KIBALI NA WITO

*🖊 KIBALI NA WITO* 🖊


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

SAUTI YA MUNGU MINISTRY


🖊 Bwana Yesu Kristo apewe sifa .

🖊 Leo tuangazie tofauti kati ya kibali na wito .


📖 7 *Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.*

Mwanzo 4 :7


🖊 Tunamwona Kaini hakubarikiwa na Mungu kwa sababu hakutenda vema yaani sadaka aliyoitoa haikuwa njema kwa Mungu .


🖊 Kibali ni majibu ya chanya ya kile ukiombacho mbele za Mungu .

🖊 Kibali ni baraka ambayo mtu anaipata kutoka kwa Mungu..

🖊 Kibali ni matokeo mazuri ya kitu ambacho mtu kakiomba kuonyesha kuwa maombi yake yamekubaliwa .


🖊 Kaini hakupata majibu ya maombi yake kwa sababu sadaka yake haikumpendeza Mungu .

🖊 Vivyo hivyo hata leo watu hawapati majibu ya maombi yao yaani kibali kwasababu ya dhambi au kutokujua kuomba .


🖊 WITO

Wito au kuitwa na Mungu ni kitendo cha Mungu kumweka mtu kwaajili ya kutimiza kusudi au kufanya kazi  fulani akiwepo hapa duniani .


Yeremia aliitwa kuwa nabii .Alipewa kazi hiyo na Mungu aifanye .

📖 *5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.*

Yeremia 1 :5


🖊 Mtu aliyeitwa na Mungu ,Mungu humfundisha nini cha kufanya .Na kile akifanyacho akifanya sawasawa na neno la Mungu .

🖊 Aliyeitwa huisimamia kweli ya Mungu hatafuata matakwa ya wanadamu bali ataliangalia neno .


Mungu akubariki


Install app yetu kupata masomo mengine

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*