NGUVU YA VIJANA KATIKA UKUAJI WA KANISA πŸ’’*

*πŸ’’ NGUVU YA VIJANA KATIKA UKUAJI WA KANISA πŸ’’*


Somo la Kwanza



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


 *UTANGULIZI*


πŸ“– ..... Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

1 Yohana 2:14b



Bwana Yesu asifiwe


πŸ’’ Ni matumaini yangu kuwa kila kijana aliyempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake atapata kujifunza kupitia mfululizo wa somo hili .


πŸ‡ Kijana anamchango mkubwa sana katika kanisa katika kuhakikisha kanisa linakua kiroho na kiuchumi pia .


πŸ’’ Kijana ni raslimali muhimu sana katika kanisa ambayo inatakiwa itumiwe vizuri ili kuhakikisha kanisa linapata maendeleo .


πŸ’’ Ili kanisa likue na liwe la kuvutia linahitaji vijana ambao wamejitoa kwaajili ya kazi ya Mungu ( self commitment )


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»



πŸ“– 1 *_Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.*

Mhubiri 12:1



πŸ‡ Kila kijana anapaswa ajitoe katika kazi ya Mungu ( amtumikie) na kukubali kujifunza ili awe kijana mwenye nguvu na shujaa katika imani .

πŸ’’ Kanisa linahitaji vijana ambao watu wakiwaona waone sura ya Mungu ( reflection of God / image of God).


πŸ’’ Kanisa linahitaji vijana ambao mienendo yao na usemi wao  inawatambulisha kuwa wameokoka yaani wanamjua Mungu .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– *Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha* .


Mathayo 26:73


✍Petro alitambulika kwa usemi na matendo yake kuwa ni mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu .Usemi wako ni barua juu ya mataifa kuwa umembeba Yesu ndani yako .


πŸ’’ Mafanikio ya vijana kiroho na kiuchumi yanaendana na kufanikiwa kwa kanisa .


πŸ“– 7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

Yoshua 1:7

8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1:8



πŸ’’kijana akikaa vizuri ndani ya Yesu atafanikiwa sana na katika kufanikiwa kwake kanisa pia litafanikiwa.



Mungu akubariki sana karibu sehemu ya pili



πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*