*USIUTAZAME WINGI WA ADUI UKAOGOPA




 *USIUTAZAME WINGI WA ADUI UKAOGOPA*



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



😨 Nikimkumbuka Yehoshafati mfalme wa Yuda naona picha ya hofu ndani ya moyo wake .Kama maandiko yanavyosema


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻



📖 3 Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.


2 Mambo ya Nyakati 20:3


✍ Yehoshafati alipoona majeshi ya Wana wa Moabi , na wana wa Amoni  na Wameuni .
Aliogopa sana

✍ Pamoja na kwamba aliogopa tunaona hakuzubaa alikumbuka wokovu upo kwa BWANA peke yake haijalishi adui wamekusanyana majeshi mangapi


✍ Nikimzungumzia Yehoshefati wa leo nakuzungumzia wewe mtu wa Mungu .


Maandui wamekuzunguka kila kona lakini ni marufuku kuchukua uamuzi wa kibinadamu yaani kupigana na adui kwa mwili bila kuanza kumwuliza Mungu

✍ Ninapomsoma Yehoshafati katika sala yake namwona akisema


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 *6 akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.*

2 Mambo ya Nyakati 20:6


✍ Wewe kama Yehoshefati wa sasa unapo tatizo au adui wa mafanikio yako tambua yafuatayo kwa Mungu


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

🍇 Anatawala falme zote za mataifa

Maana yake hata adui zako anawatawala kwahiyo sema naye awakatilie mbali kabisa .


🍇 Mkononi mwake mna

👉🏻 Uweza na

👉🏻 nguvu


Kwahiyo usiogope adui ita mkono wa BWANA ushuke ukuokoe

Pia soma

ISAYA 59:1



🍇 Hakuna awezaye kusimama kinyume cha Mungu .

✍ Uonapo adui usiogope omba msaada wa Mungu ushuke juu yako naye atawaondoa maadui .



✍ Basi sitapenda nikuache hujatambua maana ya kuutafta uso wa BWANA

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Kuutafta uso wa BWANA maana yake ni kumwuliza Mungu juu ya tatizo fulani uliloliona katika ulimwengu wa macho akupe sababu ya jambo hilo kutokea na akupe namna ya kuliondoa . 2 Samweli 21:1


Kumbuka kuutafta uso wa Bwana ni kuomba msaada juu ya tatizo unaloliona kwa macho yako akuokoe .


✍ Nahitimisha kusema kwamba


Usiogope adui kamwe , muite Mungu atakupigania

Adui ni pamoja na mazingira magumu unayopitia , usinung'unike mwite Mungu siku zote atakutendea mema kama neno lisemavyo

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 4 Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.


Zaburi 27:4





Mungu akutendee mambo mazuri , usiogope wingi wa adui au shida ulizonazo ukasema Bwana amekuacha .


Hajakuacha

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


 📖 14 Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.

Isaya 49:14

15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Isaya 49:15

16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Isaya 49:16


Pakua app kupokea masomo ya kila siku

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry


Mungu akubariki sana

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*