MOYO WA MWANADAMU

Moyo wa mwanadamu ni kama shamba ambalo inawezekana hilo shamba lina vichaka au magugu au mawe au visiki n.k
Lakini shamba hilo likisafishwa huwa shamba safi. Hata shamba lolote lazima liwe linasafishwa kila baada ya muda ndipo litabaki kuwa shamba safi.
Na moyo wa mwanadamu nao kama shamba unahitaji kusafishwa ili uwe safi.
Kuna njia njia mbili za kusafisha moyo yaani kutubu na kuacha dhambi.
Maombi ya toba husafisha moyo ili yasiyotakiwa moyoni yatoke.
Moyo kama shamba hauhitaji kusafishwa Mara moja tu Bali usafi unatakiwa uwe wa kila Mara ndipo moyo kama shamba utapaki safi siku zote.
Hakikisha katika maisha yako unahusika sana na maombi ya kutubu kisha jitenge siku zote na maovu.
Zaburi 51:1-2 " Ee MUNGU, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu."

Ukipanda mbegu katika shamba chafu ujue mbegu hiyo haitaota au itaota lakini haitastawi.
Toba katika KRISTO YESU ni ya muhimu sana.
Hatutubu ili tukaendelee na dhambi kisha tutatubu tena bali tunatubu ili tuendelee kuwa safi huku tukijitenga daima mbali na dhambi.
Katika maisha yako hakikisha unakuwa mtu wa kutubu.
Dhambi ni uchafu, dhambi huchafua moyo, toba inasafisha moyo.
Ni muhimu sana kutubu.
Kuna baraka huwezi kuzipata kama moyo wako ni mchafu hivyo toba inahitajika sana kwako.
Ukitubu na kuwa safi MUNGU anaweza kupanda mbegu njema ndani yako zitakazozaa baraka.
Mbegu ni Neno la MUNGU na Neno hilo linatakiwa kupandwa katika shamba (moyo) safi.
Ndugu unaweza kuingia kwenye maombi hata wakati huu.
Ukitaka ufanikiwe katika Maombi yako ya mahitaji tanguliza kwanza toba.

1. Tubu kwa ajili ya kilichosababisha tatizo kwako kisha ndio uombe katika jina la  YESU KRISTO ndipo tatizo litatoka.

2. Tubu kwa ajili ya misingi mibovu ya ukoo wako au familia yako iliyopelekea vifungo vya giza kufuatilia maisha yako.

3. Tubu kwa ajili ya dhambi zako mwenyewe.

Tubuni na mrejee kwa YESU KRISTO ndipo wakati wa mema utawafuata(Matendo 3:19)

MUNGU akubariki Sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*