ROHO MTAKATIFU


                           🍇 ROHO MTAKATIFU 🍇
SIKU YA KWANZA
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
Bwana Yesu asifiwe sana
Karibu sana katika ufunguzi wa semina yetu siku ya leo .
Biblia imezungumza habari za roho Mtakatifu tangu Agano la kale amezungumzwa sana lakini kwa namna ambayo msomaji wa biblia anatakiwa kumfuatilia kwa kina .
  Roho Mtakatifu alijifunua kwa watumishi wa Mungu ambao yeye aliwachagu
Ametajwa katika kitabu cha Isaya katika utatu mtakatifu .
 📖 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu , ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
Isaya 6:3
 Katika Isaya 6:3 tunaona neno Mtakatifu limetajwa mara tatu kudhihirisha jina la Mungu kwa namna ya utatu Mtakatifu .

Yaani Mungu baba, Mwana na Roho Mtakatifu
Mtakatifu , Mtakatifu , Mtakatifu .
Kwahiyo kwa waombaji wanaoanza kuomba wakianza na neno Mtakatifu lazima wataje mara tatu ili kumzunguzia Mungu katika utatu Mtakatifu .
  Roho Mtakatifu alifunuliwa kwa kinywa cha nabii Isaya
 📖 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Isaya 61:1
Nabii alifunuliwa habari hizi na kazi Roho Mtakatifu moja wapo ikiwa kutia mafuta ( upako ) .Kazi ya Roho Mtakatifu ni kumjaza mtu upako wa injili na nguvu za kiroho na mamlaka juu ya nguvu za giza  .
Maana yake ni kwamba Roho Mtakatifu akifanya makao ndani ya mtu , huyo mtu anakuwa na nguvu za kiroho na atafungua wengi sana .
 Roho Mtakatifu ni mtakatifu ( msafi , siyo mchafu ) hii ndyo sifa yake kuu .


Anakaa patakatifu
 📖 Msimzimishe Roho;
1 Wathesalonike 5:19
  Hawezi kukaa ndani ya mtu anayejichafua kwa dhambi .
Biblia ya English Revised  Version
Inasema tusiondoe kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu .
📖 Don’t stop the work of the Holy Spirit.
1 Thessalonians 5:9
ERV
Tutaondoaje kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu ❓
Ni kwa kutenda dhambi
 📖 You should know that your body is a temple for the Holy Spirit that you received from God and that lives in you. You don’t own yourselves.
1 Corinthians 6:19 ERV
Miili yetu ni hekalu ( nyumba ) ya Roho Mtakatifu kwahiyo ili akae ndani lazima tuwe safi .
Hatujimiliki wenyewe tuliookoka miili yetu ni mali ya Roho Mtakatifu
 📖 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
1 KOR. 6:19

 🍇 MATUNDA( KAZI) YA ROHO MTAKATIFU 🍇
Roho Mtakatifu ana matunda mengi sana katika maisha ya wokovu .
 🍇 Roho Mtakatifu anabadilisha tabia za mtu .
Anaondoa tabia mbaya na kumjaza mtu mambo saba ambayo Mungu anayataka ayaone ndani ya mtu .

Mambo haya ni yafuatayo :

🍇 Roho ya BWANA
Inakusaidia kudhirisha tabia za Mungu ndani yako .
Wakikuona watu waone sura ya Mungu.
🍇 Kumcha Mungu

🍇 Hekima

🍇 Ushauri

Kushauri watu kiroho.
🍇Ufahamu
Utakusaidia kupinga au kuikataa dhambi .


🍇 Uweza
Nguvu za Mungu
🍇 Maarifa
Yatakusaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako ya kiroho na kimwili bila kumkosea Mungu
📖 2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;
Isaya 11:2
Roho Mtakatifu anampa mtu uwezo wa kunena kwa lugha .
📖 1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
Matendo ya Mitume 2:1

2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Matendo ya Mitume 2:2
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
Matendo ya Mitume 2:3
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Matendo ya Mitume 2:4
Kunena kwa lugha ni moja ya kazi ya Roho Mtakatifu kwa aliyeokoka  .
📖 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.
1 Wakorintho 14:5
Kunena kwa lugha siyo kazi ya kufundishwa na mtu unene ni kazi ya Roho Mtakatifu hiyo kukufundisha wewe kunena , akikushukia utanena tu .
🍇 Roho Mtakatifu ni mwalimu .
📖 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
Luka 12:12
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Yohana 14:26
Anakufundisha ufanye nini
Unahitaji kumsikiliza Roho Mtakatifu nini anakwambia ufanye ili ufanikiwe kiroho na kimwili.
Unaweza ukapanga jambo fulani ulifanye lakini akilikataa utaona matokeo yake katika ulimwengu wa roho ( ulimwengu usioonekana ).
Mheshimu sana mwalimu wako ( Roho Mtakatifu ) akisema fanya hiki fanya akikataa acha .
Anatufundisha kuenenda katika kwa adabu na hekima  dunia hii , tusiwe na majibu mabaya kama watu wasiomjua Mungu .
Mungu akubariki sana naomba niishie hapo katika siku ya ufunguzi wa semina hii



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*