SOMO KUHUSU KUZIMU

SOMO KUHUSU KUZIMU


 *SEHEMU YA KWANZA*



WATU WAKIFA, ROHO ZAO ZINAKUWA WAPI?


Biblia inasema kuhusu Bwana Yesu kuwa:👇👇

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; (Wafilipi 2:9-10).


✍Kulingana na mstari huu, tunagundua kuwa kuna sehemu kuu tatu:
                                                 Mbinguni
                                                 Duniani
                                                 Chini ya nchi


✍Mbinguni ni mahali aliko Mungu; duniani ni mahali tuliko sisi wanadamu tulio hai; na chini ya nchi ni mahali aliko ibilisi.


✍Tangu nyakati za Adamu kulikuwapo wanadamu wema na waovu. Wanadamu wema walikufa na waovu nao walikufa. Swali ni kuwa, je, walipokufa walienda wapi?


Mwinjilisti Luka anatupatia picha nzuri kutokana na kisa alichosimulia Bwana Yesu juu ya tajiri na Lazaro. Tunasoma katika Luke 16:22-26 👇👇


22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.


23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.


24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.


25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.


26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.


✍Tunachoona hapani kuwa Lazaro alikuwa ni mwenye haki kama Ibrahimu na tajiri alikuwa ni asiye na haki. Hawa walikaa sehemu mbili tofauti, maana zilitenganishwa na bonde. Sehemu hizi zote mbili zilikuwa chini ya nchi.


✍Kabla ya Yesu kufa, wanadamu wote walipokufa walienda chini ya nchi. Na huko kulikuwa na sehemu mbili – kwa shetani na kifuani mwa Ibrahimu. Katika habari hii ya tajiri na Lazaro – ambayo ilitokea zamani sana hata kabla ya Musa, Bwana Yesu anatuonyesha kuwa tajiri alikuwa kwenye mateso; na Lazaro alikuwa penye raha.


✍Lakini mtu anaweza kusema hivi, “Huoni kuwa tajiri aliinua macho yake? Je, hii si ishara kuwa Lazaro na Ibrahimu walikuwa mbinguni?


✍Wakati huo mbingu zilikuwa hazijafunguliwa kwa ajili ya wanadamu. Tuendelee kusoma na hapo mbele tutapata jibu la maswali hayo.

 0767103520

Mathiaselias27@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*