda kuitoa madhabahuni kwako

Naomba unitendee

✍✍✍✍✍✍✍✍

Taja mambo ambayo wataka atende kwako
Hapo utakutana na baraka zake .


👉🏻 Epuka kwenda kuanza kuchambua sadaka mfukoni ukiwa ibadani , ndio useme sijui nitoe hii

Aaaah ngoja nitoe jero hapo Mungu hawezi kusema na wewe kupitia sadaka yako


👉🏻 Sadaka usiichukulie kama desturi ya kanisa

Sadaka ni jambo la kupanga ukiwa nyumbani kwako kabisa na uiombee mwenyewe kabla ya kuipeleka madhabahuni maana kuhani hawezi kujua nini wahitaji Mungu akutendee .💒


✍ Ukiinyamazia sadaka utakuwa kama unamuita mungu baali ambaye hakuonekana .😨😨😨😨😨


✍ Mungu anakuangalia anakuona anabaki anajiuliza nitambariki vipi huyu hahitaji 😨😨😨 🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂🏃🏻‍♂


✍ Mungu alipokuumba alikuweka umwabudu lakini anasema ukinyamaza hawezi kutenda anabaki anakuangalia tu 😨😨😨


📖 *19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.*


Wafilipi 4:19


✍ Umetoa sadaka wala hukusema unachohitaji hapo Mungu atabaki kimya anasubiri useme ndyo atende .

📖 8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;


2 Wakorintho 9:8

9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.


2 Wakorintho 9:9


✍ Bado tena anasema akikutoa kwenye umaskini utende mema 😊😊😊😊usiwe mbahili


📖 *4 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia kweli katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)*

Kumbukumbu la Torati 15:4


✍ Ahadi zote za Mungu zimebebwa na ndani ya ibada inayoambatana na sadaka na maombi

Usitoe sadaka bila wewe mtoaji kumweleza Mungu mambo yako .

✍ Ahadi zake ni za milele kabisa

✍ Mungu akiona unazidi kumpendeza saana huwa anafurahi sana

Anapenda umsifu na umtegemee saana


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,


Ufunuo wa Yohana 5:11

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.


Ufunuo wa Yohana 5:12

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.


Ufunuo wa Yohana 5:13

14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.


Ufunuo wa Yohana 5:14


✍ Makerubi na Maserafi wanamsifu na wewe pia msifu 🎤🛐💒


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻



📖 23 Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.


Zaburi 22:23


✍ Angalia matokea mazuri ya kumsifu na kumtolea jinsi anavyokubariki katika ardhi uikaayo .

Kila kitu atakiweka chini ya miguu yako .

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 6 *Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake* .

Zaburi 8:6

7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;

Zaburi 8:7

8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.

Zaburi 8:8

9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Zaburi 8:9


✍ Ahadi zake zipo wazi kabisa ukimpenda na kuzishika amri zake


Angalia hapa


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻



📖 6 Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha.


Kumbukumbu la Torati 8:6

7 Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima;

Kumbukumbu la Torati 8:7

8 nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;


Kumbukumbu la Torati 8:8

9 nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba.

Kumbukumbu la Torati 8:9

10 Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa.

Kumbukumbu la Torati 8:10

✍ Chunga sana usije ukajiinua ukamsahau Mungu baada ya

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Kukaa kwenye nyumba nzuri

Kununua gari

Kusomesha wanao English Medium

Kufuga ng'ombe wa maziwa na kuku

Kufungua biashara yako nzuri


🍇 Angalia hapa anakupa tahadhari sana na anakuambia kwamba utajiri wako umetokana na ibada yaani kumsifu na kumtolea Mungu sadaka ya maana huku ukiishi katika utakatifu .



👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 11 Jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.


Kumbukumbu la Torati 8:11

12 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;


Kumbukumbu la Torati 8:12

13 na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;


Kumbukumbu la Torati 8:13

14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;

Kumbukumbu la Torati 8:14

15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,


Kumbukumbu la Torati 8:15

16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.

Kumbukumbu la Torati 8:16

17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.

Kumbukumbu la Torati 8:17

18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Kumbukumbu la Torati 8:18



 ✍ Nimeongea mengi sana kuhusu uhusiano kati ya ibada na uchumi wa mtu lakini mwisho nakupa mhutasari huu

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻



🍇 Utajiri wa mtu umebebwa na ibada.


🍇 Ndani ya ibada kuna sadaka na maombi .


🍇 Baada ya maombi Mungu anaachilia baraka juu ya ardhi aikaayo mtu ili imzalie matunda katika kila kazi aifanyayo .



🍇 Baraka za Mungu ni za milele hazizuiliki kabisa akiamuru baraka kwako hakuna wa kusimama kinyume chake ( 2 Nyak .20:6 )

🍇 Mwangalie Ayubu alivyokuja kuzidishiwa mali

🔥 Baraka zitokanazo na ibada za mashetani zinazuilika na zinakoma na mwisho wake ni aibu ya milele .


✍ Unapita katika majaribu ,yaani maisha ya taabu mtukuze Mungu .

Kumbuka Mungu hajakuacha , mwone nabii Eliya alilishwa na kunguru

Unafikiri hataleta watu wa kukusaidia ❓

Kama ni mwanachuo usidhubutu kuacha mwili wako uchafuliwe mwombe Mungu sana akupe msaada .

Kumbuka wengine tulipokuwa chuo tulikuwa tunakula shilingi 1000 kwa siku tena nasubiria chakula cha mchana hadi kesho tena mchana 🤭🤭🤭🤭

Shujaa wa imani lazima apitie magumu na ni marufuku kutenda dhambi


 Mungu akubariki sana 🛐🛐🛐🛐💒💒💒


Bwana akubariki katika kila ulifanyalo ufanikiwe katika jina la Yesu .

Amen

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*