DARASA LA MAOMBI*

🖊 Mwl.Peter Francis Masanja


0679392829



📖 *DARASA LA MAOMBI* 📖🖊


✍ Kunawakati maombi yako yanakuwa yanaudhaifu fulani na kushindwa kufikia viwango ambavyo Mungu anavikusudia kwako .


🖊 Tambua kwamba kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake amefanyika hivi

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa *kufanyika watoto wa Mungu* , ndio wale waliaminio jina lake;


Yohana 1:12



🖊 Umefanyika kuwa mwana wa Mungu .


✍ Baada ya kufanyika kuwa mtoto wa Mungu ukapewa uwezo yaani nguvu zitakazokusaidia kupigana .


🖊 Mungu amekuona wa maana saana kwahiyo alikupa nguvu za kiroho kwasababu adui

Yaani shetani anafanya vita na wote wanaomwamini Yesu Kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yao .


🖊 Ndyo maana neno linasema

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Waefeso 6:12



✍ Maana yake adui anapambana nasi kiroho .


✍ Mungu hajaishia hapo tu pia alikupa silaha ,yaani neno lake

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.


Waefeso 6:11

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.



Waefeso 6:13

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;


Waefeso 6:17


✍ Pia akasema kwamba


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?


Yeremia 23:29


✍ Siyo tu ni kama moto pia neno la Mungu ni nyundo ivunjayo vipandevipande.


✍ Hajaishia pale akaendelea kusema kwamba yeye ni mkombozi wako na kiongozi wako pia .

Soma hapa

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.


Isaya 48:17


✍ Sasa huyu Mungu anataka toba kwanza kabla ya kuingia vitani .


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Isaya 1:16

17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Isaya 1:17

18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Isaya 1:18

19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya 1:19



✍ Baada ya toba anataka uite nguvu ya Roho wake Mtakatifu

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Warumi 8:26



✍ Pia anataka ujifunike kwa damu ya Yesu wewe na kila kitu ulichonacho .
Achilia damu ya Yesu kwenye eneo unapofanyia maombi .

✍ Pia Mungu anataka uamini kuwa anaweza kufanya jambo kwako .


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

📖 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.


Luka 1:37

✍ Kisha imekupasa uombe chochote utakacho Mungu atakupa / kujibu


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


📖 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yohana 14:14



Mungu akubariki saana


Nakutakia tafakari njema

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*