🍇 UTII NI KITU BORA

       *🍇 UTII NI KITU BORA  🍇*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry


💻 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.


Warumi 13:1

Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.



Warumi 13:2



💻 Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu.


Waroma 13:1 BHN




✍ Lazima utambue kwamba mamlaka yoyote ipo chini ya Mungu .


✍ Jifunze kutokubishana na mwenye mamlaka yaani kujibizana na kiongozi wako .


✍ Ukiona katika Serikali watu wanapigwa risasi usifikiri kila anayepigwa risasi hana hatia .


✍ Kuna njia nzuri za kumkosoa mwenye mamlaka na siyo kumkosoa kwenye jamii , hapo lazima utatafutwa na kukamatwa utiwe gerezani au kuuawa kabisa .


✍ Ukiona viongozi wa pande pinzani wanatiwa mbaroni usisingizie Raisi dikteta huo ni uongo kabisa .Raisi ni mpole lakini kwasababu umeamua kumdhalilisha public hapo lazima utachezea cha moto .

✍ Katika mfumo wowote wa utawala epuka malalamiko ya kutapakaa kwa kila mtu maana huchochea uvunjifu wa amani .


✍  Hakuna nchi nzuri niipendayo kama Tanzania

Tanzania kila mtu anapata nafasi ya kulala mpaka kunakucha .


✍ Angalia nchi za wenzetu kama Burundi na Kongo ukilala mpaka asbuhi wewe una Mungu wako


✍ Hayo yote ni kwasababu ya kukosa utii na kushindwa kulijua neno la Mungu vizuri .

✍ Utii ni kitu bora na cha thamani sana .

✍ Kwahiyo mtu asiyetii hichochea machafuko na kuleta umwagaji wa damu .


✍ Usipotii utatii kwa upanga , maana asiyeitii mamlaka iliyowekwa na Mungu atatii kwa upanga au kwa kutiwa gerezani .


✍ Hii ni kwa sababu asiyetii ni adui wa amani .


💻 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;


Warumi 13:3

4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.

Warumi 13:4


✍ Ni heri kumpoteza mtu mmoja anayetaka kuleta umwagaji wa damu za watu kuliko kumwaga damu za watu wengi .


✍ Mfalme , au mtawala anamamlaka ya aliyopewa na Mungu kuamua akupoteze wewe unayetaka kusababisha damu za watu zimwagike kwa sababu ya uchochezi wako .


✍ Epuka kufunua kinywa chako kumnena mabaya mtawala ( mfalme / Raisi ) kama una la moyoni mfuate kwa hekima ukaseme naye .


✍ Au ni baba yupi atukanwaye na mkewe mbele ya watoto wake ❓

Mtii mwenye mamlaka .


✍ Naamani pamoja na ushujaa wake alitii neno la BWANA akaenda kukichovya mara saba Yordani akatakasika ukoma wake ukatoka .


✍ Hili jambo la watu kuuawa wale wanaoibuka kinyume na mwenye mamlaka lipo hata kipindi cha mfalme Daudi .


✍ Naamani asingetii asingeweza kushinda vita na angekufa .


💻 1 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
2 Wafalme 5:1

2 Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.
2 Wafalme 5:2

3 Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
2 Wafalme 5:3

4 Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
2 Wafalme 5:4

6 Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake.
2 Wafalme 5:6

12 *Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi* ? Akageuka, akaondoka kwa hasira.


2 Wafalme 5:12

13 *Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi* ?


2 Wafalme 5:13

14 *Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi* .


2 Wafalme 5:14


✍ Naamani alionyesha jeuri maana hakujua hiyo mamlaka umetoka kwa nani akakataa kuitii , mpaka watumishi wake walipomsihi akakibali akaenda Yordani kujitosa kwenye maji mara saba akatakasika .


✍ Naamani asingetii angeuawa kabisa maana vita ilikuwa kali sana.


📙 Hitimisho


✍ Jifunze kutii ili uwe salama .


✍ Tii mamlaka iliyowekwa na Mungu


✍ Epuka kuongea sana isije ikawa chanzo cha umwagaji damu .


🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*