UFUNUO JUU YA MAKANISA SABA NA SIKU ZA MWISHO

 πŸ‡ UFUNUO JUU YA MAKANISA SABA NA SIKU ZA MWISHO πŸ’’


              Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829


https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry



✍ Ni muhimu sana mtu wa Mungu kujua habari za unabii juu ya makanisa saba ambayo biblia inayasema .



✍ Ni lazima utambue wakati maarifa yanazidi kungezeka maovu yanazidi kuongezeka pia
.

✍ Kanisa linazidi kufanya maovu , waliookoka nao wanakumbatia dhambi .


✍ Ni kipindi ambacho utandawazi umeingia kwa kasi na manabii wameongezeka lakini wengi ni wauongo kabisa


✍ Kama ilivyonenwa katika Daniel ya kuwa maarifa yataongezeka na maovu pia yataongezeka kwa kasi .


Kweli hata mitandao imeboresha dhambi .



πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 4 Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. 


Danieli 12:4


✍ Kipindi ambacho watu wataikataa kweli na kufuata mafundisho ya mashetani .Mafundisho yadanganyayo


πŸ“– 1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 


1 Timotheo 4:1

2 kwa unafiki   wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 


1 Timotheo 4:2



Next......
[20:32, 8/24/2018] Mwl.Peter Francis Masanja: πŸ’’ EFESO 


πŸ“– 1 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. 

Ufunuo wa Yohana 2:1

2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 

Ufunuo wa Yohana 2:2

3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. 


Ufunuo wa Yohana 2:3

4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 

Ufunuo wa Yohana 2:4



✍ Hili ni kanisa la kipindi cha mitume 12 wa Yesu Kristo .

✍ Ni katika kipindi hiki kulikuwa na mafundisho ya utakatifu na upendo wa Mungu .


✍ Lakini baadaye tunaliona kanisa hili linauacha upendo wa kwanza baada ya mitume wa Yesu kufa .


πŸ“– 21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 

Yohana 14:21

23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 

Yohana 14:23

24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. 

Yohana 14:24



✍ Ni kipindi hiki watu waliyaacha mafundisho waliyofundishwa na mitume kuhusu kumpenda Mungu na kushika amri zake wakarudi nyuma



 πŸ’’ SMIRNA


✍ Katika wakati wa kanisa hili kulitokea wafalme wakatili walitaka kuingiza  desturi za kipagani ndani ya kanisa na kuwaua watakatifu wa kanisa na kufanya mbinu za kuiondoa biblia katika dunia hii.

✍ Kinaitwa kipindi cha mateso na machungu .



πŸ“– 8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.

Ufunuo wa Yohana 2:8

9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.

Ufunuo wa Yohana 2:9

10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Ufunuo wa Yohana 2:10


πŸ’’ PERGAMO
( 312- 590 B.K)

✍ Ni kanisa lililofunga ndoa na upagani .


✍ Ni kipindi ambacho mfalme Constantine aliutangaza Ukristo ndio dini ya Rumi au Taifa .


✍ Ni kipindi ambacho sanamu ziliingizwa kanisani .


✍ Ni kipindi ambacho ubatizo wa kunyunyiziwa au kupakwa  maji kichwani uliingizwa kanisani .Ubatizo huu uliletwa na mfalme Constantine baada ya kuamua kunyunyiziwa akidai yeye ni mfalme hawezi kwenda mtoni kuzamishwa kwahiyo wakauiga mpaka na kanisani .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

Ufunuo wa Yohana 2:12

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

Ufunuo wa Yohana 2:13

14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

Ufunuo wa Yohana 2:14

15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

Ufunuo wa Yohana 2:15

16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

Ufunuo wa Yohana 2:16

17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

Ufunuo wa Yohana 2:17


πŸ’’ THIATRA

( 590-1517)


✍  Ni kipindi cha giza ndani ya kanisa .
Mfano wa sadaka katika kipindi hiki ni

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ™†πŸ»‍♂ Kutoa sadaka ili kuwatoa ndugu waliokufa motoni yaani mafundisho ya Pugatori au toharani .


✍ Ni kipindi ambacho kulikuwa na mafundisho ya kuwa wokovu unapatikana kwa sadaka .


✍ Ni kipindi ambacho Uislamu ulianza


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 18 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


Ufunuo wa Yohana 2:18

19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.


Ufunuo wa Yohana 2:19

20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Ufunuo wa Yohana 2:20

21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.


Ufunuo wa Yohana 2:21

22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;


Ufunuo wa Yohana 2:22

23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Ufunuo wa Yohana 2:23

24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.

Ufunuo wa Yohana 2:24

25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.


Ufunuo wa Yohana 2:25

26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,


Ufunuo wa Yohana 2:26

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.


Ufunuo wa Yohana 2:27

28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.


Ufunuo wa Yohana 2:28

29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ufunuo wa Yohana 2:29




 SARDI


( 1517-1750)


✍ Haya ni majira ambayo kanisa lilikuwa limekufa kabisa na linajina la kuwa hai .

✍ Walikuwepo wachache waliotoroka kutoka kwenye kanisa Katoliki baada ya kugundua giza lililopo ndani yake .


✍ Ni kipindi ambacho Martin Luther alipingana na Katoliki baada ya kuona baadhi ya ibada za kishetani .

✍  Martin Luther aliondika makosa 95 ya kanisa Katoliki kutokana na kanisa kuingiza sanamu kwenye mfumo wa ibada .


✍ Ni kipindi ambacho alihubiri kuwa wokovu unapatikana kwa imani na neema na siyo kwa matoleo ya aibu .



✍ Ni kipindi ambacho biblia ilikuwa adimu sana kwa watu .Maandiko na nuru ilikuwa imepotea ila kupitia watu kama Martin Luther ndio wakaanza kufanya matengenezo .

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.


Ufunuo wa Yohana 3:1

2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.


Ufunuo wa Yohana 3:2

3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Ufunuo wa Yohana 3:3

4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


Ufunuo wa Yohana 3:4

5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba
 yangu, na mbele ya malaika zake.

Ufunuo wa Yohana 3:5

6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ufunuo wa Yohana 3:6


SARDI maana yake waliotoroka


 πŸ’’ FILADEFIA

( 1750-1905 B.K )


✍ Hiki ni kipindi cha uhamsho wa kipekee


✍ Kulitokea wahubiri waliokuja na nguvu za kuhubiri neno na utakatifu .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ“– 7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

Ufunuo wa Yohana 3:7

8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

Ufunuo wa Yohana 3:8

9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

Ufunuo wa Yohana 3:9


✍ Kulikuwa na wahubiri kama

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

πŸ‘‰πŸ» John Wesly alihubiri kuhusu utakaso .

πŸ‘‰πŸ» Charles Finny alihubiri kuhusu usafi ,utakatifu na upendo wa kindugu .


FILADEFIA maana yake ni upendo wa kindugu



   πŸ’’ LAODIKIA

( 1905- Unyakuo )


πŸ‘‰πŸ»Hili ni kanisa la mwisho


✍ Ni majira ya maarifa kuongezeka yaani siku za mwisho na kanisa la mwisho .


✍ Ni majira ambayo Yesu alitabiri kutakuwa na
πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

MANABII WENGI WA UONGO


✍ Kipindi chote cha nyuma kabla ya mwaka 2000 hawakuwepo watu wanaojitangaza kuwa manabii.



✍ Lakini leo wapo wengi sana wanaojiita manabii .

✍ Ni kipindi Yesu Kristo alitabiri kuwepo kwa kanisa la mwisho yaani Laodikia .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


πŸ“– 14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

Ufunuo wa Yohana 3:14

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

Ufunuo wa Yohana 3:15

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Ufunuo wa Yohana 3:16

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Ufunuo wa Yohana 3:17

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Ufunuo wa Yohana 3:18

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

Ufunuo wa Yohana 3:19



✍ Kutokana na maarifa kuongezeka kwa kasi kanisa limekuwa na magari , ndege,n.k ili kurahisisha injili.


✍Ni kipindi ambacho kumekuwa na wizi makanisani  .Viongozi wa makanisa wanaficha mali ya kanisa kutokana na roho ya tamaa.


✍ Ni kipindi ambacho mahubiri ya utajiri yamezagaa sana kama vile kuombewa upate gari, pesa yaani vitu vya dunia .



✍ Ni kipindi ambacho watu wengi wanakimbia huku na huku kutafta maombezi yaani kuombewaombewa .



SIFA ZA MITUME NA MANABII WA UONGO


✍ Najua unasikia kila kona kuna mitume na manabii lakini wengi ni wa uongo .Angalia sifa zao .


πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


😩 Wanajipima kwa mafanikio ya vitu kama magari  , ndege,n.k wakati makanisa wameyabandika maturubai na mabati.


😨. Wanahubiri mambo ya mwilini ambayo hayawajengi watu kiroho yaani wanawaua kiroho .


😨. Wana ishara na ajabu za uongo huku wakiwatabiria watu kama waganga wa kienyeji .

😨 Wanapepo wa utambuzi kama waganga wa kienyeji tofauti yao ni kwamba wao huvaa suti tu lakini waganga nguo nyeusi yaani shuka jeusi.


😑 Wanapenda sana kusifiwa na kuwatumikisha wengine .


😨 Wanahubiri vitu vinavyoonekana lakini  visivyoonekana vya rohoni ambavyo ni vya milele hakuna


πŸ“– 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Wakolosai 3:2


πŸ“– 6 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.

1 Timotheo 6:6

7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;

1 Timotheo 6:7

8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

1 Timotheo 6:8

9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

1 Timotheo 6:9

10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

1 Timotheo 6:10



πŸ’’ Nabii wa kweli atahubiri toba na kukemea dhambi hadharani .


πŸ“– 11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.

Warumi 3:11

12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.

Warumi 3:12

13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.

Warumi 3:13

14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.

Warumi 3:14



Pia rejea Ebr 1:9 , Yer 23:29, Luk 17:26-30



✍ Kipindi hiki pia Yesu Kristo alitabiri kuwa upendoa wa wengi utapoa ( Math 24:11-12)


✍ Yesu Kristo alitabiri kuwa watu watakataa maonyo na kufuata mambo ya dunia ambayo yatawapeleka motoni .Alisema kutakuwa na wahubiri wanaotetea mambo ya kishetani wakiwapiteza watu .


Mungu akubariki sana kwa kufuatilia somo hili hadi mwisho

Karibu tena kwenye mwendelezo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*