JIWEKE TAYARI

🖊 *JIWEKE TAYARI* 🖊



Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829





💻 _40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.

Luka 12 :40

Bwana Yesu Kristo apewe sifa


Neno la Mungu linatukumbusha kwa habari ya kujiweka tayari mimi na wewe .

🖊 Ni vema tutambue kwamba kujiweka kwetu tayari hakupo kufanya maandalizi ya kimwili .


🖊 Hapa tunatahadharishwa kwa habari ya kudumu sana katika utakatifu maana hatujui siku wala saa ajapo Yesu Kristo kuwahukumu walio hai na wafu .


🔰 Kuna wakati tunatakiwa kujua kwamba ujio wa Yesu ni sawa na kifo mtu hawezi kujua kufa kwake ni mda gani yaani ni saa ngapi atakufa .

Apataye ajali na kufa papo hapo alikuwa hajui kama atakufa kwa ajali .


🖊 Mungu anatutaka tufanye maandalizi maana hata kufa kwetu hatujui .


🖊 Sasa kama kesho yetu ni fumbo je tukifa tukiwa hatujatubu mwisho wetu ni upi❓


🔰 Nataka nikwambie wewe rafiki yangu na ndugu yangu katika Yesu Kristo kwamba usiishi na dhambi unajua ni dhambi ukisema uendelee kuitumikia baadaye utatubu maana hujui saa ,siku ,mwezi wala mwaka wa kufa kwako yaani kutoweka hapa duniani .


🔰 Je ,kama ukikaa na dhambi na ukafa kabla ya kutubu sehemu yako itakuwa wapi rafiki yangu ❓Nafikiri jibu umelipata .



🔰 Kumbuka ndugu yangu katika Yesu Kristo kwamba duniani tunasafiri kwahiyo jihoji hili

👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇

HIVI NIKIFA LEO SIKU YA HUKUMU NITAWEKWA UPANDE GANI KULINGANA NA NIYATENDAYO ❓


🖊 Jiulize utawekwa kwenye uzima wa milele au jehanamu ?


🔰Mungu anakutaka leo hii ujiweke tayari umpendeze yeye ili uwe na uzima wa milele .


🖊 Usiishi na DHAMBI ukisema utatubu utafakari mwisho wako baada ya kutoweka hapa duniani usije ukatoweka kabula hujazitubia DHAMBI zako ukaenda motoni .



TUOMBE


Mungu uishiye milele na kutawala mbinguni na duniani  .Nalitukuza jina lako kwaajili ya uhai wa watoto wako uwakumbuke wakajiweke tayari kila saa kwa msaada wa Roho Mtakatifu wakadumu katika maisha ya toba na utakatifu ili wakapate kuurithi uzima wa milele siku ya mwisho utakapokuja kuwahukumu walio hai na wafu na kuwalipa kwa kadri ya matendo yao .

Ninaomba Roho Mtakatifu akawasaidie katika kukupendeza wewe kila saa katika jina la Yesu Kristo nawakabidhi mikononi mwako .Amen

MUNGU AKUBARIKI SANA



https://peterfrancismasanja.blogspot con

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*