VIGEZO VYA KUFANYIKA KIELELEZO MBELE ZA MUNGU

*✝ VIGEZO VYA KUFANYIKA KIELELEZO MBELE ZA MUNGU ✝*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


πŸ’» Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.


1 Timotheo 4:12



πŸ–Š Ili kijana Mkristo awe kielelezo lazima aishi kwa kufuata yafuataya

πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»


✍ Usemi wake uwe mzuri

Asiwe na majibu ya kiburi kwa watu wote .Ajue jinsi ya kumjibu kila mtu kwa hekima , busara ,na upole .

πŸ’» Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.


Wakolosai 4:6



✍ Mwenendo au tabia yake na matendo yake yampendeze Mungu .

Usemi wake na mwenendo wake viambatane .Kama anakemea zinaa huku mwenyewe anaishi maisha hayo kwa siri atakosa kielelezo kwa Mungu .


✍ Aishi maisha kuwapenda watu wote .Upendo ni amri kuu ya Mungu .



✍ Ailinde imani yake .Yaani aisimamie imani yake adumu katika maombi asije akaanguka.

πŸ’» Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.


1 Wakorintho 16:13


Kijana asimame imara asiyumbishwe na adui .


✍ Azingatie usafi ( Utakatifu ) wa mwili na roho

Zaburi 119:9

1 Wakorintho 7:32, 34




Mungu akubariki sana



🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂🚢🏻‍♂

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*