KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO


          KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO 

SIKU YA PILI
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Wagalatia 5:1
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Wagalatia 6:8
🍇 Roho Mtakatifu hutupa uwezo wa kuishinda dhambi .
Anampa mtu uwezo wa kuitawala dhambi .
Maisha ya mtu yakikaa katika uongozi wa Roho Mtakatifu , mtu huyo atakuwa kielelezo mbele za Mungu na wanadamu .
Mruhusu Roho Mtakatifu atawale maisha yako utaona mambo yako yanaenda vizuri sana
Roho Mtakatifu anamfanya mtu achukie dhambi , aondoe hali ya ukawaida .
Kila aliye na uongozi wa Roho Mtakatifu anaushuhuda mzuri katika maisha yake .
Kila aongozwaye na Roho Mtakatifu ni jasiri au ni shujaa wa imani
Anamamlaka ya kuonya , kukaripia na kukemea bila woga .
  Hii ni kwasababu Roho Mtakatifu humtia nguvu na mamlaka ya kumkemea shetani na kazi zake zote .
  Utauliza kwanini sasa baadhi ya wakristo wameangukia kwenye maisha ya dhambi , ina maana hawaongozwi na Roho Mtakatifu
💉 Jibu ni kwamba hawakuomba uongozi wake na kuamua kuuruhusu mwili uwaongoze .
Hii imewafanya vijana wengi kuanguka katika zinaa na matokea yake ni uangamivu .
  Hakikisha unawekeza maisha yako kwa Roho Mtakatifu ili umpendeze Mungu
Huwezi kuishinda dhambi kwa mwili , utaanguka tu .
Cha kufanya tafta uongozi wa Roho Mtakatifu .
Roho Mtakatifu anakupa tahadhari juu ya uovu .Kuna wakati watu wanaoongozwa na Roho Mtakatifu wakikosea wanaingia hukumuni mioyoni mwao na kujutia kwanini wamefanya hivyo Roho Mtakatifu anakufundisha njia ikupasayo kuifuata ili uwe salama .
Kunena kwako , kuwajibu watu kuwe kuzuri ,
Kinywa chako kinene maneno ya hekima .
Ili uwe na hekima na busara lazima utafte uongozi wa Roho Mtakatifu .
📖 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Wakolosai 4:6
Huwezi kuwa na hekima ya kiMungu kama huna uongozi wa Roho Mtakatifu.
Utajikuta unawajibu watu vibaya .
Kumbuka tunazungumzia umuhimu wa Roho Mtakatifu katika kuishinda dhambi .
  Roho Mtakatifu anakupa uwezo wa kujitambua thamani yako mbele za Mungu .
Kwa sababu yeye ni Mtakatifu basi na wewe inabidi ujitambue kuwa wewe ni mali yake .Kwahiyo anakwambia usiuchafue mwili wako .
📖 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
1 Wakorintho 6:19
Roho Mtakatifu anakupa uwezo wa kujitambua wewe ni nani na unapaswa kufanya nini ili usimkose Mungu ❓
Kujitambua hapa ni kujua kuwa mwili ulionao ni hekalu la Roho Mtakatifu na hupaswi kuuchafua .
Baada ya kutambua hilo uishi sawasawa na neno la Mungu na kulitendea kazi .
Anakupa akili ya kupima kila jambo ufanyalo , je linamletea Mungu utukufu ❓
Kwahiyo ni yeye anakuletea ufahamu wa kuyapima kila uyafanyayo kama yanamtukuza Mungu . Huwezi kumwomba Mungu ukisema 🛐🛐
Ee Mungu nakuomba nikanywe pombe au nikazini na mke wa mtu uniongoze kwa Roho wako Mtakatifu 😨😨😨😨
Ukiona jambo lolote huwezi kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu ujue ni dhambi achana nalo .
  Leo kaa jitafakari kwa makini sana kama ifuatavyo :
Kama unaishi maisha ya zinaa ,unazini na wake za watu , unazini na kila kijana , unanunua pombe , unatukana , unajisaga ,unapiga punyeto , unakaa barazani kupiga umbea , je una Roho Mtakatifu ❓
Jibu ni kwamba umekufa kiroho ni marehemu anayetembea .
Roho Mtakatifu amekukimbia unaishi kimwili na siyo kiroho tena .
Kama unaishi kwa kuheshimu watu wa kila rika na wengi wanatamani waige maisha yako na tabia zako njema tambua wewe unaongozwa na Roho Mtakatifu.
Matendo yako yamfanye Roho Mtakatifu afanye makao ndani yako .
Ukiishi maisha ya kutenda machukizo Roho Mtakatifu hukimbia kabisa maana wewe siyo mtu tena bali ni mwanadamu mwenye tabia za mnyama .
Kama vile mnyama asivyo na Roho Mtakatifu vivyo hivyo na mtu akibeba uanadamu hufanya mambo kama mnyama .
Mtu anatabia za Rohoni bali mwanadamu anatabia za mwilini ndiyo maana ni kawaida sana mtu akigeuka kuwa mwanadamu kanisani utamwona anajiingiza kuchafua kanisa.
📖 14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
1 Wakorintho 2:14
15 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
1 Wakorintho 2:15
  Jifikirie , je unauongozi wa Roho Mtakatifu ❓
💉 Kama unang'ang'ania umjue mchumba wako kabla ya ndoa je huko ni kuongozwa na Roho Mtakatifu au mwili ❓
Na kama ni mwili basi ni dhambi kwako wewe .
Heshimu sana mambo matamu kimwili lakini madhara yake kiroho ni makubwa sana .Wanaofanya zinaa husema ni tamu sana ni raha lakini wakiugua magonjwa wanakuwa washauri wazuri sana kwetu maana walipanda kwa mwili wamevuma mauti .
Asikudanganye mtu eti utumike , utauziwa mbuzi kwenye gunia hutafanya vizuri ndani ya ndoa , jitenge na waovu .
Mpendeze Mungu .
  Mheshimu Roho Mtakatifu akaaye ndani yako asije akakukimbia ukafa kiroho na kimwili pia . Panda kwa roho uvune mema .
🍇 Mungu akubariki sana
Nakutakia siku njema yenye baraka
Naitwa : Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
📖 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
1 Wathesalonike 4:4
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
1 Wathesalonike 4:5


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*