USIPENDE KUOMBEWAOMBEWA , SIMAMA MWENYEWEπ*
*π USIPENDE KUOMBEWAOMBEWA , SIMAMA MWENYEWEπ*
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
✍ Wakati natoka kwenye ibada ya maombi mchana huu Roho wa Mungu akaniambia , Mwl.Peter waambie watu wangu waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao kwamba ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
Sitasema nao kupitia wewe bali nitasema nao kupitia neno hili ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π *_1 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe_*
Ezekieli 2:1
✍ Mtu wa Mungu baada ya kusikia hiyo sauti nikaona tena nikukumbushe kwamba Mungu anasema na wewe kupitia maombi yako .
✍ Hajaishia hapo akakusafisha ukawa safi kabisa , ukatakaswa
Kama maandiko yanavyosema hapa
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π 9 Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta;
Ezekieli 16:9
✍ Kumbuka Mungu alipokutoa ulikuwa mchafu yaani kwenye uchafu kweli kama maandiko yanavyosema hapa
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π 4 Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
Ezekieli 16:4
5 Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.
Ezekieli 16:5
6 Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai.
Ezekieli 16:6
✍ Bado tena akaniambia nikuambie kwamba ili uweze kusimama mbele za adui lazima uache maisha ya dhambi ili awe pamoja nawe .
Kama maandiko yasemavyo :
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Waamuzi 2:14
✍ Baada ya kuacha dhambi Mungu atawapiga adui zako wote nawe huku ukiuona ukuu wa Mungu .
π 20 Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.
Yeremia 15:20
21 Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.
Yeremia 15:21
✍ Akaendelea kusema kwamba , unaweza ukateswa na magonjwa mengi sana kwasababu umemwacha Mungu na kugeukia miungu mingine ππ»♂ππ»♂ππ»♂ππ»♂
π² Embu angalia hii miungu unayoweza ukawa unaitumikia .
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
Uzinziπ
Uasheratiπ
Chukiπ
Hasira ambayo huzaa uchungu
Na matokeo yake vidonda vya tumbo ππ»♂ππ»♂
Baada ya kuitumikia miungu hiyo Mungu akakutenda mabaya .
Kama maandiko yanavyosema
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π 11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
Waamuzi 2:11
12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
Waamuzi 2:12
13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
Waamuzi 2:13
14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Waamuzi 2:14
15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
Waamuzi 2:15
✍ Akasema tena kwamba siyo kila shida uliyonayo ni shetani bali kuna dhambi siku ukiiacha ukatubu Mungu ataokoa kabisa .
Inawezekana ni binti unasumbuliwa na mapepo unaenda kanisani kuombewa yanatoka
Halafu jioni unaenda kwa bwana kujichafua π
Mapepo yanarudi tena zaidi ya sana πππ
Usipoacha hiyo dhambi utamaliza watumishi wote bila kupona π₯π₯π₯π₯
Ondoa hiyo miungu ili Bwana akuponye
✍ Mungu hakufrahii kuugua kwako lakini anataka uondoe miungu uliyonayo
Hata michepuko ni miungu π€£π€£π€£
Ulevi ni miungu πππ
Zinaa kwa ujumla ni miungu π€£π€£π€£
Embu kuanzia leo kaondoe uone kama Mungu hajakuweka viwango vya juu
Israel walipoiondoa miungu , Mungu aliwaponya kabisa kama maandiko yasemavyo
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π 15 Wana wa Israeli wakamwambia Bwana Tumefanya dhambi; utufanyie yote uyaonayo kuwa ni mema; lakini tuokoe, twakusihi, siku hii ya leo, haya tu.
Waamuzi 10:15
16 *Nao wakaiondoa hiyo miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia Bwana; na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.*
Waamuzi 10:16
✍ Kumbe matatizo mengine chanzo chake ni dhambi zetu π¨π¨π¨π¨
Ili tupone lazima kuacha hizo dhambi lazima useme
Kwaheri uzinzi ππππ»♂ππ»♂
Kwaheri uasherati ππππ»♂ππ»♂
Kwaheri michepuko mmenifilisi mno mkaniharibia ndoa yangu ππππ»♂ππ»♂
Kwaheri pombe ππππ»♂ππ»♂
Kisha Yesu akamponya yule mgonjwa akamwambia hivi
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π *Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.*
Yohana 5:14
✍ Kwahiyo napenda nikwambie kwamba ili Mungu akutendee simama mwenyewe acha uovu kisha omba lolote atakutendea .
Kama maandiko yanavyosema
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π *Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa* .
Yohana 15:7
✍ Basi na mimi Mwl.Peter Francis Masanja nahitimisha kwa kusema kwamba
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π Unaweza ukasimama mbele za Mungu ukisema akuponye lakini kama unaishi maisha ya dhambi kupona kwako sahau .
✍ Hata ubadilishe watumishi kama nguo kama hujaacha dhambi mabaya yatakuandama tu .
Mwisho kabisa nasema hivi ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
π₯ Ili Mungu aseme na wewe na akuokoe zingatia saaana yafuatayo
ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
ππ» Tubu na kuacha dhambi kabisa.
ππ» Ishi maisha ya kufunga na kuomba
ππ» Soma neno .
Na mengineyo .....
Mungu akubariki sana
ππππππππ
Maoni
Chapisha Maoni