UHUSIANO ULIOPO KATI YA TOBA NA UTAKATIFU NA SADAKA AITOAYO MTU 💒*

 UHUSIANO ULIOPO KATI YA TOBA NA UTAKATIFU NA SADAKA AITOAYO MTU 💒*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



Bwana Yesu asifiwe


✍  Jana tuliangalia maana ya toba na utakatifu .

✍ Leo naomba tuangalie uhusiano kati ya toba ,utakatifu na Sadaka .


✍ Nikukumbushe tu kwamba Mungu ili aweze kuikubali sadaka yako lazima uwe msafi .


✍ Usafi huu ninaousefa ni usafi wa mwili na roho yaani Utakatifu .

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


💻 11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.


Isaya 1:11

12 Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?


Isaya 1:12

13 Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.


Isaya 1:13



 💻 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;


Isaya 1:16

17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.


Isaya 1:17

18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Isaya 1:18

19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


Isaya 1:19



💻 8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.


Mithali 15:8

9 Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.


Mithali 15:9



💻 20 Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na uudi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.


Yeremia 6:20



 💻 22 Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.


Amosi 5:22



✍ Toba na Utakatifu ni njia pekee inayomfanya Mungu aikubali sadaka yako .


✍ Unaweza ukawa unanung'unika kwanini unatoa sana lakini hubarikiwi .


✍ Chunguza vizuri uhusiano wako na Mungu .


✍ Kaa ujihoji , hivi maisha ninayoishi ni ya kumpendeza Mungu ❓


✍ Kama maisha yako hayampendezi Mungu hawezi kupendezwa na sadaka yako pia .



✍ Lazima uishi maisha ya kiroho ya viwango ambavyo Mungu anataka uishi .


✍ Uishi maisha ya toba na Utakatifu yaani ni kuachana na kutenda maovu .


✍ Lazima ukikubali kumpendeza Mungu ukubali gharama ya kupunguza marafiki wanaokuvutia kwenye uovu .


✍ Hii itamfanya Mungu akupende na ataikubali sadaka yako .


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


💻 1 Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Zaburi 20:1

2 Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.

Zaburi 20:2

3 *Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.*

Zaburi 20:3


✍ Ili Mungu apendezwe na sadaka yako tafta kwanza apendezwe na wewe .


✍ Akipendezwa na wewe ataikubali sadaka yako .


✍ Je , atapendezwaje na wewe bila kudumu katika kuishi maisha ya toba na Utakatifu ❓


🖊 Hawezi kupendezwa na mtu asiyetaka kutubu yaani kutubia dhambi zake .



✍ Kuna wakati watu hukiri matari huu wakiwa wanasali


👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻


💻 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.


Mathayo 6:12



🖊 Huu mstari wengi huusema kimazoea tu lakini hawajasamehe kabisa .


✍ Kutokusamehe ni uchafu mbele za Mungu yaani huondoa Utakatifu .

🖊 Usitoe sadaka kama hujasamehe maana haitakubaliwa na Mungu wako kabisa .


 💻 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.


Mathayo 5:24



🖊 Maisha ya toba na Utakatifu ni maisha ya kuwa na amani na watu wote .

🖊 Kupatana na mliyekoseana ni kanuni ambayo Mungu anaiangalia ili aikubali sadaka ya mtu aitoaye .



✍ Kuna mengi sana ya kuandika lakini naomba niishie hapa kwa leo .


✍ Kumbuka toba na Utakatifu ndyo inamfanya Mungu aikubali sadaka yako .




Mungu akubariki sana ,nakutakia tafakari njema .



💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒💒

Maoni

  1. Kama mtu amemkosea nabii anafaa atoe sadaka au dhabihu kiasi gani?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*