SOMO KUHUSU KUZIMU

SOMO KUHUSU KUZIMU

*SEHEMU YA PILI*




Bwana alipokuja duniani, akateswa na akauawa, tunaambiwa kuwa:


*Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri. (1Petro 3:18-19)*


✍Mbinguni hakuna vifungo; vifungo viko chini ya nchi. Kwa hiyo, Bwana alienda kuwahubiria waliokuwa kifungoni.


✍Bila shaka hii ndiyo sehemu ambayo Wakatoliki huita toharani. Sehemu hii ilikuwapo zamani kama makao ya muda kwa wale waliokufa kabla ya Kristo. Humo waliwekwa kungojea ukombozi wa mwanadamu ufanye na Kristo. Lakini sasa hivi haipo tena.


✍Maana ya andiko hili katika Petro ni kuwa, wale waliokuwa kifuani mwa Ibrahimu (au tuseme toharani), Bwana alienda akawahubiria katika zile siku tatu alipokuwa katika tumbo la nchi.


*Je, baada ya kuwahubiria, nini kilifuata?*


Imeandikwa:
*Hivyo husema, alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? (Efe 4:8)*


✍Shetani alikuwa amewashikilia wanadamu wote kuzimu, lakini Bwana akaenda akawateka na kuondoka ndao. Na ndiyo maana kabla Bwana hajafa, alisemaπŸ‘‡πŸ‘‡


*Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. (Mathayo 12:29)*


✍Na ushahidi wa jambo hili uko wazi kwa sababu Biblia inatuambia kwamba baada ya Bwana kufa, watakatifu waliokuwa wamekufa zamani walionekana Yerusalemu.

*Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. (Mat 27:50-53)*


*Je, alipoteka mateka aliwapeleka wapi?*


Imeandikwa kuhusu yule mwizi aliyesulubiwa pamoja na BwanaπŸ‘‡πŸ‘‡

Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami *peponi.* (Luka 23:42-43)

✍Ukisoma kwenye Kiingereza, imeandikwa hivi: And Jesus said unto him, Verily I say unto thee, To day shalt thou be with me in paradise. Peponi ndio *paradiso.*


*Paradiso si Yerusalemu Mpya.* bali  *Paradiso* ni makao ya muda kwa ajili ya watakatifu, kusubiria mwisho wa mambo yote ambapo Yerusalemu mpya itafunguliwa na kuwa makao ya milele pamoja na Bwana.


✍Kama ambavyo watakatifu wako kwenye makao ya muda paradiso, ndivyo ambavyo na wenye dhambi wako kwenye makao ya muda kuzimu aliko shetani sasa – maana shetani hayuko jehanamu bado. Yaani, wako kule alikokuwa yule tajiri aliyezungumza na Ibrahimu kuhusiana na Lazaro kutumwa duniani.


Pia tunasoma kuwa:
*Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. (2Petro 2:4)*

✍Hawa mashetani wako kifungoni lakini kumbe wala hiyo si hukumu bado. Ndiyo maana anasema wako pale hata ije hukumu. Itakapofika sasa mwisho wa mambo yote, ndipo kila mtu ataenda sasa kwenye makao ya milele.

Biblia inasema kuhusu wakati huo:
*Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; (Mat 25:34)*


*Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; (Mat 25:41).*


✍Kumbe moto wa milele ndiyo hukumu ya mwisho iliyotajwa hapo juu.


✍Hata tukisoma kwenye Ufunuo imeandikwa: *Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. (Ufu 21:8)*

      0767103520

Mathiaselias27@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*