KUPOKEA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU πŸ–*

*πŸ’’ KUPOKEA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU πŸ–*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



πŸ“– 8 *Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu* ; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.


Matendo ya Mitume 1:8



✍ Kila aliyempikea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake anahitaji nguvu ya Roho Mtakatufu ili aishi maisha ya ushindi katika dunia hii .


✍ Ili mtu amshuhudie Kristo anahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili aishangaze dunia wanadamu wabaki wanashangaa 😨😨

Nakujiuliza maswali kwanini huyu mtu anaishi kwa amani sana na watu 🧠

Amewezaje kuvumilia yote haya 🧠


✍ Yesu alipokuwa nyikani siku arobaini amefunga alipokutana na shetani akajibizana naye kwa ujasiri sana kwasababu ya alipokea nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yake .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,

Luka 4:1

2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.

Luka 4:2



✍ Tunamwona alitiwa nguvu ya Roho Mtakatifu yaani nguvu ya kukabuliana na kila hila za adui shetani .



✍ Ile nguvu ya Roho Mtakatifu ilimfanya asiingie kwenye mitego ya ibilisi .

✍ Tukisoma tunaona alipokuwa nyikani aliona njaa hiyo njaa ilikuwa ni kipimo cha imani yaani ni jaribu lingine ambalo lilichukua nafasi kwa  mtu wa kawaida kama shida au tatizo ambalo linahitaji litatuliwe .

Na mtatuaji ambaye alijitokeza hapo mbele ni shetani lakini kwa masharti .Kwamba amsujudie yeye ampe fahari yote ya dunia .❌❌


✍ Hii inawakilisha kwamba mtu wa Mungu asipokuwa na nguvu ya Roho Mtakatifu anaweza kuingia kwenye tamaa za dunia ambazo zinaweza kumpeleka jehanamu .



✍ Mtu asipokuwa na nguvu ya Roho Mtakatifu ni rahisi sana kumwasi Mungu kwa kutaka mafanikio ya haraka ya kimwili kama vile majumba ya kifahari , magari , biashara kubwa , ndoa ya haraka yaani kuharakia kuoa kwa tamaa za mwili na kujikuta amekosea mwenzi wa ndoa .

✍ Ni rahisi kwa binti asiye na nguvu ya Roho Mtakatifu kuuza mwili wake ili apate hela ya kusuka nywele au kushiriki ngono na boss ili apate nafasi ya ajira .



✍ Nguvu ya Roho Mtakatifu inatupa ujasiri wa kumpinga shetani kwa kukataa vitu vyote vizuri vinavyoweza kutupeleka jehanamu .



✍ Yesu hakukubali kumsujudia shetani aliiona thamani ya maisha yake ya milele hakuiangalia thamani ya vitu vya duniani ambavyo ukifa hutazikwa navyo



✍ Mtu wa Mungu anapoipokea nguvu ya Roho Mtakatifu inamfanya kuwa shahidi wa Yesu Kristo duniani kote.

✍ Sifa ya shahidi wa Yesu Kristo ni kukataa dhambi na kuitetea imani ya Yesu Kristo .

✍ Nguvu ya Roho Mtakatifu inakufanya uwe shujaa wa imani πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻



✍ Je , unataka maombi yako yawe na matokeo mazuri ❓


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


✍ Omba Mungu akupe nguvu ya Roho Mtakatifu yaani upako au mafuta ( Spiritual power / Spiritual Jurisdiction / Spiritual authority )


✍ Nguvu ya Roho Mtakatifu ikiwa ndani yako unauwezo mkubwa wa kuwatangazia watu waliofungwa na ibilisi kufunguliwa kwao , kuwaweka huru waliotiwa kwenye magereza ya ibilisi .Kila aliyeonewa na ibilisi atakuwa huru .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 38 habari za Yesu wa Nazareti, *jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu* naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.


Matendo ya Mitume 10:38



✍ Ili uishangaze dunia unahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ndipo Mungu atakutumia kuangusha falme za giza na kuangamiza majeshi yote ya shetani.


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;

Yeremia 51:20

21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

Yeremia 51:21

22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;

Yeremia 51:22

23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.

Yeremia 51:23



✍ Mtu wa Mungu akiwa na nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yake anaogopwa sana na wakuu wa giza na maombi yake yanasafiri haraka sana na yanavuruga mipango ya shetani mingi sana .


✍ Nakumbuka siku moja nilikuwa Shinyanga nikiwa katika kuomba maana eneo hilo kulikuwa na uganga mwingi sana .Niliona watu wananiogopa hata kukaa nao kuongea , wengine waliiba picha zangu walizirudisha wenyewe nikakuta wamezitupia dirishani  πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯


✍ Vita vyetu ni vya kiroho .



✍ Neno la Mungu linasema


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.


Mathayo 11:12



✍ Unahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili uuteke ufalme wa Mungu .

✍ Nguvu ya Roho Mtakatifu inakupa .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ‡imani ( kupokea , maana tunaishi kwa imani na tunapokea kwa imani ).

πŸ‡ Ushindi ( tunapata ushindi ndani yetu tunakuwa mashujaa wa imani huku tukimtetea Yesu bila woga πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻



πŸ‡ Neno , hii ni silaha ya kiroho ambayo inahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili uweze kuiachilia kila mahali kumwaibisha shetani .Hapa ndiyo utaona Yesu alipokuwa akihojiana na shetani alikuwa anamjibu

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

Imeandikwa.......



✍ Neno linamnyima shetani uhalali wa kummiliki mtu linamfanya akose pa kudanganyia kabisa



Mungu akubariki sana

Leo nitaishia hapa ,

Karibu tena katika uchambuzi wa kazi za Roho Mtakatifu ndani yako .

Umekuwa nami

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

Mwl.Peter Francis Masanja

What's app group app

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Visit for daily lessons



God bless you with all Spiritual blessings and live a triumphant life .



πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*