USIUIGE UBAYA

💒 *USIUIGE UBAYA* 💒


✍ Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


💻 11 *Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.*

3 Yohana 1:11



✍ Kuna baadhi ya Wakristo leo kanisani wamekuwa waigaji wa maovu kutoka kwa watumishi waovu .



✍ Wakristo hawa wanaitwa wa kina *mbona fulani anafanya*😨😨


✍ Wakristo hawa wamekuwa adui wa Mungu kwa kuiga ubaya.

✍ Wanajidhania wao ni watu wa Mungu kumbe wanamilikiwa na ibilisi .


✍ Wamebaki kusema kwamba

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


🤷🏻‍♂ mbona mtumishi fulani anafanya .

🤷🏻‍♂ Mbona fulani alizaa kabla ya ndoa na amebarikiwa .

🤷🏻‍♂ mbona kuna mtumishi anafanya hilo lakini akisimama madhabahuni anaupako ❓



✍ Tumefikia nyakati za hatari ambapo watu wanaiga ubaya yaani dhambi .

✍ Ninataka ujifunze kwamba ukiwa na kauli za mbona fulani anafanya ujue unamilikiwa na adui .


✍. Iga mema usiige ubaya maana aigaye ubaya ni wa shetani .

✍ Wengi wameshindwa kujua kwamba upako hautoki kwa Mungu pekee hata shetani anaupako na anatenda ishara na ajabu .


✍ Pia utambue kuwa hata mashetani nayo hunena .


✍Unaposema mbona fulani anafanya unamsaidia shetani kueneza uovu kanisani na anakumiliki kabisa ijapokuwa unajihudhurisha kanisani wewe ukifikia hatua ya mbona fulani ujue huko unakoelekea utamaliza vibaya safari yako ya wokovu .

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


💻 8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.

Mhubiri 7:8



✍ Ulipookoka hukuiga ubaya ulianza vizuri sana lakini umesoma neno na kuanza kusema mbona fulani .


✍ Je , unatambua kuwa unaweza ukawa mhubiri mzuri sana na mwimbaji mzuri sana kanisani lakini kama unaiga ubaya wewe ni mtumwa wa shetani ❓

✍ HizBwana Yesu asifiwe hazikufishi mbinguni kama unaiga ubaya maana Mungu atakuja kuchambua kanisani mbuzi na kondoo .

Heri uwe kondoo .

✍ Usiseme unamjua Mungu kama unaiga ubaya

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

💻  16 *Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.*

Tito 1:16



Mungu akubariki sana


Nakutakia tafakari njema .

Mwl.Peter Francis Masanja

From : SMM

App : https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry


💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*