THAMANI YA UBIKIRA WAKO
🍇 THAMANI YA UBIKIRA WAKO 🍇
Mwl.Peter Francis
Masanja
0679392829
📖 Basi
watumishi wa mfalme waliomhudumu walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira
vijana wazuri;
Esta 2:2
🍇 Ijue thamani ya
ubikira wako ,
Jitunze , subiri ndoa .
📖 Mwenye
busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 22:3
📖 10 Mwanangu,
wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.
Mithali 1:10
🍇 Epuka makundi
yapotoshayo ili utunze ubikira wako .Epuka kujichafua
📖 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na
wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako.
Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
Ufunuo
wa Yohana 14:4
🍇 SABABU ZA KUPOTEZA UBIKIRA 🍇
Pointi
1;Kukosa hofu ya Mungu .
✍Uongo wa wanaume.
Pointi 2.Tamaa
Point 3: Makundi ya marafiki wabaya .
Pointi 4 . Utandawazi
Pointi 5: Ubakaji
Pointi 6: Malezi mabaya toka kwa wazazi
Pointi 7:Wanawake kukubali kutolewa
Kutaka kujaribu wajione
nao wamekua .
Pointi 8: Malezi hafifu ya kiroho .
Pointi 9: Ni mpango uliosukwa na shetani kuvuruga
ndoa za watu .
Pointi 10: Kuingia kwa mafundisho ya mashetani .
Pointi 11: Umaskini ( maisha magumu ).
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
🍇 Leo
nitazungumzia mambo yanayosababisha mabikira kupungua hapa duniani
✍ Katika darasa la jioni
hii tutaangalia sababu hizi ili vijana na wazazi pia watambue
✍ Kamwe hakuna apendaye
kununua bidhaa iliyotumika ili akaifanyie marekebisho .
✍ Kila mtu mume au mke
anapenda ampate mwenzi aliyejitunza na hili ndiyo kusudi kuu la Mungu .
✍ Kwa maana hii Mungu
anauthamini sana ubikira kuliko unavyofikiria .
✍ ✍
Kwenye biblia tukiangalia katika agano la kale tunaona kwamba
Mwanaume akimtoa binti
ubikira sharti amuoe kwasababu amemtia unajisi ( thamani ya usichana wake
imepotea tena ).
Na atakuwa amewaletea
aibu wazazi wake kwenye jamii
📖 13
Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia,
Kumbukumbu la Torati
22:13
14 kisha akamshitaki
mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami
nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira;
Kumbukumbu la Torati
22:14
15 ndipo babaye yule
kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee
wa mji langoni;
Kumbukumbu la Torati
22:15
16 na baba yake yule
kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye
amchukia;
Kumbukumbu la Torati
22:16
17 angalieni, amemwekea
mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo
alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa
mji.
Kumbukumbu la Torati
22:17
18 Basi wazee wa mji
ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi,
Kumbukumbu la Torati
22:18
✍ Ubikira ukitolewa
thamani ya binti inakuwa haipo tena , ndyo maana enzi za Musa kijana akimtoa
ubikira binti lazima amuoe
.✍
Bikira ilithaminiwa mno hapo zamani na ndoa zilikuwa hazina migogoro mingi na
mababu zetu walizeekea kwenye ndoa .Lakini leo miaka miwili tu mikwaruzo .
📖 Naye
yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua
bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.
Mwanzo 24:16
✍ Raheli mke wa Yakobo
alimuoa bikira ✍✍✍✍✍✍✍
✍ Ubikira unaambatana na
malezi mazuri , ukikuta familia mabinti bikira hiyo familia inaheshimika sana.
✍ Binti kutolewa bikira
ni ishara ya malezi feki na wazazi kukosa utii mbele za Mungu .
📖 Hawa
ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio
wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu,
malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
Ufunuo wa Yohana 14:4
✍ Ubikira wa kiroho
yaani kutokutumikia miungu mingine baada ya kuzaliwa mara ya pili unathamani
sana kwa Mungu
Huu unafananishwa na
ubikira wa mwili thamani yake kutokutiwa unajisi .
✍ Mungu mwenyewe anasema
mbinguni wataingia mabikira ( wasiotiwa unajisi kwa kuabudu sanamu au
kumtumikia shetani yaani wasio na chapa ya ibilisi )hawa wasio na chapa ya
shetani ( maovu ) ni mabikira mbele za Mungu .
Kwahiyo Ubikira lazima
utunzwe sana .Usiguswe na mwanaume yeyote subiri uolewe kabisa , mwili wako ni
kwaajili ya mume wako .
Nawewe mwanaume usiguse
binti yeyote subiri uoe maana mwili wako ni kwaajili ya mkeo tu .
📖 2
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili
nimletee Kristo bikira safi.
2 Wakorintho 11:2
3 Lakini nachelea; kama
yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu,
mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
2 Wakorintho 11:3
✍ Mungu anataka kuona
watu wakioana mabikira
✍ Kwahiyo thamani ya
ubikira inatambuliwa na Mungu pia kuwa ni usafi
Kipindi kijacho
tutaangalia hasara za kutolewa ubikira wako .✍✍✍✍✍✍✍✍
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni