NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA💪🏻*
*🔰 NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA💪🏻*
SIKU YA PILI
Mwl.Peter Francis Masanja
0679392829
📖 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.
Ezekieli 2:1
🖊 Maranyingi ni vigumu sana kupokea majibu ya matatizo yako kama utategemea mtu asimame aseme na Mungu kwaajili yako .
🖊 Baada ya kifo cha Yesu Kristo pale msalabani ,Mungu alimimina Roho Mtakatifu kwa kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake .
🖊 Kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake amepewa mamlaka ya kiroho endapo atasimama imara katika maombi akilitumia jina la Yesu Kristo wa Nazareti .
🖊 Katika somo lililopita tuliona maana ya jina la Yesu Kristo na uweza lililobeba ndani yake.
🖊 Leo tuangalie mamlaka iliyobebwa na hili jina la Yesu .
1⃣ MAMLAKA JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA NA NGUVU ZA GIZA
✍🏻 Mungu wetu ni mkuu sana na anatupenda sana kwa upendo mkuu sana.
✍🏻 Mungu alipomtoa Yesu Kristo afe kwaajili ya dhambi zetu alikuwa na maana ya kurejesha mamlaka ya kiroho kwa mwanadamu .
✍🏻 Aliona kwamba amtume Yesu Kristo na akampa jina kuu kupita majina yote na lenye mamlaka kupita majina yote .
📖 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. *ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi* ; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Wafilipi 2:8, 10-11
✍🏻 Jina la Yesu Kristo ni kuu sana na kila mtu aliyelipokea akiomba kwa kulitumia kwa imani yaani asiwe na mashaka ataushinda ufalme wa giza .
✍🏻 Ukiwa na jina la Yesu Kristo unamamlaka ya kuyaambia mapepo yafunge kinywa na kutoweka maana biblia inasema kila goti litapigwa mbele ya jina la Yesu Kristo .
✍🏻 Unapokuwa kwenye maombi hasa usiku wa manane unatakiwa kuamuru majeshi ya pepo wabaya yaliyotumwa kwako yapige magoti na kuyaamuru kusimama kurudi kwa waliyoyatuma katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti .🔥🔥🔥
✍🏻 Kumbuka wewe uombaye kupitia jina la Yesu Kristo unamamlaka mbinguni na duniani .
📖 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, *Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.*
Mathayo 28:18 SUV
✍🏻 Yesu Kristo aliyewa mamlaka alituachia mamlaka pia
📖 Akawaita wale Kumi na Wawili, *akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote* na kuponya maradhi.
Luka 9:1 SUV
✍🏻 Mamlaka aliyowapa Yesu Kristo wanafunzi wake ni kuu sana .
✍🏻 Hii ni pamoja na jina lake lenye upako na mamlaka kupita majina yote.
📖 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; *kwa jina langu watatoa pepo* ; watasema kwa lugha mpya;
Marko 16:17
✍🏻 Pepo hawezi kumtoka mtu kwa kutaja jina tofauti na jina la Yesu Kristo.
✍🏻 Kwa jina la Yesu mapepo hutoweka na kukimbia.
✍🏻 Kwa jina la Yesu , ufalme wa giza unakosa amani.
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, *akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza* magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 10:1
Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, *akawapa amri juu ya pepo wachafu* ;
Marko 6:7
Akawaita wale Thenashara, *akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.*
Luka 9:1
✍🏻 Katika Marko 16:17 tunaona biblia inasema kila aliaminiye jina la Yesu amepewa mamlaka juu ya pepo wabaya mamlaka hiyo imo ndani ya jina la Yesu pekee .
✍🏻 Katika biblia tunaona mapepo yanavitu vya kusimamia katika maisha ya mtu ya kiroho na kimwili pia .
✍🏻 Kuna mapepo mtu hutumiwa na mawakala wa shetani yaani wachawi au washirikina ili kuharibu afya yake .
✍🏻 Afya ni kitu cha msingi kwa mwanadamu na akili ipo kwenye afya
✍🏻 Kuna watu walikuwa na akili timamu walitumiwa pepo la wazimu wakawa watu wa kula jalalani hawajitambui kabisa.
✍🏻 Wengine makao yao yamekuwa makaburini kama hivi
👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
📖 27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini.
Luka 8 :27
28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese.
Luka 8 :28
29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo.
Luka 8 :29
30 Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.
Luka 8 :30
31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.
Luka 8 :31
32 Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.
Luka 8 :32
33 Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.
Luka 8 :33
Nataka nikwambie kwamba wewe uliyelibeba jina la Yesu Kristo unamamlaka lakini inawezekana umekosa imani tu ndyo maana tatizo dogo unapiga simu kwa mchungaji wako akuombee .
Namwomba Mungu akupe imani ya viwango vya juu sana uweze kulitumia jina la Yesu Kristo kushinda nguvu za shetani .
✍🏻 Naomba nikwambie kwamba mapepo yanalijua jina la Yesu Kristo hata kabla hujaanza maombi kama umembeba Yesu sawasawa utaona yanapiga kelele .
✍🏻 Mungu akusaidie usiwe na mashaka kama hawa watu 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
📖 13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
Matendo ya Mitume 19 :13
15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
Matendo ya Mitume 19 :15
16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Matendo ya Mitume 19 :16
✍🏻 Watu hawa walikuwa hawana imani katika jina la Yesu Kristo ndyo maana pepo aliwashinda .
✍🏻 Mamlaka ya jina la Yesu Kristo juu ya pepo wabaya inategemea imani ya mtu isiyo na mashaka .
✍🏻 Unaweza ukawa unamwonya mume wako au mke wako aache uzinzi lakini kuacha ameshindwa .
🖊 Tambua kuwa huyo anapepo la uzinzi unatakiwa umwombee sana ili awekwe huru .
🖊 Pepo la uzinzi lipo kwajili ya kuharibu uchumi wa mtu na kumkosesha mtu kuurithi uzima wa milele .
🖊 Nataka nikwambie kwamba usimchoke mwenzi wako kikubwa funga na kuomba juu yake .
Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake hivi 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
📖 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Mathayo 17 :18
19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema *Mbona sisi hatukuweza kumtoa* ?
Mathayo 17 :19
20 Yesu *akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu* . Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Mathayo 17 :20
21 [Lakini namna hii haitoki *ila kwa kusali na kufunga* .]
Mathayo 17 :21
Mume wako au mke wako anasumbuliwa na pepo la zinaa usimwache unatakiwa kufunga na kuomba kamata akili yake na moyo wake ukinyunyizia damu ya Yesu Kristo kisha amuru pepo la zinaa limtoke katika jina la Yesu Kristo. Jina lipitalo majina yote .🔥🔥🔥🔥🔥
🏻 Mambo haya matatu yatakufanya uwe tishio kwa shetani na mawakala zake.
1⃣ Imani
2⃣ Jina la Yesu
3⃣ Kufunga na kuomba
Ili mamlaka ya jina la Yesu Kristo ifanye kazi ndani yako unahitaji ufunge na kuomba pia uliamini jina la Yesu Kristo na uweza wake.
✍🏻 Usiliamini jina la Yesu Kristo peke yake tu bali unatakiwa kuamini pia uweza wa jina lake .
🔥 Katika jina lipitalo majina yote .Jina lenye nguvu kupita majina yote .Jina lenye mamlaka kupita majina yote .Jina ambalo kila goti kitapigwa na kila ulimi utalikiri .Jina lenye uponyaji na liowezalo kuokoa .Jina la Yesu Kristo wa Nazareti .Ninaamuru nguvu za giza na majeshi ya pepo wabaya yaachie maisha yangu 🔥🔥🔥🔥🔥
✍🏻 Mchukulie Yesu viwango vya juu sana 💪🏻💪🏻💪🏻💪🏻💪🏻
✍🏻 Ile kwamba kuna mtu mshirikina anakusumbua tambua kuwa anapepo ndani yake yaani ni roho chafu .
🔥 Tumia jina la Yesu Kristo kuishughulikia hiyo roho ikaayo ndani yake .
🔥 Wewe ni shujaa unalindwa na nguvu za Mungu .
✍🏻 Unatakiwa kujua kwamba waganga wa kienyeji pia wanapepo .Yaani pepo la uaguzi na utambuzi .Shughulikia hayo mapepo ikiwa katika familia au ukoo wenu kuna mtu wa aina hiyo .
👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻
📖 16 Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na *pepo wa uaguzi* akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
Matendo ya Mitume 16 :16
17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.
Matendo ya Mitume 16 :17
18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, *Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile* .
Matendo ya Mitume 16 :18
✍🏻 Paulo alimwamuru pepo wa uaguzi kwa jina la Yesu Kristo akamtoka.
Kwahiyo litumie jina la Yesu Kristo juu ya pepo wa ushirikina wanaosumbua watu au eneo fulani .
🏻 Umeugua ugonjwa madaktari wanapima hawaoni chochote lakini unaumwa sana .
✍🏻 Kumbuka kwamba mapepo yanaweza kutumwa kwako kuja kusimamia gonjwa fulani
✍🏻 Mbaya sana mapepo hayaonekani kwenye vipimo na hakuna dakitari aliyesomea mapepo isipokuwa dakitari ni Yesu Kristo ukilitaja jina lake mapepo pamoja na ugonjwa waliousimamia utaondoka.
✍🏻 Kumbuka yule mama aliyetokwa damu miaka mingi na madaktari walishindwa kumtibu huo haukuwa ni ugonjwa wa kawaida walikuwa ni pepo walisimamia huo ugonjwa lakini alipokutana na Yesu Kristo yale mapepo yakatoka pamoja na huo ugonjwa
Nakuombea kwa Mungu akupe nguvu na jina la Yesu Kristo na uweza wake pamoja na imani vikae ndani yako .
Mungu akubariki karibu katika somo linaloendelea siku nyingine
Maoni
Chapisha Maoni