TOBA NA UTAKATIFU ✝*
*π TOBA NA UTAKATIFU ✝*
Mahali : JESUS CO-WORKERS MINISTRY
SIKU YA KWANZA
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
*UTANGULIZI*
π Bwana Yesu apewe sifa
π Nakukaribisha sana katika semina hii ya neno la Mungu upate kujifunza yale ambayo Roho wa Mungu amenipatia hivi leo .
π Ikiwa leo ni siku ya kwanza ya semina hii somo letu linasema
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
πTOBA NA UTAKATIFU π
✍ Tuangalie kwanza maana ya maneno haya mawili .
✍ Toba ni nini ❓
πWhat's repentance ❓
✍ Toba ni ile hali / kitendo cha kujutia juu ya kosa( dhambi ) ulilolifanya na kuomba msamaha kuwa hutarudia tena kulifanya .
π Repentance is the act of showing that you're sorry for something wrong that you have done .
✍ Katika toba kuna kujutia kwa kile ulichokifanya yaani kibaya ulichokifanya .
: ✍ Mtu yeyote wa toba lazima ajutie baada ya kutambua kwamba kitendo alichokifanya ni chukizo mbele za Mungu .
✍ Kisha atachukua hatua ya kumwomba Mungu amsamehe , amtakase, amuoshe, amsafishe , maana dhambi ni uchafu na inamfanya mtu awe adui Mungu.
: ✍ Neno toba linaelezewa na maneno yafuatayo kwenye biblia
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
1⃣ JIOSHENI
✍ Mtu anapojiosha maana yake ni mchafu anatakiwa awe msafi .
✍ Kwa lugha ya kiroho mchafu ni mwenye dhambi na msafi ni mtakatifu.
✍ Ndiyo maana tunaambiwa tujioshe dhambi zetu yaani tutubu ili tuwe safi ( watakatifu ) .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 16 *Jiosheni* , jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Isaya 1:16
Mungu anakuomba ujioshe ndyo umweleze mambo yako .
2⃣ *JITAKASENI* ( KUJITAKASA)
✍ Tunapoambiwa tujitakase Mungu anatuambia tuwe watu wa toba tunapotubu Mungu hutufanya kuwa safi kabisa .
π» 16 Jiosheni, *jitakaseni* ; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Isaya 1:16
✍ Utakatifu ( usafi ) wa mwanadamu upo katika kujitakasa dhambi zake .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 7 Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Mambo ya Walawi 20:7
✍ Baada ya kujitakasa kinachofuata ni utakatifu yaani ni usafi ( bila dhambi ) .
✍ Mtu anapoambiwa ajitakase maana yake kuna uchafu ndani yake ( dhambi ) na kujitakasa hapa ni kwa njia ya toba pekee kwa kutumia sabuni ya kiroho iitwayo damu ya Yesu , kisha mtu anakuwa msafi yaani mtakatifu baada ya kuuondoa uchafu ( dhambi ).
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 5 akawaambia, Nisikieni, enyi Walawi; *jitakaseni* nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu, mkautoe uchafu katika patakatifu.
2 Mambo ya Nyakati 29:5
3⃣ *JISAFISHENI*_( KUJITAKASA).
✍ Toba pia inatambulishwa na neno kujisafisha
✍ Usafi wa mtu ni kimwili na kiroho pia .
✍ Aliyeokoka anahitaji usafi wa mwili na roho pia .
✍ Simaanishi usafi wa kuchukua maji ukaoge na kujichubua bali namaanisha kuwa huo mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu usiuchafue kwa dhambi kama vile zinaa .Tafadhali kuwa msafi .
✍ Usafi wa roho maana yake utu wako wa ndani umtukuze Mungu ujaze mema .
✍ Kwahiyo usafi wetu ni kwa njia ya toba pekee .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 7 Basi, *jisafisheni* , mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
1 Wakorintho 5:7
✍ Toba inakupa kibali mbele za Mungu yaani kumiliki na kutawala .
✍ Kila aliye safi anakibali cha kuomba chochote kwa Mungu naye atapewa .
✍ Kila aliye safi anamamlaka juu ya adui
✍ Kila aliye safi anauwezo wa kusimama mbele ya adui na kushinda .
✍ Kila aliyesafi anaweza kuingia popote akiongozwa na Roho wa Mungu kwaajili ya kazi yake .
✍ Haya yote ni kwasababu ya toba ( kutubu dhambi ) .
πUTAKATIFU
✍ Biblia inazungumzia sana neno utakatifu .
✍ Hata biblia yenyewe pia ni takatifu yaani Biblia Takatifu ( Holy Bible ).
✍ Hata maandiko nayo ni matakatifu , yaani ni Maandiko Matakatifu ( Holy Writ/ Scriptures).
π Kama biblia tu na maandiko ni takatifu na maneno yote yaliyomo .
✍ Basi na aisomaye ili aweze kuisoma na kuelewa siri za Mungu anahitaji kuwa Mtakatifu .
✍ Anahitaji kuwa Mtakatifu kwa sababu anahitaji msaada wa Roho Mtakatifu ili amfundishe maana ya yale yaliyoandikwa humo .
✍ Roho Mtakatifu anakaa kwa Mtu Mtakatifu kwa sababu yeye ni Mtakatifu .
✍ Mtu Mtakatifu ni mtu wa toba na rehema yaani ni yule anayetubu na kuacha dhambi .
✍ Utakatifu ni nini ❓
π Utakatifu ni hali ya kutengwa na uchafu ( kuwekwa mbali na dhambi ) kwa ajili ya kazi ya Mungu .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni *watakatifu* , kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.
Mambo ya Walawi 11:44
45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
Mambo ya Walawi 11:45
✍ Kinachotangulia ni toba kwanza ndyo utakatifu unafuata .
✍ Bila utakatifu hakuna mtu awezaye kumwona Mungu .
Maandiko yanasema hivi
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo *utakatifu* , ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
✍ Utakatifu ni tiketi ya kumwona Mungu .
✍ Utakatifu ni tiketi ya kuingia uzima wa milele ( Kuurithi Ufalme wa Mungu ) .
✍ Utakatifu pia kwa lugha nyingine huitwa
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π Utauwa
π» 7 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata *utauwa* .
1 Timotheo 4:7
8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini *utauwa* hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
1 Timotheo 4:8
✍ Utakatifu( utauwa) ni kwaajili ya uzima wa milele.
✍ Utakatifu unapatikana katika kumcha Mungu huku tukijitakasa nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho .
✍ Unapojitakasa unakuwa na utu upya yaani maisha ya bila lawama kwa Mungu .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» _24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu_ wa kweli.
Waefeso 4:24
π» *10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;*
1 Wathesalonike 2:10
MIZANI YA UTAKATIFU⚖*
π Utakatifu wa mtu hupimwa kwenye mizani miwili .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
1⃣ Mwili
2⃣ Roho
Kama wewe ni msomaji wa biblia utaona Belshaza mfalme wa Babeli alipimwa kwenye mizani akaonwa amepungua , yaani alipimwa kiroho na kimwili akaonwa anadhambi kwahiyo hafai tena kutawala .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π» 27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.
Danieli 5:27
✍ Kwa tafsiri rahisi alipungukiwa na Utakatifu kwa kutenda dhambi .
✍ Chunga sana utakapopimwa na Mungu kwenye mizani halafu akute neno TEKELI π€£π€£
✍ Watu wataona TEKELI kwa matendo yako ya mwili pia yasiyomfurahisha Mungu .
π» 34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, *apate kuwa mtakatifu mwili na roho* .
1 Wakorintho 7:34
✍ Mwili wako ni chombo kitakatifu
π» 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
1 Wakorintho 6:19
✍ Ukiuharibu mwili wako nawe utaharibiwa na Mungu
π» 16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1 Wakorintho 3:16
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
1 Wakorintho 3:17
✍ Mungu akikuchagua umtumikie anakuta Mtakatifu kama yeye alivyo ,
✍ Ukijichafua anaweza kukuadhibu .
π» 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
2 Wakorintho 6:16
Wewe ni chombo kitakatifu kwa Bwana
✍ Ili uwe mtakatifu dumu katika maisha ya toba
Ufunuo 22:11
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni