MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU ROHO MTAKATIFU


MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU ROHO MTAKATIFU

                      ROHO MTAKATIFU NI NANI?
Ø  ni mwalimu ,msaidizi , kiongozi wetu anayetuongoza kwenye kweli yote
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Yohana 14 :16
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 14 :17
Ø  Roho mtakatifu ni Nguvu inayotuwezesha kuwa mashahidi wa nini

·         Utilifu wa ahadi za Bwana
·         Udhihirisho wa nguvu za Mungu
·         Kweli ya Mungu yerusalemu samaria na hata mwisho wa nchi
Roho mtakatifu ni msaidizi wetu aliyetumwa kutusaidia kukamilisha kazi ya kujenga ufalme wa Mungu hapa Duniani
Ndiye pekee aliyepewa uwezo wa kutusaidia kutimiza mapenzi ya Mungu
·         Madhehebu
·         Makabila
·         Utajiri na umasikini
·         Rangi nk
Haya ni mapambo na majengo yakujihifadhia tu
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Matendo ya Mitume 1 :8
Baada ya huo utangulizi sasa tuingie katika somo letu la leo
Natambua masomo ya walimu wenzangu waliotangulia

Nami kwa unyenyekevu naomba nieleze kidogo tu

MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU ROHO MTAKATIFU
1.Anauwezo wa kufunua mbingu na kukupa uwezo wa kuona ndani yake
Mdo 7:55
2.Roho mt anapatikana kwa njia kuu mbili
A. Mara baada ya kubatizwa yaani unapotoka katika maji mengi
Luka  3:21,22
B.Kwa kuwekewa mikono na watumishi ambao wamejazwa Roho mtakatifu
Mdo 19:2,Mdo 8:17
3. Ndiye shahidi mwaminifu ambaye akikueleza jambo ujue ni hakika na amina.
Shahidi huyu anaaminika kuliko hata malaika na wakuu wa dini
Mdo 11:12
Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu.
Matendo ya Mitume 7 :55
4. Mara nyingi huwa sambamba na neno la Mungu ndio maana Neno linapohubiriwa huambatana na miujiza.
Siri hii ndiyo inaitofautisha Biblia na vitabu vingine
5.Anaweza kuamua kuanza kubatiza watu mwenyewe kabla ya ubatizo wa maji  .
Jambo hili alilitenda kwa kornelio hiyo mdo 11:15
21 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
Luka 3 :21
22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Luka 3 :22
2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Matendo ya Mitume 19 :2
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 8 :17

12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
Matendo ya Mitume 11 :12
15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.
Matendo ya Mitume 11 :15
6.Roho mtakatifu ndiye siri ya uwezo waliokuwa nao akina Musa, Eliya, Elisha ,na manabii wote wa kweli waliopo sasa.
Unataka kutenda kama wao kaa vizuri na Roho mtakatifu
27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia.
Matendo ya Mitume 11 :27
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Petro 1 :21

7.Roho mtakatifu anamipango yake tena ya kipekee na hapendi kuingiliwa na mtu .
Unataka kufanya maajabu na kwa ukamilifu na kuwa na utumishi uliotukuka msikilize na kumtii
Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
Matendo ya Mitume 13 :2
3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
Matendo ya Mitume 13 :3
4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Matendo ya Mitume 13 :4
8.Ndiye anayetusaidia kujua kipi halali na kipi usifanye wakati gani

Mdo 9:1
1kor 12:3
Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
Matendo ya Mitume 16 :6
Anaweza kumchagua yeyote bila kujali umri wake katika huduma rangi wala kabila
Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
Matendo ya Mitume 9 :1
..Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
1 Wakorintho 12 :3
Watu wa Mungu hugombana na Mungu hapa wanadhani kisa ni haki yao basi ni halali kuchukua kusema na hata kutenda
1 Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu,
Warumi 9 :1
πŸ”ŸMmiliki wa kanisa ni Roho mtakatifu hawa maaskofu wachungaji nk ni waajiliwa shambani .
Ni sawa na vinyozi, watu wa saluni , shoe shiner , mafundi cherehani wa mwili wa Kristo
Mdo 20: 28
Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
Matendo ya Mitume 19 :1
2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Matendo ya Mitume 19 :2
3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
Matendo ya Mitume 19 :3
28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Matendo ya Mitume 20 :28
1. Roho mtakatifu anatudhihirishia kuwa sisi ni sehemu ya ufalme .
Kupitia
🀝🏾amani moyoni
🀝🏾kuwa naHaki mbele za Mungu
🀝🏾Furaha isiyotegemea vinavyoonekana
Rumi 14:17
Rumi 15:13
2. Roho mtakatifu husababisha sadaka zetu kupata kibali kwa
Kuzitakasa
kukuelekeza kiasi na kitu cha kutoa
Sehemu ya kupeleka
lini na kwa nani

: πŸ“– 16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
Warumi 15:16
3.Roho mtakatifu pekee ndiye awezaye kufanya miujiza na ishara za kweli na za kudumu .
Haya tunayoyaona  mengi ni maigizo mazingaombww na uganga
Mdo 15:19
 4. Roho mtakatifu ndiye anayetuwezesha kuwa
πŸ™πŸΏ. Safi
πŸ™πŸΏ.na Elimu
πŸ™πŸΏ.Wavumilivu
πŸ™πŸΏ.Watu wema
πŸ™πŸΏ.na Upendo usio na unafiki

2korintho 6:6
5. Roho mtakatifu akiwa anahuzunika kila mara ndani yako hiyo ni dalili kuwa anataka kukuacha

Waefeso 4:30
Maana ukileta unafiki wako atatujulisha tu
Ukijichafua atatujjlisha
Ndio maana hatuna haja ya sheria maana Roho wa Mungu mwenyewe atakushughulikia bila huruma
6. Huwezi kuwa mpya na kuachana na tabia zako za kale kisa eti unasali kanisa la kilokole la ghorofa au la.
Tunafanywa kwa kumpokea Roho mtakatifu
Tito 3:5
HITIMISHO
Amini ufanyike kuwa mwanafunzi .
 Batizwa ubatizo wa Yesu ili ukitoka kwenye maji ujazwe na Roho mtakatifu.
Kubali kuwekewa mikono na watumishi waliojazwa Roho mtakatifu.
 Unataka kuwa mcha Mungu kubali kuwa Hekalu la Roho mtakatifu
1 korintho 6:19
 Pastor Sponga:
MUNGU AWABARIKI SANA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*