HUDUMA NI NINI*

🖊 *HUDUMA NI NINI* ❓


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



Huduma ni kazi ambayo mtu kapewa na Mungu aifanye kwa uongozi wa Roho Mtakatifu  kwaajili ya kuwafanya watu wamjue Mungu na kudumu katika maisha matakatifu ili wawe na uzima wa milele .

🖊 Huduma ni kazi apewayo mtu na Roho wa Mungu ili apeleke ujumbe wa Mungu kwa watu .


🖊 Mfano

1⃣ Utume

2⃣ Unabii

3⃣ Uchungaji

4⃣ Uinjilisti


5⃣ Ualimu


📖 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

1 Wakorintho 12 :5

28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, *wa kwanza mitume* , wa *pili manabii* , *wa tatu waalimu,* kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.

1 Wakorintho 12 :28

29 Je! *Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu?* Wote wanatenda miujiza?

1 Wakorintho 12 :29


🖊 Huduma ni kazi ya Kiroho


📖 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;


Waefeso 4:11


🖊 Huduma ni wito ambao mtu huitwa na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwake.


📖 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Yeremia 1 :5


🖊 Mungu alimjua Yeremia tangu tumboni mwa mamaye .


🖊 Pia alimjua Yohana tangu tumboni mwa mamaye


📖
13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
Luka 1 :13

14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
Luka 1 :14

15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
Luka 1 :15

16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.
Luka 1 :16

17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.
Luka 1 :17


Mungu akubariki sana

🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*