NIMECHOKA NA MAISHA HAYA 😨*

[8/26, 15:53]

201 8
*πŸ”° NIMECHOKA NA MAISHA HAYA 😨*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


Presenting from

πŸ’’SAUTI YA MUNGU MINISTRY ( whats app group ) πŸ›

Daily lessons

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry



πŸ”° Kila mtu hupitia katika aina ya maisha fulani na kujikatia tamaa kabisa na kujiona ameachwa na Mungu.


✍ Lakini leo nakuomba sana twende tujifunze hili somo likutie moyo usije ukakatisha safari ya maisha yako na kupoteza welekeo .


✍ Mtu wa Mungu unapopitia katika majaribu mbalimbali tambua kuwa siyo wewe tu unayepitia bali kunawengine wanaweza hata kuyatamani maisha yako .Lakini wakikufunulia siri zao unaweza ukatoa machozi .


✍ Kunawakati waweza kufukiria kwamba unaishi maisha magumu kumbe wapo wanaishi magumu zaidi yako .



✍ Kuna wakati unaweza kusema unaumwa lakini ukipelekwa ICU kuwaangalia wanaoumwa utasema huumwi .


✍ Palipo na ugumu wa maisha kuna fursa kwa Mungu yaani fursa kwako kukupandisha kiimani na kukuweka viwango vya juu sana .


✍ Hauhitaji kulalamika , maana maandiko yanasema


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– *13 _Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili._*


1 Wakorintho 10:13


✍ Magumu upitiayo hayakupati wewe tu , tambua wapo na wengine wanapitia majaribu .


✍ Mungu hawezi kukuacha kamwe ipo siku ,atakuinua na kukuweka juu sana .

✍ Amekuandalia njia ya kutokea kwenye hilo jaribu .
✍ Wakati unapitia kwenye majaribu acha kusema umechoka kuishi au umechoka na maisha hayo .


✍ Mshukuru Mungu amini ipo siku ya kuinuliwa .


✍ Usinung'unike kwasababu ya shida upitiazo .


✍Kila jaribu linamlango wa kutokea .

✍ Kila jaribu ni ushuhuda kwa wengine kujifunza kwako .


✍ Lengo la jaribu ni kuudhihirisha ukuu na uweza  wa Mungu .


✍ Upitapo katika jaribu usiseme umechoka na maisha hayo maana Mungu anakupima hapo aone kama utakuwa mwaminifu kwake .


✍ Jaribu ni kipimo cha uaminifu kwa Mungu na wanadamu pia .


✍ Jaribu ni kipimo cha Saburi yaani subira au uvumilivu ( uwezo wa kuvumilia shida ).


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– *3 _mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi._*


Yakobo 1:3



✍ Mungu anaupima uaminifu wako kupitia jaribu ili aweze kukupandisha viwango vya juu sana .

✍ Ayubu alijarubiwa kwa lengo la kuona uaminifu kwa Mungu.


✍ Ayubu alivumilia shida alijua ipo siku ya kuinuliwa kwake .Ayubu alisimama imara japo mkewe uvumilivu ulimshinda akawa anamwambia akufuru afe .Ayubu hakusikiliza maneno ya mkewe .

✍ Upitapo katika majaribu acha kusikiliza maneno ya watu ambayo yanaweza kukuingiza kwenye kumkosea Mungu na kusababisha ukose kuinuliwa .



✍ Wapo watu wamejikuta hawainuliwi kwasababu ya kukimbia ugumu wa maisha wanayopitia kumbe 😨😨😨😨

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


Mungu alikusudia kufanya nao kazi mahali hapo na kuwaonyesha watu wengine kuwa yeye ni Mungu mweza wa mambo yote .Yeye ni Mungu anayewainua watu wake kutoka kwenye tabu na kuwaweka viwango vya juu .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– *Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.*

1 Samweli 2:8


✍ Kuwa na subira usilalamike kuwa umechoka .


✍  Mvumilivu ni shujaa

✍ Mvumilivu atapata mema .


✍ Mbinguni wanaingia wavumilivu watakaovumilia dhiki kuu wakiamini kuwa ipo siku Mungu atawatetea .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.


Ayubu 19:25



πŸ”° Vumilia shida upitiazo tambua Mungu yupo karibu atakutoa hapo uwe viwango vya juu .




Mungu akubariki sana


πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°✍πŸ”°πŸ”°πŸ”°πŸ”°

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*