USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA

*🤣 USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA 🔥*


Mwl.Peter Francis Masanja


What's app group

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

https://chat.whatsapp.com/HEplO5f5kuDA74vGPdIxI8


What's group App

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry



BWANA YESU ASIFIWE 💒




✍ Kuna kitu mtu wa Mungu lazima utambue kwamba hizi ni nyakati za mwisho.


✍ Nyakati hizi ni nyakati za hatari sana kwasababu watu wanaikataa kweli waziwazi wakifuata mafundisho ya uongo yatakayowapeleka motoni .

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
_
1 Timotheo 4:1

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

1 Timotheo 4:2



✍ Siku hizi za wisho kumeibuka mahubiri ya majumba , magari, pesa , n.k


✍ Ni kipindi ambacho mambo mengi yanayofurahisha mioyo ya watu ambayo yapo kinyume cha Mungu yanaruhusiwa katika baadhi ya makanisa.


✍ Kipindi hiki dhambi haikemewi na baadhi ya wahubiri wanahubiri utajiri kuliko kuwahubiri watu waokoke waishi maisha matakatifu .




✍ Baadhi ya watumishi walioitwa na Mungu wakikemea dhambi kama maandiko yasemavyo

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;


2 Timotheo 4:1

2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


2 Timotheo 4:2

3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;


2 Timotheo 4:3

4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.


2 Timotheo 4:4

5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.


2 Timotheo 4:5


✍ Basi watu hawa wakikemea dhambi ( uovu ) wanachukiwa sana .

Kutokana na kukariri maandiko bila kuyajua wakemewao huwaambia hivi

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.


Mathayo 7:1


✍Wakisahau kuwa maandiko yanasema .

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?


1 Wakorintho 6:2

3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?


1 Wakorintho 6:3




✍ Basi kwa sababu ya kuikana kweli watu wanakataa maonyo na kufuata roho zidanganyazo huku wakienda motoni.



✍. Imekuwa desturi ya watu waliookoka wakiambiwa acha dhambi hii itakupeleka motoni .

Wanaikataa kweli wakidai wanahukumiwa huku wakimwasi Mungu .



Mwisho wa kunukuu hatukulazimishi kupokea maonyo .

Chagua kupokea maonyo ukaishi au uyakatae ufe .



https://peterfrancismasanja.blogspot.com



YER 15:19-20

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*