NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA
💪🏻 NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA
SIKU YA KWANZA
Mwl Peter Francis Masanja
0679392829
UTANGULIZI
✍🏻 Katika somo hili kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake aweze kujisimamia mwenyewe akitumia jina na damu ya Yesu Kristo kushinda nguvu na ufalme wa giza
✍🏻 Kuna wakati mtu anatafta msaada wa kuombewa ombewa halafu yeye haombi anasubiri aombewe na kumwuliza mwombaji majibu ya maisha yake.
✍🏻 Hii ni mbaya sana kushindwa kujisimamia mwenyewe katika maombi
✍🏻 Nataka nikwambie kwamba ukimpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako umetangaza vita na shetani
✍🏻 Kwahiyo ili shetani asikunase na mitego yake lazima uvae silaha kuu zifuatazo.
1⃣ Neno
2⃣ Jina na damu ya Yesu
3⃣ Utakatifu
4⃣ Bidii,katika,maombi
✍🏻 ,Haya ni mambo unatakiwa kuyazingatia sana baada ya kumpokea Yesu
✍🏻 Lakini sasa tuangalie jambo la pili hapo juu
2⃣ Jina na damu ya Yesu
✍🏻 Tuangalie namna ya kujisimamia mwenyewe ukitumia jina la Yesu kushinda ufalme wa giza
Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.
Ezekieli 2:1
✍🏻 Mungu anataka usimame mwenyewe ili aseme na wewe
✍🏻 Anataka usimame katika maombi ukitumia jina na damu ya Yesu Kristo
✍🏻 Basi napenda tujifunze kwanza Yesu ni nani hasa
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Isaya 9:6
YESU ANATAMBULIWA KWA MAJINA HAYA 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
🖊 Mshauri wa ajabu
.🖊 Mungu mwenye nguvu
🖊 Baba wa milele
.🖊 Mfalme wa amani
🖊 Mungu pamoja nasi yaani Immanueli
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Mathayo 1:23
Tomaso akajibu, akamwambia, *Bwana wangu na Mungu wangu* !
Yohana 20:28
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto wa kiume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Isaya 7:14
🖊 Ni mwana wa Mungu
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
.
Yohana 3:16
Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Mathayo 28:19
🖊 Yesu ni neno
Tunamshinda shetani kwa damu ya Yesu na neno huyu neno ni Yesu pia
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1:1-4
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
1 Yohana 5:8
🖊 Yesu ni BWANA
Naye akiisha kusema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona *Bwana* .
Yohana 20:20
🖊 Yesu ni mpakwa mafuta
✍🏻 Jina lake lina upako
✍🏻 Kazi ya upako ni kuvunja kazi za ibilisi na kufukuza majeshi ya pepo wabaya pamoja na kumweka mtu huru kutoka kwenye mateso au nguvu za mauti
✍🏻 Jina hili yaani Yesu Kristo wa Nazareti likitajwa shetani na mawakala zake hutetemeka na kukimbia
✍🏻 Kwahiyo hauhitaji vitu vingine viitwavyo vinaupako tumia jina la Yesu Kristo ndyo lenye upako mkuu sana
✍🏻 Usinunue upako msogelee Yesu akupe upako na muujiza wako kupitia kuomba kwako
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Isaya 61:1-3
habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Matendo 10:38
✍🏻 Huhitaji jina lingine katika maombi maana hakuna jina litajwalo na kutetemesha ufalme wa giza isipokuwa jina la Yesu Kristo pekee.
✍🏻 Hili ndyo jina lenye upako pekee na usitafte vitu vya upako liite jina la Yesu Kristo
🖊 Yesu Kristo ni kuhani na mwombezi wetu
✍🏻 Hakuna jina lingine liwezalo kumfanya mtu asamehewe dhambi zake isipokuwa jina la Yesu Kristo pekee
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kafara ya upatanisho wa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
1 Yohana 2:1-2
🖊 Jina la Yesu ni wokovu
✍🏻 Hakuna wokovu mwingine tofauti na kumpokea Yesu Kristo
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Matendo 4:12
Mungu akubariki sana karibu katika somo linalofuata.
Maoni
Chapisha Maoni